Elipendo joseph
New Member
- Dec 7, 2020
- 4
- 6
Kaka naomba hiyo nambaWatu wasikukatishe tamaa ndg, tena mimi si kwa rafiki wala jirani, nilianza mtumba, kwa kununua bero moja tu pale mnazi mmoja, faida ikatoka karibu sawa na bei ya baro nikarudia.
Nguo za kike zinalipa, mashuka na viatu, za kiume suruali na mashati ila wanaume wanakamatika kiurahs ukiwafikishia maeneo yao ya kazi au kwa kufuatwa.
Nimewai kwenda Uganda, najua vizur pia huko, anzia nyumbani uimarike kibiashara, japo mimi nimeajiriwa serikalini lakn nafanya sana mtumba. Na ivi sasa naanza likizo june, nitaendelea na mtumba kama kawa.
Mil 3 ni nyingi, suala la kununua bero na au za kuotea za kutundika/mnada ni wewe tu na upendo wako, za bero lazima ukute na marapurapu ndani, ingawa huwa tunauza cheap, na hazikosi wavaaji au wanunuzi, za kuotea utauza zote bila kuacha rapurapu lkn je? Unauzoefu wa kuotea nguo? Yani ukiiona tu unapoint? Maana mnakuwa wengi kayika ku point na wwngi ni wazoefu.
Hapo inahtaji mtu anaeona nguo tu nakujua hii ni sumu la sivo utaotea zote takataka au zinazokuvutia wewe binafs alafu zisivutie wateja.
Sehemu ya kupoint nguo ni ilala Boma, alifajir saa kumi na moja, baadae hakuna soko asbh meza ni za wanaouza kawaida kwa wapita njiA
Uliza swali kwa kile sikuandika nitakujibu.
Dresses za kike bero ya bei ya juu ni 380000/= kwa zile za kg 45, lakn unakuta bero ya top hadi 170000/= zinatofautiana kuanzia 150000/= mpk 400000/= hapo ndio juu sana kwa beri ya kilogram 45 na ukienda utaonesha hapa grade B hapa 1
Note: bero zinauzwa kwa kilogram, bei nilioweka ni. Kwa kg 45 ambazo mara nyingu utakuta nguo hadi 200
Bero za mil 1 ni kilograms 100 nk
Kuna maduka wana nguo uhakika. Naweza kukupa namba private nikakuunganisha.
Jaribu usikatishwe tamaa.