BMT: Marufuku Simba Na Yanga Kubadili Umiliki, Zibaki Kwa Wanachama

Ni ukweli usiopingika kuwa uwejezaji ni muhimu sana katika uendeshaji wa soka la kisasa. Lakini uwekezaji huo ni muhimu kuendana na mpangilio wa utunzaji wa fedha wa kisasa (financial accouning). Pia umiliki wake uwe unajulika wazi. Kama kuna uhamishaji wa umiliki basi ijulikane anayetoa anapata faida gani kutoka kwa anayenunua. (Maelezo ya jumla kutoka kwa mnunuzi kuwa anadai 11b/= ni utata mtupu usiokubalika). Timu hizi zinataka kununuliwa bila kujulikana wauzaji watapata faida kiasi gani. Sio faida ya ushindi. Ushindi ni matokeo ya mchezo kwa kuwa mpaka sasa ushindi huwa unapatikana. Faida hapa ni ya kifedha, kwamba aliyecha senti 5 yake mwaka 1930 atapata faida gani ya kifedha leo ikiwa timu hiyo itauzwa.
Tukumbuke kuwa kuna tofauti ya uanzishaji wa club ya wanachama na ya uwekezaji. Timu nyingi za ulaya zilianzishwa na watu binafsi kwa lengo la uwejekaji na zimekuwa zikibadili wawekezaji kulingana na makubaliano. Mashabiki wanabaki palepale.
Yanga na Simba zilianzishwa sio kwa nia ya uwekezaji. Wanachama ndio ngao yao kuu. Kabla ya kuuza timu wajiuliza raslimali walizonazo sasa wanazitumiaje? Tuwaulize Simba kodi ya jengo lao wanaitumiaje. Fedha za tbl, vodacom n.k. zinatumikaji?
Inawezekanaje mtu huyo huyo ni mwenyekiti wa timu halafu ageuke tena kutaka kuinunua timu? Upande uleule uliomweka madarakani ndio anataka kuununua?
Kama wanataka uwekezaji kwenye soka waanzishe timu zao. Zikipata ushindi zitapata mashabiki.
hapo utasikia sisi Yanga malengo yetu na kumfunga Simba na Simba nao utawasikia tukimfunga Yanga tu kwisha......tuwekeze kwa hawa jamaa ili tufanikishe haya!
Nawaza tu kwa sauti!!!
 
Mzee Akilimali ameishinda pesa ya Manji. Manji Chaliiiii. Manji abwagwa na Akilimali (Hivyo ni vichwa vya habari kwenye kijiwe cha Yanga Bomba na Yanga Asili)!
Hii ina maana thamani ya hizo klabu kwa serikali ni zaidi ya unavyofikiri. Yawezekana serikali imewekaza sana kwenye hizo klabu na hakuna anayeweza kuzinunua. Hili ni jaribio la pili kwa wafanyabiashara kutaka kuzimiliki na ikashindikana.
Tatizo siasa zinatuharibu,we huoni kuna kasoro katika ukodishaji na umiliki wa hizi timu?? Na ni yale yale ushabiki kwa kwenda mbele??
 
Kitendo cha kuzuia timu hizo kuendeshwa ki kampunin.ni kuturudisha nyuma miaka hamsini na tano..yaani wanachama wamepigwa propaganda na wapinga maendeleo .humo humo siasa zimeingia yaaani upumbavu mtupu nchi ya watu wajinga sijapata ona
 
Kama unandoto za kuiona tanzania inapiga hatua katika mpira wa miguu basi utasubiri sana.Labda kizazi hiki kilichopo kiondoke chote.
 
alichosema kiganja upande wa yanga ni Kama mkulima ambae anajiandaa kuvuna halafu unamwambia usipanda mazao
 
Watu wa Simba na YANGA mnaleta mambo kama ya Burundi. Walipojiunga ICC, walipewa na katiba. Hawakuisoma. Ghafla wanakurupuka kujitoa. Wakaambiwa someni katiba kwanza. Kurudi kuisoma aibu.

Ningependa kujua zaidi hapo! Japo tuko kwenye sportsss!
 
Back
Top Bottom