Biashara ya Nguo za Mtumba: Ushauri na Muongozo wa Kuifanya kwa Mafanikio

Mkuu nguo za mitumba zinatofautiana bei. kuna balo la laki2, 3, 4, 5 hadi laki sita na kuendelea. na balo lenye nguo za kike, kiume, watoto., mashuka, sidilia. chupi nk. kama utakua unauza kwa jumla freh lakini kama rejareja ni kuomba Mungu. Balo lenye nguo 200 nguo nzuri unakuta ni 80 na zinazo uzika ni 140 inategemea simetoka wapi kama ni china itakula kwako. je zinazo baki utazipeleka wapi?.
USHAURI WANGU.
Nenda kwenye minada ya nguo ununue moja moja inayo kuridhisha kisha upeleke golini kwako. mia
Yap,kumbe wewe unaijua vzuri hii biashara!
 
Balo laki 5 na 6 huwa zina nguo cllassic kama upo chuo kwa nini usinunue viatu na vinguo vya kina dada mkifungua unauza?chuo inalipa sana kama huna aibu mi nimefanya sana nilipokuwa chuo, suruali niliyonunua kiboriloni mia 5 ilitosha kuuza hadi elfu kumi .
 
Email ni faoincredible@yahoo.ca Kuna ambao wamenitumia email sasa sijui tatizo la email kugoma linasababishwa na nini. Ila waweza niwekea simu yako ya mkononi kwenye PM na hivyo nami nitakupa simu yangu ya mkononi kwa njia hiyo.

Katika kutuma sms au email naweza jibu mara moja kama umeituma kuanzia saa 8 mchana maana Tanzania mpo masaa saba mbele ya Canada. Otherwise niko open ili pamoja tusonge mbele.
 
Mkuu e-mail yako inanigomea kaka ikague vizuri

kama unatumia gmail itagoma, mi mwenyewe jamaa zangu wenye email za canada inakataa nikitumia gmail, huwa sielewi ni kwanini, ila ukitumia yahoo inakwenda
 
Ndg zangu wana JF naomba kusaidiwa mawazo katika biashara hii ya nguo za kike;

1. Mtazamo wako kama inalipa au hailipi
2. Location sahihi ni ipi
3. Nitarajie changamoto zipi?

Pia, kama unaushauri mbadala nitaupokea na kuufanyia kazi.
 
Habari wana Jamii!

Niko US nataka sana kuanzisha biashara ya mitumba , ningependa kuuza marobota. Sasa basi kama kuna mwanaJamii anahusika na hii biashara ningependa kujua yafuatayo:

- Robota la grade A ni kiasi gani?
- Bora kuuza mnadani au kuwa na sehemu?
- Vipi usumbufu Bandarini?
- Ili kuchukua, approximately kiasi gani kuanza biashara?

Na kama una ushauri za zaidi ningeshukuru

Asante wanaJamii..

========

Baadhi ya michango, maoni na maswali mengineyo kutoka kwa wanaJF..

Balo zipo sehemu nyingi
Changamoto ni iyo uchakachuzi wa mabalo, niliwai kwenda uganda balo hazifunguliwi.

Mara nyingi balo ikiwa na koa, imefungwa na yale mabati inakuwa haijafunguliwa, ila ikiwa na plastic mara nyingi izo ndizo zimefungwa upya, ila c lazima iwe ivo.

Haya ni jibu swali wanalokwepa wengi zinapatikana wap?

Ukifika mnazi mmoja dar, kama unatoka k.koo nyooka moja kwa moja kama unaenda mnara wa saa au stesheni, unapovuka tu makutano ya pili ya mataa, ya mnazi mmoja kuna maduka wanauza sana kanga na vitenge, kuanzia hapo, maduka ya mitumba nikibao, nenda mtaa wa pili kama sikosei unaitwa sofia, maduka kibao hapo mitumba tupu, yani zunguka eneo ilo utapata mitumba kibao.

Pili ukiwa congo, k.koo kituoni mkono wa kulia ukiwa unaelekea mnazi lipo duka moja hapo kwa mhind linapakana na duka la samsung.

Tatu Magomeni, ni eneo jipya hili, ofis za ttcl ukifika hapo upande wa pili utaona mitumba had ya viatu wholesale bales.

Hapa magomeni ni makutano ya mataa pale ukiuliza ofis za ttcl utaoneshwa.

Changamoto ni kupata bales nzuri, kama unaweza mtafute mteja wao mzoefu wanaempaga vitu bora, akuchukulie.

Au washikishe wale jamaa tingo wa dukani kitu kidogo, wambie nipe kitu cha maaana jifanye ni mzoefu ila unabadili duka tu.

