Benard Saanane jisafishe haraka; atoa maelezo

Status
Not open for further replies.
nitakugongea thanks kama ukinijibu swali hili........kwa nini uligombea wakati ndani ya nafsi yako ulijua kabisa kwamba unataka mtu mwingine ashinde na awe mwenyekiti?....hakukuwa na njia nyingine ya wewe kumsapoti huyo mgombea?......

Kwanza kabisa ndani ya Nafsi yangu niliamini kwamba naweza kutoa mchango wangu katika harakati hizi moja kwa moja. Hata hivyo niliona haja ya kuunganisha nguvu na wagombea wengine waliokuwa tayari.

Lengo langu halikuwa Madaraka, tulijadili, tukaulizana sasa ni nani wa kuitoa sadaka Nafasi yake? Mimi nikawa tayari kufanya hivyo, nikawapa changamoto wale wagombea wawili wakubaliane.

Pia nilizingatia utayari wa kushaurika, uwezo wa kusimamia hoja zetu katika uongozi. Lengo langu lilikuwa ni kuwa na baraza huru, lisiloshikwa Mateka na lenye maslahi kwa vijana katika kurahisisha harakati zetu za kuchukua dola.

Pia tulizingatia Baraza lenye kubeba haiba na sura ya kitaifa litakalowafanya vijana wajiskie wao ni sehemu ya baraza hilo bila kujali kabila au Dini.

Pia kama wanasiasa tulitathmini uwezo wa kushinda kwa kiwango cha kuridhisha, ilionekana kutakuwa na uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 75 ingawa kabla nilikuwa na uhakika wa kushinda kwa zaidi ya Asilimia 60.

Nitarudi baadae.
 
Kwanza kabisa ndani ya Nafsi yangu niliamini kwamba naweza kutoa mchango wangu katika harakati hizi moja kwa moja.Hata hivyo niliona haja ya kuunganisha nguvu na wagombea wengine waliokuwa tayari,lengo langu halikuwa Madaraka.Tulijadili,tukaulizana sasa ni nani wa kuitoa sadaka Nafasi yake?Mimi nikawa tayari kufanya hivyo,nikawapa changamoto wale wagombea wawili wakubaliane.Pia nilizingatia utayari wa kushaurika,uwezo wa kusimamia hoja zetu katika uongozi.Lengo langu lilikuwa ni kuwa na baraza huru,lisiloshikwa Mateka na lenye maslahi kwa vijana katika kurahisisha harakati zetu za kuchukua dola.Pia tulizingatia Baraza lenye kubeba haiba na sura ya kitaifa litakalowafanya vijana wajiskie wao ni sehemu ya baraza hilo bila kujali kabila au Dini.

Pia kama wanasiasa tulitathmini uwezo wa kushinda kwa kiwango cha kuridhisha,ilionekana kutakuwa na uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 75 ingawa kabla nilikuwa na uhakika wa kushinda kwa zaidi ya Asilimia 60.Nitarudi baadae
umeeleweka
 
ulijadili namna au uwezekano wa kuunganisha hoja zetu ili tumpigie kampeni mgombea huyo ashinde. Wakati huo huo mimi nikiwa tayari kujitoa lakini nimsaidie mgombea mwingine. hii sentesi hapo juu kwa kweli inanipa wakati mgumu.......sion umuhim wa wewe kuwa mgombea...sasa tunaposema umetusaliti ndo katika mambo kama haya..ulikuja na sera nzuri hapa jf.tukakuamini sana kumbe deep down ulikuwa na plan ya kujitoa.......huku ndo kusaliti kwenyewe...........
Kujitoa doesnt equal usaliti,inategemea na mazingira ya kujitoa kwenyewe.Mimi si mwanachadema akama ilivyo kwa Ben,ila namtambua kama mwana JF,na kuna hoja nyingi tu tuna either mitizamo sawa ama yenye kupingana,yote bila kujali utashi wa itikadi za kisiasa.So kwenye hili niko naye bega kwa bega unless muonyeshe hicho kifungu cha 10 kinavyorelate na uvunjifu wa kanuni kama ilivyoainishwa.
 
Jamani,

Kwa nini tunamshurutisha Ben ajieleze hapa? Naheshimu maelezo yake nimeyasoma hapo juu lakini JF si kamati ya nidhamu ya chama chochote. JF hatuna nguvu ya kumtia hatiani au kumsafisha mtu na tuhumu za ndani ya chama chake. Ana uhuru wa kutoa maoni yake publicly lakini sidhani kama ni sahihi JF kujitwika jukumu la kuchunguza na kumhukumu mtu kichama.

