bryan2
JF-Expert Member
- Jun 8, 2016
- 3,323
- 4,667
Kumekucha tena ni siku nyingine nzuri, wengi wanapenda kutumia hii kauli Soka letu tunalifahamu wenyewe au soka letu kivyetu vyetu.
Nimetizama mechi kadhaa za Yanga nakugundua pindi Yanga inapokutana na wachezaji iliowaacha na kwenda timu nyingine timu hizo wakikutana na Yanga wale wachezaji mwanzo mwisho ni kukaza.
Rejea mchezo wa Mashujaa hiyo jana Golikipa Johora alikua yupo radhi kufia kiwanjani ila Yanga isipite goli tu, angalia gemu na Namungo golikipa Dida Munishi alimwaga mchozi kabisa baada ya kufungwa pamoja na Pius Buswita aliyecheza Jihad mwanzo mwisho na mwenzake Domayo.
Mifano ni Mingi swali la kujiuliza je wanataka kuwaonyesha Yanga walifanya makosa kuwaacha au yanakua ni maelekezo kutoka kwa makocha wao.
Njoo sasa upande mwingine pale Simba asilimia kubwa ya wachezaji wanaoachwa na Simba wakienda upande mwingine ni ka vile bado wanakua wanatumika na Simba kuhujumu hizo timu rejea penalti ya Kagere na Singida Utd Kombe la mapinduzi jamaa ni kama alimpa mpira kipa, pia kipindi cha nyuma mchezaji Ulimboka aliwahi kushutumiwa kutumika kuwapa wachezaji wa timu pinzani mlungula ili waachie ushindi kwa Simba.
Sio wachezaji tu hata makocha rejea kocha wa Tabora Utd mserbia Karpunovic naye alipita Simba ajabu anashangaa na kusema kuna matukio yalitokea ndani ya masaa 24 kuonyesha kwamba kulikua na viashiria vya rushwa kwa wachezaji wake na kubaki kulalamikia nyasi ndefu wakati uwanja ni wao kila siku.