Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Yebo Yebo nafikiri alikuwa anamaanisha kuchaguliwa kwake Bungeni.. siyo kuzungumzia jambo hili...
 
Kuhusu mahojiano na Mh Malima

Malima ameamua kumshitaki Spika ndani ya CCM au ameamua kupinga hukumu/uamuzi wa Spika ndani ya CCM.


Iwapo ameamua kupinga uamuzi wa Spika; Mimi naona amenishangaza zaidi kulipeleka hili suala kwenye chama chake. MKJJ amemuliza hili swali lakini naona alipitiwa kutokuuliza kuhusu upande mwingine wa hili saga.

Kama yeye anaona hakutendewa haki mbele ya Kamati ya Bunge la Jamhuri ni kwa nini basi anaona mpinzani wake Bw Mengi atatendewa haki na CCM..??

CCM watasikiliza suala hili wao wakiwa kama nani...na iwapo Mengi atatakiwa kwenda kutoa ushahidi itakuwa ni kwa mantiki ipi?
 
Ndg. wanaJF,

Katika habari kuu ya mchakato husika hapa, yaonesha MANJI anamtandao mkubwa tuu unaomsupport baada ya magazeti ya THISDAY kumkomalia na hela za walalahoi anazotafuna.

Kama mtakumbuka Makamba alimpigia sana debe la Ubunge Manji katika kampeni za ndanikwandani CCM alipokuwa RC, sasa Makamba ni KM ccm, hivyo ana nafasi kubwa ya kumteua tena Manji 2010.

Baada ya ThisDay na Kulikoni kuanza kuzimua uozo NSSF na PPF, Manji akaona hapa maji yapo shingoni, ndo akaanza kuwatafuta wabunge wa kumlinda....akampata mdanganyika Malima....! Story ikaendeleeeaaa... nk

JAMANI nani ataweza niambia kabla ya Ugomvi wa Mzawa MENGI na Ghabachori Manji, kuna pahala gani Manji alishawahi support Michezo?
...Nadhani Jibu ni....Hapana...Sasa kafumbuka macho, kajua akijikita kwenye michezo atapata support kubwa saaanaaaa! Huyooo kujikita YANGA, na simnamsikia anavyopaa hewani? mara kajichanganya na TMK wanaume....HIZO NDO PROPAGANDA za kujitangaza kuwa u mwema!

Hapa deal imechezwa kisawasawa, yaani ili kutusahaulisha na mamilioni yaliyofujwa kwa kununua Quality Group, ndo Manji kamtumia mtoto malima kudivert issue. Malima naye kwakutojua kuwa yatakuja kuwa hot kwake kajichokonoa, mara kaaza ooo Mengi anatumia vibaya vyombo vyake vya habari, mara oo....Sasa weye kid, kama ndivyo yakuhusuni? kwani wakati mwenzio anaumiza kichwa kuwekeza kwenye biashara..weye si ulikuwa washinda barazani kutwa wachezwa bao na kikombe cha khahawa mkononi? ulitazamia muwe sawa kwa mtindo huo? ona sasa yamekutoka macho pwaaa... u've had screw ur self!!!

Hivyo basi Malima anachokifanya sio kwa kutumwa na CCM bali kwa kutumwa na Bwana wake Manji. Pia Malima kumtumia Makamba barua kina uhusiano gani na mambo ya BUNGE? kama sio MAKAMBA+MANJI+MALIMA Wote ni wahujumu uchumi kwa kula pesa za walalahoi NSSF na PPF, wakati walengwa wastaaafu wanapiga miayo foleni kwa DAU na vilevile pesa hawapati! Wameshabeba hao MANYANG'AU!!!!!!!!!!!!!
 
Mkumbuke tu kuwa Makamba aliwahi kumbusu Manji miguuni huko Kigamboni na alitaka sana Manji awe mbunge wa Kigamboni. Kwa hiyo naiona connection ya Malima-Makamba-Manji (MMM) very clearly!
 
mwanasiasa,

Harusi ya mtoto wa Makamba wa kiume manji alitoa tshs ngapi? nadhani unakumbuka ishawahi kuongelewa humu au Bsc times....

FD
 
Mzee ES,

Kwa kuwa Mwanakijiji amemuhoji Mh Malima tusubiri tusikilize mahojiano ndio tutapata ukweli, pamoja na mambo mengine kama kweli Mh Malima kaajiriwa na Manji. Hii habari ya kupiga simu naona haina haja kwa sasa tusubiri mahojiano.

Ni kweli Spika ana mamlaka ya kuamua kwa kadiri anavyoona inafaa kwa mujibu wa Kanuni 4(2)

Lakini kanuni ya Bunge 88 (1), (3), (5), (6), (7), (9), na (11) zinaweka utaratibu wa uwazi zaidi wa kupokea taarifa ya kamati ya kudumu nakuiwasilisha kwa Bunge ili ijadiliwe na iridhiwe na Bunge.


Hapa inatushangaza wengi kwani Spika kwa sababu ambazo hakuzisema pamoja uzito wa kesi ambayo ilikuwa na mvuto mkubwa bado hakuona umuhimu wa kuruhusu mjadala wa Wabunge kwa suala lenye uzito wa namna hii na badalå yake akajifungia ndani na akaona busara zake pekee yake zitatosha kuamua suala kubwa kama hili. Katika hali ya kawaida alitakiwa atumie utaratibu wa utawala bora na demokrasia ya kibunge ambao ndio hutumika mara nyingi ktk kuamua mambo mbalimbali.