JF haina damu ya kumsafisha mtu, ingelikuwa heri sana kama tungeshikilia msimamo wa kutokulalia chama chochote cha kisiasa. Watanzania walio wengi hawana chama lakini wana mawazo mazuri ya kujenga na kuikomboa nchi yetu, kuna wachache wako kwenye vyama wenye mawazo mazuri na nia njema, wote wako humu humu JF. JF isimamie maslahi ya nchi na vyama tuwaachie watu binafsi na itikadi zao.
 
I admire you!!
i hope macheche yako yataendelea, na wanaojitahidi kuwagawa hawataweza.
Kazi ilio mbele yenu ni kubwa sana!! Mungu akujalie uweze kuwashinda wauza magazeti wanaotafuta stori, usiwape za migogoro, uwape stori za kuhimiza ifanyike kazi ilio mbele, ya kuongoza vijana (wengi wakiwa hohehave, mbumbumbu, fuata bendera etc) wachache wakiwa na nguvu, akili, motisha, ari ambayo inahitaji tu viongozi kama nyie.

God be with you!!
 
Jamani,

Kwa nini tunamshurutisha Ben ajieleze hapa? Naheshimu maelezo yake nimeyasoma hapo juu lakini JF si kamati ya nidhamu ya chama chochote. JF hatuna nguvu ya kumtia hatiani au kumsafisha mtu na tuhumu za ndani ya chama chake. Ana uhuru wa kutoa maoni yake publicly lakini sidhani kama ni sahihi JF kujitwika jukumu la kuchunguza na kumhukumu mtu kichama.

JF haina damu ya kumsafisha mtu, ingelikuwa heri sana kama tungeshikilia msimamo wa kutokulalia chama chochote cha kisiasa. Watanzania walio wengi hawana chama lakini wana mawazo mazuri ya kujenga na kuikomboa nchi yetu, kuna wachache wako kwenye vyama wenye mawazo mazuri na nia njema, wote wako humu humu JF. JF isimamie maslahi ya nchi na vyama tuwaachie watu binafsi na itikadi zao.
Wengine hatuna vyama na issue kama hizi zitatusaidia kuvifahamu vyema vyama hivi vya siasa.Najuwa Ben amekubaliana na matokeo nk,yeye ni mwana chadema.Hata hivyo binafsi ninataka kujua nini haswa kilitokea kwa mwana JF mwenzangu.Issue si kusafishana hapa,you're in a wrong track.
 
Kwanza kabisa ndani ya Nafsi yangu niliamini kwamba naweza kutoa mchango wangu katika harakati hizi moja kwa moja.Hata hivyo niliona haja ya kuunganisha nguvu na wagombea wengine waliokuwa tayari,lengo langu halikuwa Madaraka.Tulijadili,tukaulizana sasa ni nani wa kuitoa sadaka Nafasi yake?Mimi nikawa tayari kufanya hivyo,nikawapa changamoto wale wagombea wawili wakubaliane.Pia nilizingatia utayari wa kushaurika,uwezo wa kusimamia hoja zetu katika uongozi.Lengo langu lilikuwa ni kuwa na baraza huru,lisiloshikwa Mateka na lenye maslahi kwa vijana katika kurahisisha harakati zetu za kuchukua dola.Pia tulizingatia Baraza lenye kubeba haiba na sura ya kitaifa litakalowafanya vijana wajiskie wao ni sehemu ya baraza hilo bila kujali kabila au Dini.<br />
<br />
Pia kama wanasiasa tulitathmini uwezo wa kushinda kwa kiwango cha kuridhisha,ilionekana kutakuwa na uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 75 ingawa kabla nilikuwa na uhakika wa kushinda kwa zaidi ya Asilimia 60.Nitarudi baadae
dogo wanaokusifia hapa wanakudanganyana na hiyo baadae usirudi kabisa.
Hivi unataka kutuaminisha kuwa baraza halipo huru kwakuwa mbinu yako haikufanikiwa? Ni kweli Regia amesema hayo maneno kwamba watu wanachaguo zao pale, sasa unatueleza nini kama unaonekana unakubali kwa shingo upande? unadhani tatizo ni kabila na dini tu kwa watanzania? Km ni hivyo why were you against Heche? (according to Regia).
 
Hayo uliyosema hapo juu ndo kifungu cha 10?Kama mbinu yake ya kuunganisha nguvu ilivunja kanuni,then wekeni wazi how,otherwise tutaamini kuwa ni kweli baraza haliko huru.
 
