Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Masatu,

Umeshawahi kufika ofisi za Manji? Nenda pale au piga simu uulize ninasema bila tatizo na sio siri kuwa Mbunge. Malima ni mfanyakazi wa kampuni za Manji kama mkurugenzi, kama huamini nenda uulize mwenyewe bro, hilo simsingiziiii, ni FACT!


Mzee Mugishagwe,

Ninarudia kuwa uache huo ujinga wako, wa kurukia usiyoyajua na kurukia jina langu kila wakati, hizo siasa za kusema eti JM amejiunga na kundi la Sitta, unahitaji kwenda huko maporini Holland, au Kumekucha.com ambako watu hawajui siasa ndio utawamabia huo ujinga waukubali,

Sitta alikwenda kumuomba JM baraka za kuwa Spika, akapewa na akawa halafu leo JM tena akajiunga na kundi la Sitta,

pure NONESENSE, vijana kama mnahitaji data mseme mpewe data za kweli sio hizi garbage data, wewe hata wapika chai bungeni ukiwaambia hizi data watakushangaa JM ajiunge na kundi la Sitta ili apate nini? Sitta ana ubavu gani wa kuwa na kundi wakati hata huo u-Spika alipewa na EL na RA? kwa kumtumia Marehemu Akukweti, aliyemuuua Msekwa kwa kutoa siri kibao ambazo alikuwa akizikusanya akiwa msaidizi wake wa Spika, wewe uliza kama Msekwa alienda kwenye mazishi ya naibu wake wa zamani,

Please do not get me started!
 
Nimezungumza na Mhe. Adam Malima kuhusu barua yake ya kuhoji uamuzi wa Spika. Pamoja na maswali mengine nimemuuliza pia kama yeye ni mfanyakazi au amewahi kuwa mfanyakazi wa Manji. Zaidi ya yote anajibu pia uhusiano wake na chama cha NRA na kama ana mpango wa kurudi huko endapo CCM watamtilia ugumu. Matangazo hayo yatarushwa saa sita usiku mida ya Marekani mapema asubuhi nyumbani TZ.

Asanteni.
 
BTW,
Uchunguzi uliokuwa unafanyika Marekani (tuliambiwa Black Box na vitu vingine vimepelekwa huko) kuhusu kuanguka kwa ndege ile umefikia wapi?

Wahusika huwa wana tabia ya kutuahidi taarifa za matokeo lakini ni nadra kutekeleza. Nakumbuka hata pomboo (dolphins) walivyokufa kwa mamia huko Zanzibar tukaambiwa kuwa wanapeleka sampuli muhimu kwa uchunguzi Sweden; mpaka leo sijawasikia...

Unless, of course, kama haya yote (na hil hapo juu) yalinipita.
 
Mzee nadhani sasa unaanza kuonyesha matatizo yako . Yaani unadiriki kunishambulia hata wakati sijasema lolote ? Nimekuja kuelezwa kwamba umenishambulia hapa ndiyo nakuja kuangalia . Mzee heshima mbele . Unaweza kutoa ushahidi wa mimi Mugishagwe kusema kwamba JM anaungana na Sitta ? Kwa maeleo ya wengi hapa na wewe ni kweli sasa JM ni kundi la Spikla ushahidi upo sasa matusi ya nini wakati hata wewe mwenyewe una shinda hapa unampigia debe spika kumbe unajua kwamba JM ndiye King Maker na wewe uanendeleza kwa sababu hizo hizo .

U need to university degree kujua kwamba u are shouting because JM ana ties na Spika na you have made it clear hapa sasa haya maneno ya kufoka na povu kukuyoka kama umekunywa Petroli ya lori laki yana sababu gani ?

Unalia na Holland ? Unalia na Kumekucha? That is low since you know nothing nakuacha uendelee kutembea uchi watu wacheke . Eti unakata issue zipi ? yaani kuwa na uhakika kwamba JM ana ties na Spika ukathibisha hapa ni issue kweli wakati kila kitu ndani ya CCM ndiyo kinavyo enda kwamba kuna miungu watu na wanao gawa madaraka kama ulivyo thibitisha mwenyewe .

Pole sana Mzee sina muda wa kulumbana nawe .
 
Nimezungumza na Mhe. Adam Malima kuhusu barua yake ya kuhoji uamuzi wa Spika. Pamoja na maswali mengine nimemuuliza pia kama yeye ni mfanyakazi au amewahi kuwa mfanyakazi wa Manji. Zaidi ya yote anajibu pia uhusiano wake na chama cha NRA na kama ana mpango wa kurudi huko endapo CCM watamtilia ugumu. Matangazo hayo yatarushwa saa sita usiku mida ya Marekani mapema asubuhi nyumbani TZ.

Asanteni.
Tunasubiri Kuyasikiliza na ninafikiri umemuuliza kilichomsukuma kulipeleka hili swala la mengi na manji Bungeni na vile vile hali ya hilo swala kugharimu millioni 100 za walipa kodi kwa kuunda tume.............................Haoni kwamba yeye ndiyo chanzo kilichopelekea matumizi ya fedha ya walipa kodi kutumiwa kwa ajili ya kuwajadili wafanyabiashara wawili?
 
Mzee Moderator,

Hapo hunipatiii haki, huyu bwana kila wakati ndiye anyenichokoza akifikiri hafahamiki, wakati tayari ninazo id na ifo zake zote, juzi nimekuomba umpe salam zangu kuwa sasa ninamjua kuwa ni nani na mpaka majina anayotumia hapa kama, Murangira, Abdalah Hussein, Tibwili tibwili, na kule kumekucha.com anayoimiliki anatumia jina la mvutakamba, na mimi sina tatizo yeye kuniiita mtoto wa Jm, kama ambavyo amekuwa akinililia siku nyingi hapa na sijaona ukimuonya,

sasa leo amenianza tena kuniconnect na maneno yakje ya kawaida ya JM, ninamjbu unainambia niache matusi? are you serious? Wewe huoni kuwa alioandika pale juuu ni ujinga? Ninarudia tena kuwa ni NONESENSE, huyu mtu hana hoja siku zote ni Jm, jm,

Mzee Ole, mimi simuogopi huyu mjinga na niko njiani kula naye sahani moja only a matter of time, na usiniambie tena kuwa niache matusi kama huwezi kumwambia huyu mjinga kwanza!

Tena kwenye hili bwana Ole you can ban me go ahead!
 
Mzee Mugishagwe,

Ndugu yangu un*****, najua una hasira ya mimi kutokuja kwenye ile forum yako maana toka nitoke hakuna watu tena,

Pole sana kijana ndio dunia, wewe ninakutembeza ukiwa na nguo!
 
Tunasubiri Kuyasikiliza na ninafikiri umemuuliza kilichomsukuma kulipeleka hili swala la mengi na manji Bungeni na vile vile hali ya hilo swala kugharimu millioni 100 za walipa kodi kwa kuunda tume.............................Haoni kwamba yeye ndiyo chanzo kilichopelekea matumizi ya fedha ya walipa kodi kutumiwa kwa ajili ya kuwajadili wafanyabiashara wawili?


of course nimemuuliza hayo yote... ndio maana sisi ni KLH News.. hapendelewi mtu, haogopwi mtu, na hapendwi mtu.. YOTE yanazungumzika.
 
Hakuna mtu anayefungiwa ila kama artical yako itakuwa haikubaliki itabidi tuifunge isisomwe na members.

KITU AMBACHO NAOMBA NI KWAMBA MEMBERS TUHESHIMIANE NA TUWE WASTAARABU.
Is that too much to ask?
 
ndio maana kwenye forum yangu nilianzisha mahala pa watu kutukanana.... wawekeeni sehemu ambapo wenye beef wanapelekana na kukunjana mashati wakati wengine tukiendelea na mada zetu.
 
Mzee MMJ'

Hakuna mwenye beef hapa, isipokuwa ni lazima data ziulizwe hapa huwa hatuogopi mtu, data zinazosema kuwa Jm amejiunga na kundi la Sitta, okay sasa uchambuzi wa siasa kama ninavyoijua bongo on hizo data,

Ni kwamba Sitta ana kundi lake ndani ya mtandao, kundi hilo ni strong kiasi cha kumshawishi Jm kujiunga nalo, likiwa na nia ya urais wa mwaka 2015, maana 2010 hakuna uwezekano ni lazima Muuugwana amalizie ngwe ya pili kama waliopita, Jm sasa hivi ni miaka 72, by mwaka 2015 ina maana ongeza miaka kama 8 zaidi atakuwa at least 81, Tanzania tutakuwa na waziri mkuu mwenye huo umri? Maana akishajiunga na hilo kundi watampa kazi gani wakishinda? Hawezi kuwa waziri tena, umakamu anauacha karibuni sasa niambie na hizo data watampa kazi gani?

Data latest za ndani ya bunge sasa ni Mzindakaya, kujiunga na kundi la el kutoka kiundi la asilia, hizo ndio news ndani bunge sasa hivi ndio maana kwenye rada, na richmond yuko kimyaa!

Otherwsie, tutaendelea kukata ishu hapa, kiongozi kama hafai hafai I do not care kama ni CCM au upinzani nitasema, kama jana nilivyounga mkono hoja ya wachangiaji wengine kuwa Mama Meghji wiazara imemshinda, na ninarudia kuwa hiyo sio siri ndio maana hata alipopangiwa kwenda kushiriki kwenye kampeni ya uchaguzi Tundurru, wajumbe wengine walimkataa ikabidi atolewe kwenye ujumbe huo wa CCM, kama kiongozi hafai hafai lakini lazima kuwe na ukweli kuwa hafai,

Otherwise tutaendelea kukata ishu kiroho mbaya hapa, mwenye beef tutafutane uso uso tusisumbue wananchi hapa! Yes nilikuwa kwenye forum ya jamaa nikaisimimamisha, nikaamua kutoka ikafa sasa dawa ni kuja hapa na kunilazimisha kuwa mimi ni mtoto wa JM? What a joke!

Halafu Sitta mwaka 2015 atakuwa na umri gani?
 
ndio maana kwenye forum yangu nilianzisha mahala pa watu kutukanana.... wawekeeni sehemu ambapo wenye beef wanapelekana na kukunjana mashati wakati wengine tukiendelea na mada zetu.

Bila watazamaji hakuna ngoma; that you can be sure of.
 
kalamu, nina maana wapewe uwanja ambapo wengine tutaenda kuangalia, sina maana wajifungie wao wawili.. ili siasa ibakie siasa... na mambo mengine.

Mzee Es.. haya endeleeni wengine tunaangalia hatukwaziki na lolote lisemwalo hapa, wote ni watu wazima!!!
 
Nimekusikia mkuu, ila sina uhakika kama wote ni watu wazima maana kuna some of the posting zinawashitaki wanaozituma kama ni watu wazima au!
 
(a) Hii kesi ya Malima na Mengi haikutakiwa itumie mapesa yote hayo; hayo ni matumizi mabaya ya fedha za walipa kodi. Kwanza kabisa kesi hii ilishavurugwa kutokana na kuwepo kwa madai ya rushwa ambayo yalitolewa na Mheshimiwa Ndesamburo. Sijui kama Spika alitaka kuimaliza harakaharak kusudi madai ya rushwa dhidi ya wabunge yasifanyiwe upelelezi, hasa kwa vile yalikuwa yanamhusisha na waziri mkuu. Kwa vyoyote vile kesi ya Malima na Mengi kwa kweli haikutakiwa ituchukuliwa muda hivi kwa vile siyo tu kuwa haikuwa na maslahi yoyote kwa taifa bali pia kwa vile imegubikwa na mashaka mengi.


(b) Unfortunately Mheshimiwa Malima ame-underestimate powers za spika. Pamoja na kuwa standing order number 88 inaeleza kuwa ripoti za kamati ziwasilishwe bungeni ili zijadiliwe, kanuni number 4(2) inampa madaraka spika kuamua ni ripotri gani ijadiliwe na wala hakuna kifungu chochote kinacho-overide madaraka hayo ya spika. Kwa hiyo hata kama ni kweli ripoti hiyo ilitakiwa ijadiliwe bungeni, ni lazima ipate baraka za spika chini ya madaraka yake hayo aliyopewa chini ya kifung 4(2). Hata katika taratibu nyingi za undeshaji mijadala ya bunge, bado kuna vifungu kadhaa vinavyompa spika madaraka ya kuamua jinsi ya kuendesha mjadala ikiwa ni pamoja na kutumia njia aliyotumia: angalia kwa mfano vifungu 32(2) na 122(1). Kwa hiyo Mheshimwa Malima ni lazima awe macho na madai yake.


(c) Kwa kupeleka madai yake kwa katibu mkuu wa CCM ambaye madaraka yake hayahusiani na shughuli za bunge, Mheshimiwa amekiuka kanuni namba 4(3) ya bunge inayomtaka atoe malalamiko yake kwa Deputy speaker ambaye ndiye atamwarifu spika kuji-recuse kwenye kesi hiyo na ku-act kama mwenyekiti wa commitee on standing orders. Sijaangalia kwa kina sana kanuni zote za bunge lakini nadhani kuwa Mheshimiwa malima amevunja kanuni nyingine kama mbili hivi.
 
One may decide to call it CHUKI or whatever, however huwezi kubadilisha fact kwa pumba kuwa mchele, huo ndio ukweli wenyewe.

Hebu soma maelezo ya spika ambayo unaweza kuyapata hapa
http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1677

halafu soma maelezo ya KID (Malima) hapo juu then decide

Sitta ana mapungufu yake, that can be discussed ktk mada nyingine.
 
subirini mumsikilize mwenyewe akiwaambia kwanini ameamua kupeleka suala hili kwa Katibu wa CCM.
 
Mzee MMJ,

Hiyo ndiyo price ya demokrasi, kutakuwa na uchunguzi wa mambo ya maana na uchunguzi wa mambo yaisyokuwa na maana kwa taifa,

Either tuendelee na hiyo demokrasia kiduchu tuliyo nayo au tuache na kurudia ya zamani, ila kwa sasa sheria ya bunge inasema mwananchi yoyote wa Tanzania meaning wewe au mimi endapo majina yetu yatatajwa bungeni kwa sababu yoyote ile tuna haki ya kuwakilisha malalamiko kwa Spika wa bunge na yakafanyiwa uchunguzi bila ya kujali gharama,

sasa kusingekuwepo na hicho kifungu ina maana mbunge akilalalmika kama Malima alivyolalamikia Mengi, basi ilikuwa ni Mengi kuhukumiwa tu bila due process, hiyo enzi haitakuja kurudia tena, demokrasia hat ikiwa kiduchu ina price to pay for, na mahali popote duniani hulipiwa na kodi za wananchi!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom