BMT: Marufuku Simba Na Yanga Kubadili Umiliki, Zibaki Kwa Wanachama

Nchi imepatwa na ugonjwa mbaya sana. Ugonjwa wa kukataa kufikiri.

Hivi kipi hamjakielewa kwa BMT. Wao washasema, tatizo ni katiba za Simba na YANGA.

BMT wameenda mbali zaidi na kushauri Simba na YANGA zianze kwa kubadilisha katiba zao kwanza. Mbona iko wazi hii.

Watu wa Simba na YANGA mnaleta mambo kama ya Burundi. Walipojiunga ICC, walipewa na katiba. Hawakuisoma. Ghafla wanakurupuka kujitoa. Wakaambiwa someni katiba kwanza. Kurudi kuisoma aibu.

Wenye macho na akili zao waliyaona haya pale YANGA zamani sana. Wakataka kuanzisha kampuni, wenyewe wanachama wakaleta unafiki, wakaikataa kampuni.

Leo tena washasahau. Kinachotokea leo YANGA ni matokeo ya kuikataa Yanga Kampuni.

Ajabu povu lote mnalipeleka kwa BMT. Mshasahau.
Umeona ndugu!! Unafiki huu wa watanzania kuendekeza ushabiki bila kufuata misingi ndo maana mpira hauendelei,hata hapa JF kila anayechangia anachangia kwa kueleza maslahi yake dhidi ya Simba ama Yanga namna hii hatuendi!!!!

Ukweli lazima usemwe ni kuwa Simba na Yanga rekebisheni kwanza katiba zenu ndo mambo mengine yafuate!!!
 
Wadau wakuu wa klabu ya mpira ni wanachama na mashabiki. Hawa wakiamua klabu iuzwe inauzwa tu BMT ikitaka isitake. Klabu ni mashabiki na wanachama. Klabu ipo kuburudisha mashabiki.
 
Mzee Akilimali ameishinda pesa ya Manji. Manji Chaliiiii. Manji abwagwa na Akilimali (Hivyo ni vichwa vya habari kwenye kijiwe cha Yanga Bomba na Yanga Asili)!
Hii ina maana thamani ya hizo klabu kwa serikali ni zaidi ya unavyofikiri. Yawezekana serikali imewekaza sana kwenye hizo klabu na hakuna anayeweza kuzinunua. Hili ni jaribio la pili kwa wafanyabiashara kutaka kuzimiliki na ikashindikana.
 
DUNIANI KOTE MFUMO WA MPIRA NI BIASHARA HAWA BMT WANAUMWA TRAKOMA

Naomba niwatetee BMT, nadhani wadau wengi hawaijui na labda hawajaisoma sheria ya michezo na ile iliyounda BMT pamoja na kanuni zake. Ni kupitia hiyo sheria ndipo vyama na vilabu vinapata usajili wake. Sasa basi, vyama vyetu na vilabu vingi viliundwa ktk mfumo wa ridhaa, si professional au kibiashara kama dunia inavyoenda sasa. Kama tatizo basi linaanzia kwenye sheria ya vyama na si uongozi wa BMT kama BMT au vilabu kama vilabu. BMT inatekeleza kile ambacho sheria ya michezo inataka. Ukiangalia hata umiliki wa vilabu, Katiba za vilabu hazioneshi mahala popote kwamba mtu mmoja anaweza kumiliki klabu isipokuwa klabu ni mali ya wanachama halali na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho kulingana na katiba waliyojiwekea wenyewe. Sasa basi kama Yanga au Simba wana mtazamo mpya, wanatakiwa kurudi kwenye katiba zao na kufuta vipengele vyote vinavyowabana, kisha ku-update kwa msajli wa vyama vya michezo hapo ndipo labda wanaweza kuwa na maamuzi wanayotaka kuyafikia sasa!

Hili ndio tatizo la kuwa na sheria za zamani katika nyakati ambazo nchi nyingi zimekwisha kubadilika!

Nawasilisha!

Simba wa nyika - Kaduguda!
 
BMT ni mbovu IVUNJWE TU HAKUNA NAMNA,WE WANT TO GO AHEAD ON FOOTBALL,KWA KASI YA RAIS WETU, MABWANA HAWA PAMOJA NA VIBABU VYAO VICHAWI HAWATAKI MAENDELEO KILABUNI../
• NI TABIA YA WACHAWI KUTOPENDA KITU MAENDELEO.../
CHUNGUZENI....!?!

Si kweli, hebu tafuta sheria ya BMT uisome uone kama kweli BMT ni wachawi wa michezo au sheria yetu ndio tatizo?
 
Naomba niwatetee BMT, nadhani wadau wengi hawaijui na labda hawajaisoma sheria ya michezo na ile iliyounda BMT pamoja na kanuni zake. Ni kupitia hiyo sheria ndipo vyama na vilabu vinapata usajili wake. Sasa basi, vyama vyetu na vilabu vingi viliundwa ktk mfumo wa ridhaa, si professional au kibiashara kama dunia inavyoenda sasa. Kama tatizo basi linaanzia kwenye sheria ya vyama na si uongozi wa BMT kama BMT au vilabu kama vilabu. BMT inatekeleza kile ambacho sheria ya michezo inataka. Ukiangalia hata umiliki wa vilabu, Katiba za vilabu hazioneshi mahala popote kwamba mtu mmoja anaweza kumiliki klabu isipokuwa klabu ni mali ya wanachama halali na hao ndio wenye maamuzi ya mwisho kulingana na katiba waliyojiwekea wenyewe. Sasa basi kama Yanga au Simba wana mtazamo mpya, wanatakiwa kurudi kwenye katiba zao na kufuta vipengele vyote vinavyowabana, kisha ku-update kwa msajli wa vyama vya michezo hapo ndipo labda wanaweza kuwa na maamuzi wanayotaka kuyafikia sasa!