Kwanza kabisa ndani ya Nafsi yangu niliamini kwamba naweza kutoa mchango wangu katika harakati hizi moja kwa moja.Hata hivyo niliona haja ya kuunganisha nguvu na wagombea wengine waliokuwa tayari,lengo langu halikuwa Madaraka.Tulijadili,tukaulizana sasa ni nani wa kuitoa sadaka Nafasi yake?Mimi nikawa tayari kufanya hivyo,nikawapa changamoto wale wagombea wawili wakubaliane.Pia nilizingatia utayari wa kushaurika,uwezo wa kusimamia hoja zetu katika uongozi.Lengo langu lilikuwa ni kuwa na baraza huru,lisiloshikwa Mateka na lenye maslahi kwa vijana katika kurahisisha harakati zetu za kuchukua dola.Pia tulizingatia Baraza lenye kubeba haiba na sura ya kitaifa litakalowafanya vijana wajiskie wao ni sehemu ya baraza hilo bila kujali kabila au Dini.

Pia kama wanasiasa tulitathmini uwezo wa kushinda kwa kiwango cha kuridhisha,ilionekana kutakuwa na uwezekano wa kushinda kwa zaidi ya asilimia 75 ingawa kabla nilikuwa na uhakika wa kushinda kwa zaidi ya Asilimia 60.Nitarudi baadae

........kwa nini hukutaka kuisikiliza nasfi yako? ..............kama ulikuwa unaweza kushinda kwa zaidi ya 60% na huyu ameshinda kwa 53% huoni kama wewe ni zaidi yake? ..........lengo lako ni kuwa na baraza huru...kwa nini usiseme kuwa ni chadema kuwa na baraza huru hili neno ''lako'' linazua maswali........ ......kama dhamira yako ilikuwa nyeupe hivi na mikono yako misafi hivi..kwa nini umeenguliwa? .......mwisho naomba nikuulize Ben..unahisi umeonewa?au ilikuwa ni haki kuenguliwa kwa kile ulichofanya
 
Hongera kwa maelezo yako lakini ulifanya makosa makubwa na ya kujidhalilisha wakati ulipewa imani kubwa ya kuongoza jahazi la CDM.......cha msingi uache malumbano na mpe ushirikiano mshindi aliyetangazwa.
 
asante kwasababu amefunika kombe mwanaharamu apite.

wanafiki sana nyie chadema hamna lolote. kuna mawili huyo kijana ni mtoa rushwa au viongozi wa chadema mnachakachua watu msiowataka.

hamuwezi kuendesha uchaguzi kila siku vurugana tu.
I aggree with you as much as i dont want to.Something aint right,sasa mnafunika kombe this time,mkichukua nchi itakuwa vipi?Naelewa wanachama wa chadema ni wengi humu,na hivyo mnaogopa mijadala ambayo inakichambua chama chenu,however ni lazima tujue ukweli ili kuweka heshima ya jamvi ya kutokuwa bias....Issue hapa sasa kwa ujumla siyo Ben,ila ni utaratibu uliotumika.Tunaambiwa kifungu cha 10 kilivunjwa,lakini wanachama na wapenzi hawazungumzii hilo,bali porojo tu na tuhuma wasizotaka kuzithibitisha.
 
Froida,naelewa sana hofu yenu wanachadema ya mambo yenu kujadiliwa hapa JF kiuwazi.Si vyema kwa wana JF wote kuwa na hofu za kuchambua mienendo ya vyama vya siasa na uwakilishi wake kwa wananchi.Ben hawajibiki kwenu hapa JF,bali kwa wananchi kupitia JF,kwa mfano mimi si mwanachama wa chama chochote cha kisiasa,however ni mwanachama mwaminifu wa JF.

Mijadala tuliyoijadili na ambayo tunaendelea kuijadili humu JF ina maslahi kwa wengi wetu ambao tunataka kuvisoma vyama hivi kabla ya kujiunga navyo.Ben was here long time ago,na namkumbuka kwenye mijadala mingi tu,na kwahivyo naifahamu baadhi ya misimamo yake,kuwa ni mwanachadema.Tofauti na hapo sijui.

Umegusia kuhusu usalama wa Taifa.Unazumzungumzia Ben ama nani?Sijakuelewa unaposema sisi ni usalama wa Taifa tuliopandikizwa.Tafadhali jibu kuendana na matamshi ya kiongozi wako kama wewe ni chadema,alisema something kuhusu kifungu cha 10,unakifahamu wewe hicho kifungu?
 
Nilikuwa natafuta lengo la hii thread nadhani malengo yake hasa yalikuwa ni haya uliyoanza kuandika hapa!

Cha ajabu sana wanaolalamika sana humu kuhusu Ben kuenguliwa ni CCM na siyo Chadema! Kulikoni? Hii thread haikuwa na maana yoyote tofauti na lengo lenu nyie mliotaka kuleta mtandao wenu ndani ya CDM utafuta njia ya kujiosha lakini hamjui mlifanyalo maana kama mnataka kujisafisha njia nzuri ni ndani ya Chama na si hapa JF maana hapa sipo maala pake, kumbukeni kuwa hapa ndipo mlipo potezea turufu yenu ya nia mbaya dhidi ya Chadema msidhani kuwa humu JF wote ni watoto wenzenu wengine ni baba zenu na wameanza kuliona jua kabla hamjazaliwa.