Ukijifanya mzoefu usizubae, kwa mfano ukiuliza mixer ya nguo za kike, akikuuliza kg ngap unakuwa shapu kuonesha unajua, sio wanauliza Kg hujui kuwa balo zina kilogram

Au unaulizwa material inayotaka hukui, either cotton, nylon n.k

Nahs nimesema kidogo kitakachowasaidieni

nimeiona mkuu text yako!
ila biashara ipo hivi:

Kila baro inavyotoka nje inakua na mchanganyiko wa nguo zote yaani grade A, B,C na zinginezo na haswa kwa zile mixture kinachosumbua kuna aina fulani ya baro huwa wabongo huzifungua na kuchukua nguo nzuri then huzipack tena
sasa hukikumbana nazo hizo zilizofunguliwa unaweza ukakata mtaji

Kuna aina kama tatu hivi za baro ambazo ni nzuri kwa mnada kwani zenyewe ni mixture

Aina ya kwanza ambazo zenyewe hutoa nguo nyingi ambazo ni grade one ni Australia ambazo zinapatikana ktika uzito wa kg 100 na bei yake ina range Tsh 450000 hadi 500000,hizi ni nzuri na ndio ninazoziuza Mimi nawe nakushauri uzipate hizo kwani si rahisi kukata pesa yako ,umeanguka sana unarudisha pesa yako

Za pili ni baro za kichina nazo ni nzuri na hata bei yake ni affordable kg 100 @ Tsh 370000 hadi Tsh 420000

Na za tatu ni za kimarekani maarufa kama SUMMER, zinapatikana katika uzito wa kg 50 na 80 na bei zake Tsh 250000 hadi Tsh280000 kwa za kg 50 na Tsh 320000 hadi Tsh 370,000/=
ndio hivyo mkuu jipange kachukue mzigo huo

Biashara ya mitumba ni nzuri ila kwa sababu ndo unaanza usitumie kiasi chote kufanya hiyo biashara kwa sababu huwezi jua kama itakulipa au lahh..Kwa kuanzia tumia angalau hata 1mil.kwa kuanza kuchagua baadhi ya nguo kwenye masoko then unauza kwa staili yako kama ni kutafuta frame yote ni juu yako.

Nakwambia hivo kwa sababu na mimi ni muajiriwa kama wewe na nimeshafanya sana mambo ya biashara, yana challenge zake. Usitoe kwanza kiasi chote angalia mwelekeo wa iyo biashara yako mana najua utapata ushauri mzuri tu kutoka kwa wafanyabiashara wa mitumba ila nakushauri usiingie kichwa kichwa...


Ushauri wangu, lete hiyo mitumba Tanzania 70% iwe ya kiume na 60% ya kike! na kwa kuwa unaanza lete grade 1, ili ujenge good will na wateja! Wahindi wanachokifanya wanaleta grade tofauti kisha wanachanganya ili kupata super profit! Uzuri mmoja ni kuwa, ukileta mali nzuri, mteja mmoja akifungua na kuona ni mzuri, huwaambia wenzake na wote huja kwako.

Kizuri kingine ni kuwa, kuna watu wana hela zao chini.. Wao wanasubiri wasikie fulani kafungua mali nzuri na inakimbia....yeye anakufuata, kisha anakupa hela ya belo zote ulizonazo store.... Kisha yeye anauza rejareja kama wewe ila anakuwa kaongeza elfu kumi au ishirini kwa belo!

Kwenye hii biashara, umakini mkubwa ni ubora wa hizo nguo....na jinzi sio jinzi tu....ziwe za kisasa....sio chupa (juu pana, chini inabana, hutouza)! Nilishawahi kuingiza nguo frm Tz zamani from USA via Charlestone port via S.Carolina.....zilinikata kwa kweli!

Hakikisha kwenye huo mtumba, hakuna sox wala chupi.... TBS watakupa shida bandarini!

Kama unaweza, mkuu badala ya nguo za mitumba weka mitumba ya viatu vya kiume, au changanya nguo za mtumba na viatu vya mtumba ili upime biashara! open shoes, canvas, mukasin, sendoz raba n.k! Kikweli biashara ya viatu vya mtumba inakimbia kupita maelezo......!

Huna haja ya kuwa na duka au stoo kariakoo...wewe ukitangaza tu una viatu vya mtumba hasa vya kiume na kama utaweka kidogo vya kike visiwe kokoko, watu wananunua mali yote kwa siku moja! Ukiwa mvivu, utawauzia kontena lote, faida utaiona lakini ni kidogo sana ukilinganisha na watakachoenda kupata wao!

