Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Msikile Waitara akitema cheche hapa


Asema watanzania wengi wanaisha maisha ya ufukara sana kiasi cha kushindwa hata kuwalipia ada watoto wao na kwenda kuomba msaada wa kufanikishiwa jambo hilo, akisema watumishi wa umma wote wanasomeshwa na watanzania na wana elimu ya kutosha, na kwamba wanafanya makusudi na kuiba kwa utaalamu.


Akisema uzembe upo kwa wabunge, kama mtu ameiba ripoti ipo, taarifa zipo, vyombo vipo, lakini mwizi hawajibishwi, je wanafundisha nini vijana wa Tanzania? Kwamba mtu ataiba na kuhamishwa tu wizara bila ya kuwajibika? Ataka wote waliothibitishwa kuhusika na wizi huo wanyongwe.

Asema wasisubiri kuambiwa kuwa wanantakiwa kuchukua hatua, bali wawajibishe sababu wao wabunge ndio wenye dhamana ya kufanya hivyo. Asema kama fedha zinatolewa kwaajili ya ripoti ya CAG kufanya uchunguzi halafu hakuna kinachofanyika zaidi ra ripoti hizo kuwekwa kwenye makabati na mwaka unaofata mambo kuwa yale yale, yeye Waitara ataachana na kuchangia maoni juu ya ripoti hiyo.
 
CEB48C8D-49DC-4883-8F16-C9D71626CED4.jpeg
 
Back
Top Bottom