Suala la Ukombozi wa Tanzania limefika katika peak hours watu wenye mtazamo na macho ya Utumwa hawana nafasi tena! Kuna watu wanadhani kuwa hili swala ni la CDM peke yake si kweli hii sasa ni agenda hadi ndani ya vyombo vyote vya Umma, ndani ya Makanisa na hata ndani ya Misikiti ukishaona agenda inasumbuwa hadi vichwa vya Makasisi na Maimamu juwa kuwa hata anayekutuma kwenda kuivuruga anaweza kuwa anaiunga mkono, na unapoondoka tu ofisi anatoa taarifa sehemu husika kuwa Mr.xyz is not good fellow angalia moja. mbili na tatu utajionea mwenyewe.

Tanzania ya Leo siyo ya Jana Poleni sana.
 
nilikuwa natafuta lengo la hii thread nadhani malengo yake hasa yalikuwa ni haya uliyoanza kuandika hapa!

Ndugu Mwafrika Arafat,ni mijadala gani hiyo wachache wenu mnayoona inafaa na ambayo haifai?Kama haifai,basi si muipotezee tu?Na kama ni issue zenu za ndani za chama basi mzisolve ndani ya chama.However kulimit what we can disscuss as long as hatuvunji kanuni za JF ni ukiritimba.Unaweza kutuwekea kanuni ya 10 hapa?
 
Hivi mnafikiri hamfahamiki mnaficha kichwa kama mbuni huku mwili mzima ukiwa nje mmemponza Ben kwa visifa vya kijinga na ben akaingia kichwa kichwa.
Huwezi kusema unamfahamu mtu bila kutaja ni kivipi,unless wewe ni mmojawapo wa mamods ama wamiliki na unataka kutuaminisha na kutuhabarisha vinginevyo kuhusu baadhi ya members humu?
 
Huyo saanane kuna siku alikuwa anawaambia wazambia na wazimbabwe kuwa serikali zote afrika zinahitaji kupinduliwa,wana kikundi chao cha wanasiasa chipukizi wanataka kuleta mapinduzi.huyo ni mroho wa madaraka na ni hatari akiwa ndani ya taasisi yoyote.Hatumtaki Tanzania hii,aondoke!
 
Ndugu Mwafrika Arafat,ni mijadala gani hiyo wachache wenu mnayoona inafaa na ambayo haifai?Kama haifai,basi si muipotezee tu?Na kama ni issue zenu za ndani za chama basi mzisolve ndani ya chama.However kulimit what we can disscuss as long as hatuvunji kanuni za JF ni ukiritimba.Unaweza kutuwekea kanuni ya 10 hapa?

Mimi sikuleta hii thread hapa ndio maana ukiangalia mchango wangu wa mwanzo niliuliza nini dhamira ya hii thread hapa wakati uchaguzi umeisha unaweza kuisoma ipo juu mwanzoni kabisa; ninachoona hapa nikuwa CCM wanalalamika sana Ben kuenguliwa na yamkini ndio walioanzisha hii thread kwa lengo ambalo nyie mnalijua na mnataka kututia kwenye mtego ilituingie tunase! Mi ninavyojua na ninavyoona maneno ya Ben na malalamiko yenu humu na michango yake bado mnamponza na kama wana CDM makini wamo humu wanaona na kufuatilia lazima kuna points wanazipata juu yenu na juu ya Ben!

Mi sioni haja ya hii thread hapa labda kama lengo ni kumsafisha mtu wenu, na kumsafisha mnakotaka ndiko kunazidi kudhiirisha kuwa ni mtu wenu! Kama nilivyosema awali Nyie rafikize ndio mmemponza zaidi na hapa bado mnazidi kumponza msidhani watu ni wajinga kiasi hicho, mtaweza kuwadanganya mara moja lakini hamta weza kuwadanganya kila siku!

Huwezi kusema unamfahamu mtu bila kutaja ni kivipi,unless wewe ni mmojawapo wa mamods ama wamiliki na unataka kutuaminisha na kutuhabarisha vinginevyo kuhusu baadhi ya members humu?

Unaweza kumsoma mtu kutokana na mchango wake na hoja zake ukamjua anakotoka na anakoenda! Nadhani kubalini kuwa mmeshindwa katika hili na mbadilishe mbinu yaani mjipange upya! Kujadili zaidi hii hoja aina mashiko labda kama Ben anatakakujiunga na CCM baada ya hii thread kwa hiyo mna jaribu kutengeneza njia ya kutokea!
 
Status
Not open for further replies.
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom