BMT: Marufuku Simba Na Yanga Kubadili Umiliki, Zibaki Kwa Wanachama

BMT hawana ss wanchama tushaamua Simba tutaiendesha kwa mfomo share basi wawazie hao Yanga sio ss
 
Bado tuna safari ndefu sana kufikia mafanikio kwenye michezo ikiwa haya ndiyo mawazo ya viongozi wa baraza la michezo.
Hivi hili baraza huwa linatoa ruzuku kwa ajiri ya uendeshaji wa hivi vilabu? Eti hao matajiri waanzishe timu zao!!! Waingereza wangekuwa na mawazo hayo leo hii vilabu kama chelsea visingekuwa na fan base waliyonayo leo hii
 
Hivi BMT wanasaidia nini kwenye mchezo wa soka? Navyojua serikali haina mamlaka ya kuingilia mchezo wa soka, hawa BMT kama ndege hawalimi Ila wanakula, wanachukua gawio la viingilio kila mechi inapochezwa.
 
Kuna wazee wanatia aibu taifa. Sijui wamesomea wapi.
Akili za kimasikini sana.
 
Na wasiruhusiwe mikutano ya ndani na nje kama vile NCCR..CHADEMA....CUF (MAALIM SEIF)
 
Hivi kuna watu bado wanaona hao jamaa wanavyotaka kuzichukua hizo timu ndo zitapata maendeleo?? Yaani mtu kakufadhili kwa miaka kadhaa tu anakwambia nataka kukodi timu ila kuna deni la bil.11 kweli? Mwingine alikuwa na Timu yake akamuuzia Zamunda eti haina fans,kwani huwez itengeneza ikawa na Fans,mbona Bakhresa ameweza??
Hawa wafanyabiashara wetu wanapenda miteremko hapo washaona vichaka wanataka kupiga!!! Mi nawaunga mkono BMT hao Simba na Yanga wajipange upya kama wanataka maendeleo hasa kujipanga kwenyewe kuanzie kwe katiba!!!
 
Mbona BMT wameongea kitu cha maana tu? Hawajazuia nani awe mmiliki, wanachotaka ni taratibu za kisheria zifuatwe.

Mambo yasipodhibitiwa mwanzoni hivi, yakija kuharibika ni sisi sisi tutakaoilaumu BMT kwamba ilikua wapi wakati mikataba ya kidhalimu inasainiwa?
Ni sisi tutakaoishutumu BMT kuwa imepewa 'takrima' ndio maana imefumbia macho sakata ya umilikishwaji Yanga.

Tufikirie kwa umakini sana.
 
Kuongoza timu mpaka kufikia deni la Bilion 11 ndo usimamizi mzuri???
tunahamu sana ya kufikia maendeleo lakini siyo kwa njia hii
Yale Maghorofa yanayojengwa na serikali pale UDSM kama Hostel, yanacost 10b Tshs tu wanafunzi karibia 4000! So kama YANGA inadaiwa 11 b na gabachori na Kaunda hakuna hata nyasi ! World wonder!
 
Nchi imepatwa na ugonjwa mbaya sana. Ugonjwa wa kukataa kufikiri.

Hivi kipi hamjakielewa kwa BMT. Wao washasema, tatizo ni katiba za Simba na YANGA.

BMT wameenda mbali zaidi na kushauri Simba na YANGA zianze kwa kubadilisha katiba zao kwanza. Mbona iko wazi hii.

Watu wa Simba na YANGA mnaleta mambo kama ya Burundi. Walipojiunga ICC, walipewa na katiba. Hawakuisoma. Ghafla wanakurupuka kujitoa. Wakaambiwa someni katiba kwanza. Kurudi kuisoma aibu.

Wenye macho na akili zao waliyaona haya pale YANGA zamani sana. Wakataka kuanzisha kampuni, wenyewe wanachama wakaleta unafiki, wakaikataa kampuni.

Leo tena washasahau. Kinachotokea leo YANGA ni matokeo ya kuikataa Yanga Kampuni.

Ajabu povu lote mnalipeleka kwa BMT. Mshasahau.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa uwejezaji ni muhimu sana katika uendeshaji wa soka la kisasa. Lakini uwekezaji huo ni muhimu kuendana na mpangilio wa utunzaji wa fedha wa kisasa (financial accouning). Pia umiliki wake uwe unajulika wazi. Kama kuna uhamishaji wa umiliki basi ijulikane anayetoa anapata faida gani kutoka kwa anayenunua. (Maelezo ya jumla kutoka kwa mnunuzi kuwa anadai 11b/= ni utata mtupu usiokubalika). Timu hizi zinataka kununuliwa bila kujulikana wauzaji watapata faida kiasi gani. Sio faida ya ushindi. Ushindi ni matokeo ya mchezo kwa kuwa mpaka sasa ushindi huwa unapatikana. Faida hapa ni ya kifedha, kwamba aliyecha senti 5 yake mwaka 1930 atapata faida gani ya kifedha leo ikiwa timu hiyo itauzwa.
Tukumbuke kuwa kuna tofauti ya uanzishaji wa club ya wanachama na ya uwekezaji. Timu nyingi za ulaya zilianzishwa na watu binafsi kwa lengo la uwejekaji na zimekuwa zikibadili wawekezaji kulingana na makubaliano. Mashabiki wanabaki palepale.
Yanga na Simba zilianzishwa sio kwa nia ya uwekezaji. Wanachama ndio ngao yao kuu. Kabla ya kuuza timu wajiuliza raslimali walizonazo sasa wanazitumiaje? Tuwaulize Simba kodi ya jengo lao wanaitumiaje. Fedha za tbl, vodacom n.k. zinatumikaji?
Inawezekanaje mtu huyo huyo ni mwenyekiti wa timu halafu ageuke tena kutaka kuinunua timu? Upande uleule uliomweka madarakani ndio anataka kuununua?
Kama wanataka uwekezaji kwenye soka waanzishe timu zao. Zikipata ushindi zitapata mashabiki.
 
Back
Top Bottom