Kila siku asubuhi saa kumi uwe ushafika kariaokoo (mchikichini) na baloo tatu au nne hivi..... Na kuhakikishia mpaka inafika kwenye saa moja asubuhi, unakuwa umemaliza mali yoote na unarudi home na furushi la kimango! Kule unakodisha meza kwa huo muda ni shilingi 5,000/- na vijana waaminifu wapo wa kukusaidia kulinda na kupiga debe, wewe kazi yako ni kupokea hela!

Kinachofanyika ni kuwa a day before upeleke hizo balo za viatu kariaokoo, unaita vijana wanatenganisha viatu vya kushoto na kulia, kwahiyo ukifika mchikichini asbuh unamwaga eiza vya kulia unabaki na vya kushoto and vice vser! Akikipenda kiatu unamtajia bei, bkoz kila kiatu kina bei yake, anakupa hela huku ameshika kimoja alicholipia! wakati wakufunga biashara, unampa mguu uliobakia...!

Ofkoz, hadi mida hiyo lazima kuna pea kadhaa zinakuwa hazijapata wanunuzi, good news ni kuwa pembeni kuna watu kibao wanasubiri muhesabiane in a flat rate vyote vilivyobaki...ana ku'cash wewe unarudi na hela home saa moja asbh....na kuandaa mazingira ya kesho!

You can send mtu wako pale mchikichini, mida hiyo asbuhi akathibitishe nilio kwambia!

==========

Swali lingine lenye kona tofauti lakini maudhui sawia

Wakuu habari zenu

Nina wazo la kufanya biashara ya kuuza nguo za mitumba kwa mfumo wa kununua Mabaro then kuyapeleka kwenye masoko mbalimbali, natafuta vijana wanazipiga mnada then mzunguko unajirudia kama kawa.

Mtaji nilionao mpaka sasa ni 5 Million Tshs, sina uzoefu wowote wa biashara, hivyo kwa yeyote mwenye kuielewa hii biashara please tupeane uzoefu.

Kwasasa bado nipo kwenye ajira, ila natamani sana kuanza kuwa mjasiriamali maana siko happy kabisa na suala zima la kuajiriwa, niliingia humo kwa lengo la kukusanya mtaji then nikafanye yangu

Naomba kuwasilisha, napokea pia mawazo mapya....

Nimesoma comments za watu kuhusu business hii nyingi ni nzuri ila ningependa kuongea vichache ninavyovifahamu.

Kwanza gross profit margin ya 50% to 100% kwenye bness hii IPO Na watu wanatengeneza hiyo pesa however mi namshauri huyu Jamaa aanze na mitumba ya watoto na nguo za wanawake...

Baro la nguo nzuri kwa watoto linaanzia 200,000 mpaka 480,000 inategemea Na za nchi gani,umri na material kwa nguo za akina Dada cjui bei ya Baro but am sure kwa laki 4 was 5 anapata.

Halafu aanze kwa kununua mabaro hapa Kariakoo (Dsm, Tanzania) then awe anauza nje ya mji Mfano Kimara, Mbezi Bunju etc coz costs za fremu huku town itamgharimu lakini pia competition kubwa mjini.... Mi ndo naanza ya nguo za watoto
 
Sina uzoefu sana, ila kwa sasa kila unapotembelea wauza mitumba wanadai wadosi wanachakachua sana Bales, linalosemekana grade 1 unakuta 75% ni gade ya mwisho kabisa. Kwahiyo source iliyobaki, reliable ni nchi za jirani kama Kenya na Uganda, ambapo kwa mfanyabiashara mwenye mtaji mdogo ni kitendawili.

Kwahiyo itategemea kama unaleta kusupply wauzaji wakubwa au wauzaji wa mwisho, ila opportunity kutokana na mazingira hayo niliyokuambia ipo na tena nzuri, kizuri kinajiuza jombaa.
 
Kaka Asante.

Yes mi nataka kuleta contena niuze Mabelo sio nguo moja moja. Na as far as I know uko minus huku Mabelo yameshafungwa kwenye grade unayoitaka wewe. Kwa hiyo mi kama kuleta ntaleta na kuuza moja kwa moja. Asante kwa kunielimisha kaka
 
Kama kuna mwenye uzoefu anielimisha kwenye hili swala please: je belo lenye nguo mchanganyiko (za kike na za kiume) linauzwa tofauti na belo lenye nguo za aina moja?
 
Kaka nguo zikiwa mchanganyiko huwezi kuuza vizuri.let me tell u nguo za kiume first class ndio znalipa sanaaaaa mfano muhindi anauza belo ya jeans znakua 200 kwa Tzs 540,000 jeans 80 mpk 90 ndio hua nzuri
 
So far nimeongea na 3 different companies moja hapa US, nyingine Australia, na UK wote wanadai wanauza Mabelo mchanganyiko tu. ntaendelea kutafuta Kabla sijaanza kuleta mzigo bongo. Asanteni wana jamii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom