Abdudlquarim Malisa naye Ajitokeza Kumuomba Baba Askofu Mwamakula na Viongozi wa CHADEMA Msamaha

Kurunzi

JF-Expert Member
Jul 31, 2009
9,288
9,923
Drama inaendelea baada ya jana Voronica France kujitokeza kuomba msamaha Baba askofu Mwamakula na Viongozi wa wa CHADEMA


Naye Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Abdudlquarim Malisa amejitokeza adharani na kuimba msamaha Askofu Mwamakula na Viongozi wa CHADEMA

Soma hapa Na eno ya Askofu na kile alichoandika Malisa

"Askofu ni mtu, kiongozi, taasisi na pia ni alama ya Kanisa. Jambo lo lote ambalo anatendewa hadharani wanatendewa walio nyuma yake na maumivu hayo huenda kwa watu hao. Ujumbe wa hapa chini ulitumwa kwa Askofu akiombwa msamaha. Askofu anaomba wauamini, wafuasi na watu wengine kumsamehe mtu huyu kwani yeye amekwisha kumsamehe na zaidi ya hayo atamuandikia ujumbe maalum wa kumtia moyo kwa kumtangazia msamaha.

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula!
Dar es Salaam, 24 Mei 2023"


"Baba Askofu Mwamakula!
Kwa majina ninaitwa Abdoulquarim Malisa, jina ambalo nimeanza kulitumia ukubwani. Jina nililopewa ningali mdogo kabla ya kubadili niliitwa Abdul Moshi, nimefika hapa kwa lengo moja tu; kukuomba msamaha.

Nimetafakari kwa kina na kwa dhati kabisa nimetambua kwamba nilikukosea mimi binafsi yangu, nilikukosea kwa maana ya kwamba kuna mahali kama kijana nilipaswa kutafakari kabla ya kukujibu lolote lile, majuzi nilikujibu vibaya kuhusu taarifa ya msiba wa mdogo wangu Dr Isac aliyeuawa Tarime. Ilikuwa ni hasira ya kuondokewa na ndugu yangu.

Msiba unatufika kwa namna nyingi na tunafuswa kwa maumivu ya namna tofuti. Mimi nilikosa mahali pa kupumzikia, kila nikiona mtu amesema tofauti na maelezo niliyonayo juu ya kifo cha mdogo wangu nilijikuta nimemparamia, zilikuwa ni hasira, naomba uniwie radhi mzee wangu.

Lakini pia nimewahi kukukosea kipindi cha nyuma upande wa kisiasa. Mimi ni mwana CCM, kuna mengi nilipingana na upande wa pili lakini leo nimetafakari kwa kina na kwa dhati kabisa, nilikosea. Inawezekana nilikuwa sahihi kipindi hicho lakini kwa sasa najiona mkosefu sio tu mbele za macho ya wanadamu bali hata mbele ya Mungu Mwenyezi.

Nakuomba unisamehe sana. Naomba niombee msamaha kwa Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Mzee wangu Mbowe, Tundu Lissu na wenzake. Niliwakosea.

Nashukuru kwa kuwa nimefikisha ombi langu kwako. Namuomba Mwenyezi Mungu pia anisamehe. Ahsante.

Abdoulquarim Malisa
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Kinondoni, Dar es Salaam.
24 Mei 2023."
 
I see kweli siasa ni dynamic Sana..
Ngoja tuone kufika 2025 kitatokea kitu gani.. lakini wafuasi wa mwendazake naona Kama wamekuja kivingine..Sina uhakika wanamaanisha nini..muda utatuambia
 
kuna kundi halimwambii ukweli Mama, (inawezekana ni kwa maslahi yao binafsi)anaweza KUdhani kwamba mambo yanakwenda sawa lakini mmh. kitendo cha maandalizi ya wanenaji na hata wasanii kuliweka jumla jumla tu kitendo cha ufunguzi wa Ikulu ya chamwino na (Kutokumpa nafasi stahiki JPM kama mtu aliyekwamua wazo lililochukua miaka 50 bila kikamilika ) kummwagia sifa Mama na yeye akazipokea haimpi credit kwa wanyonge (nahisi hizi ni hisia zangu tu) wala msinihukumu badala ya kumjenga wanambomoa na kumbomoa Mama ni kuibomoa CCM,
 
I see kweli siasa ni dynamic Sana..
Ngoja tuone kufika 2025 kitatokea kitu gani.. lakini wafuasi wa mwendazake naona Kama wamekuja kivingine..Sina uhakika wanamaanisha nini..muda utatuambia
Kwakweli huenda wanabadilisha strategies
 
Baada ya Askofu Mwamakula kumuomba Membe amsamehe Musiba, na kisha kikatokea kifo kabla ya msamaha kutolewa. Naona waliokuwa upande wa watesi wake wakianza kujitokeza ili kuomba masamaha, pengine hufanya hivyo kwa hofu ya kitu fulani!

"Perhaps this is due to the fear of unknown. If this thing happened to him, there is big possiblity of that thing also to happen to me".
 
There is something wrong,wait and see
Wanasemaga what goes around comes around ! Ni hicho tu hakuna kingine ! Ukishaona mambo mazito yanakuelemea ni lazima ukumbuke ni mabaya gani makubwa umemtendea binadamu mwenzio na ni lazima umuombe msamaha kwani ukishupaza shingo utajuta zaidi !!
 
Baada ya Askofu Mwamakula kumuomba Membe amsamehe Musiba, na kisha kikatokea kifo kabla ya msamaha kutolewa. Naona waliokuwa upande wa watesi wake wakianza kujitokeza ili kuomba masamaha, pengine hufanya hivyo kwa hofu ya kitu fulani!

"Perhaps this is due to the fear of unknown. If this thing happened to him, there is big possiblity of that thing also to happen to me".
Time will tell !
 
Back
Top Bottom