Hili ndio tatizo la kuwa na sheria za zamani katika nyakati ambazo nchi nyingi zimekwisha kubadilika!

Nawasilisha!

Simba wa nyika - Kaduguda!
Ndivyo inavyotakiwa kufanyika.
 
Hivi mtu anweza kukupangia jinsi ya kuiendesha familia yako? Wenye timu ndio wameamua timu zao zibadilishe mfumo wa uendeshaji.

Hakuna mtu anaweza kumpangia mtu namna ya kuendesha familia yake, lakini zipo taratibu ambazo jamii imejiwekea na ambazo inatarajiwa wewe kama Baba mwenye nyumba uzitekeleze. Usipofanya hivyo, pamoja na kwamba wewe ni Baba bado jamii inaweza ingilia kati. Kinachofanyika na vilabu hivi ni kinyume na Katiba zao hata kama lengo ni zuri. Kama ikiamriwa leo wapewe hizo timu waziendeshe, mambo yakiharibika huko mbele nani wa kulaumiwa? Ni wapi hawa mambwana wanabanwa na sheria au kanuni za vilabu? Okey, nini nafasi ya wanachama walioanzisha na kuunda hivyo vilabu? Katiba zinasema wenye maamuzi ya mwisho ni wanachama. Zikichukuliwa na mtu binafsi, je bado wanachama watakuwa na sauti?

Nadhani jambo rahisi tu, kama kweli wana nia ya kuendeleza michezo, kwa nini wasianzishe za kwao kama AZAM?
 
Umeona ndugu!! Unafiki huu wa watanzania kuendekeza ushabiki bila kufuata misingi ndo maana mpira hauendelei,hata hapa JF kila anayechangia anachangia kwa kueleza maslahi yake dhidi ya Simba ama Yanga namna hii hatuendi!!!!

Ukweli lazima usemwe ni kuwa Simba na Yanga rekebisheni kwanza katiba zenu ndo mambo mengine yafuate!!!

Na ndio mzaha mzaha kama huu, tunafanya hata katika mambo ya msingi mf. Uchaguzi Mkuu wa Rais.
 
Bado tuna safari ndefu sana kufikia mafanikio kwenye michezo ikiwa haya ndiyo mawazo ya viongozi wa baraza la michezo.
Hivi hili baraza huwa linatoa ruzuku kwa ajiri ya uendeshaji wa hivi vilabu? Eti hao matajiri waanzishe timu zao!!! Waingereza wangekuwa na mawazo hayo leo hii vilabu kama chelsea visingekuwa na fan base waliyonayo leo hii

Je unazifahamu sheria na kanuni zinazoendesha michezo kwenye nchi na timu ulizorejea? Sheria yetu ni Namba 12 ya mwaka 1967 na marekebisho yake namba 6 ya mwaka 1971. Sasa njoo uone sera ya michezo ni ya mwaka 1995. Hapo je, utalinganisha na nchi ambazo wana-update sheria zao mara kwa mara kulingana na mahitaji yanavyojitokeza?
 
Ni ukweli usiopingika kuwa uwejezaji ni muhimu sana katika uendeshaji wa soka la kisasa. Lakini uwekezaji huo ni muhimu kuendana na mpangilio wa utunzaji wa fedha wa kisasa (financial accouning). Pia umiliki wake uwe unajulika wazi. Kama kuna uhamishaji wa umiliki basi ijulikane anayetoa anapata faida gani kutoka kwa anayenunua. (Maelezo ya jumla kutoka kwa mnunuzi kuwa anadai 11b/= ni utata mtupu usiokubalika). Timu hizi zinataka kununuliwa bila kujulikana wauzaji watapata faida kiasi gani. Sio faida ya ushindi. Ushindi ni matokeo ya mchezo kwa kuwa mpaka sasa ushindi huwa unapatikana. Faida hapa ni ya kifedha, kwamba aliyecha senti 5 yake mwaka 1930 atapata faida gani ya kifedha leo ikiwa timu hiyo itauzwa.
Tukumbuke kuwa kuna tofauti ya uanzishaji wa club ya wanachama na ya uwekezaji. Timu nyingi za ulaya zilianzishwa na watu binafsi kwa lengo la uwejekaji na zimekuwa zikibadili wawekezaji kulingana na makubaliano. Mashabiki wanabaki palepale.
Yanga na Simba zilianzishwa sio kwa nia ya uwekezaji. Wanachama ndio ngao yao kuu. Kabla ya kuuza timu wajiuliza raslimali walizonazo sasa wanazitumiaje? Tuwaulize Simba kodi ya jengo lao wanaitumiaje. Fedha za tbl, vodacom n.k. zinatumikaji?
Inawezekanaje mtu huyo huyo ni mwenyekiti wa timu halafu ageuke tena kutaka kuinunua timu? Upande uleule uliomweka madarakani ndio anataka kuununua?
Kama wanataka uwekezaji kwenye soka waanzishe timu zao. Zikipata ushindi zitapata mashabiki.

Well explained Congo
 
Zilisajiliwa kwa sheria ya bunge la JMT ilioanzisha BMT, na ndio maana leo kuna mtu anaitwa MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA, ukibadili malengo ya usajili wa chama cha siasa, utaingia mgogoro na Msajili wa Vyama! Simba na Yanga wanachofanya ni kubadili malengo ya kusajiliwa kwao, tena bila hata kubadili katiba yao kwanza. Ndio maana kwa busara, BMT wameshauri, Simba na Yanga waanze kubadili katiba zao.

ie
Kwani hizi timu zilianzishwa na wanachama au BMT?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom