Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,581
- 18,124
nitakugongea thanks kama ukinijibu swali hili........kwa nini uligombea wakati ndani ya nafsi yako ulijua kabisa kwamba unataka mtu mwingine ashinde na awe mwenyekiti?....hakukuwa na njia nyingine ya wewe kumsapoti huyo mgombea?......
Kwanza kabisa ndani ya Nafsi yangu niliamini kwamba naweza kutoa mchango wangu katika harakati hizi moja kwa moja. Hata hivyo niliona haja ya kuunganisha nguvu na wagombea wengine waliokuwa tayari.
Lengo langu halikuwa Madaraka, tulijadili, tukaulizana sasa ni nani wa kuitoa sadaka Nafasi yake? Mimi nikawa tayari kufanya hivyo, nikawapa changamoto wale wagombea wawili wakubaliane.
Pia nilizingatia utayari wa kushaurika, uwezo wa kusimamia hoja zetu katika uongozi. Lengo langu lilikuwa ni kuwa na baraza huru, lisiloshikwa Mateka na lenye maslahi kwa vijana katika kurahisisha harakati zetu za kuchukua dola.
Pia tulizingatia Baraza lenye kubeba haiba na sura ya kitaifa litakalowafanya vijana wajiskie wao ni sehemu ya baraza hilo bila kujali kabila au Dini.
Pia kama wanasiasa tulitathmini uwezo wa kushinda kwa kiwango cha kuridhisha, ilionekana kutakuwa na uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 75 ingawa kabla nilikuwa na uhakika wa kushinda kwa zaidi ya Asilimia 60.
Nitarudi baadae.