Kuanza kumnyooshea kidole Mh Malima kuwa ndiye chanzo cha mamilioni kutumika nadhani sio sahihi. Ikumbukwe pia katika uamuzi wa spika, kifungu 9.3. pia kimemtia hatiani Mengi nanukuu "Na kwa kuwa kitendo cha Bw Mengi cha kukosea utaratibu kwa kutumia lugha ya kuudhi, kukanusha matamshi ya Mh Malima kupitia vyombo vya habari na kuwa pia imemuathiri Mh malima"

Nakubaliana na Mzee ES kuwa ndio price ya demokrasi mindhali tumeitaka demokrasi then we have to pay! Na kama tunaona ni ghari basi turudi tulikokuwa kwa kura za NDIO na HAPANA.

Juu ya yote narudi kusema mtu alietuingiza kwenye matumizi ya milioni 100 ni Spika mwenyewe kwa jambo lingeweza kusuluhishwa kirahisi.

Tusubiri mahojiano.
 
Wana JF,

Huu mjadala kwa kiasi kikubwa hauna maslahi kwa Taifa kuendelea kuumiza vichwa vya watu, lakini unahatarisha USALAMA WA TAIFA, na inawezekana kabisa wahusika wakawa sawa na WAHAINI ama wanajaribu NGUVU ZAO kama zinaweza kutawala ama kuyumbisha nchi.

Kwa harakaharaka tunaweza kuona kuwa ni mambo madogo, lakini hebu tujiulize;

1-Kama Mengi na magazeti yake wameshambuliwa na hadi sasa wanaendelea kushughulikiwa eti kwa sababu tu wamepingana na maslahi ya watu fulani, je, ni wangapi watafurukuta?
2- Ikiwa baada ya Mengi sasa naye Spika Sitta, ameanza kushughulikiwa na malengo ni hata KUMNG'OA, je nini maana yake?

3-Spika kawaudhi wanamshughulikia, Waziri Mkuu akiwaudhi itakuaje? Rais naye akiwaudhi ama kama tayari ameshawaudhi, nini kitafuata kama si UHAINI, ama HUJUMA? MWENYEZI MUNGU AEPUSHIE MBALI.


JAMANI AMKENI MASLAHI NA USALAMA WA TAIFA UKO HATARINI; ZINDUKENI: HII NI HATARI, TUSIKUBALI KUBURUZWA KUWABEBA MAFISADI.

MUNGU INUSURU TANZANIA, MUNGU MNUSURU RAIS WETU.
 
Wana JF,
Naamini sasa kuwa kuna haja ya kuunganisha haya matukio na mengine, kwani hili sio jambo la kawaida kwa mbunge te4na wa ccm kukataa maamuzi ya spika na mbunge mwenyewe ndio huyo aliyeingia bungeni kwa mara ya kwanza hapa lazima kuna mkono wa mtu.
Nimejaribu kulifuatilia kwa karibu na nimepewa majibu kuwa kitendo cha spika kueleza vyombo vya habari kuwa bunge hili la mwezi april ataruhusu kujadiliwa kwa ishu ya RICHMONDni kumtafuta ugomvi EL.
Wajuvi wa mambo wameendelea kueleza ya kuwa kijana malima ana support ya mzee wa DOWANS hivyo hayupo peke yake kwani inaonekana kuwa spika anataka kuwaweka akina EL na wenzake hadharani.

Tulifuatilie hili jambo kwani pia habari zinapasha ya kuwa ni ama za spika au EL hapo wanasema ni mpaka kieleweke,
Wanatoa mifano kuwa safari za EL za hivi karibuni amekuwa akiambatana na wabunge wale ambao ni opionion makers kule bungeni na huwa fedha za safari hizo huwa zinakuwa sponsored na mzee wa DOWANS kwa kutumia zile pesa za import support.
Naishia hapa kwa leo.
 
CV mheshimiwa malima fungua hapa

http://www.parliament.go.tz/bunge/Mp_Cv3.asp?PTerm=2005-2010&fpkey=427&vusername=GUEST")
 
--------------------------------------------------------------------------------

Members Profile >> MP CV
--------------------------------------------------------------------------------

Malima , Adam K.
GENERAL

--------------------------------------------------------------------------------
ID No.: MEMBER'S PICTURE
Salutation:
First Name:
Middle Name:
Last Name:
Member Type:
Constituent:
Political Party:
Office Location:
Office Phone:
Office Fax:
Office E-mail:
Member Status:
Start Date:
End Date:
Date of Birth

--------------------------------------------------------------------------------
EDUCATION
School Name/Location Course/Degree/Award Start Date End Date Level
University of London (SOAS) MSc (Econ) 1994 1995 MASTERS DEGREE
Univesity of London (SOAS) Post Graduate Diploma (Econ) 1993 1994 POSTGRADUATE
University of Hauana (Cuba) MSc (Economicy) 1984 1989 MASTERS DEGREE
Shaban Robert Secondary School O-Level Education 1979 1982 SECONDARY
Upanga Primaru School Primary Education 1972 1978 PRIMARY

--------------------------------------------------------------------------------
CERTIFICATIONS
Certification Name or Type Certification No. Issued Expires
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
EMPLOYMENT HISTORY
Company Name Position From Date To Date
Private Consultants Business Consultant 2002 2005
Pwani Finance Business Consultants Consultant 1996 -
Bank Of Tanzania (BOT) Financial system 1990 1996

--------------------------------------------------------------------------------
POLITICAL EXPERIENCE
Ministry/Political Party/Location Position From To
No items on list



PUBLICATIONS
Description
Published Date
No items on list

--------------------------------------------------------------------------------
SPECIAL SKILLS
Skill Name or Description Years Experience Acquired Through Skill Level
No items on list
 
Haijakaa vizuri lakini..Sorry

Hakwenda A level??? huko BOT nako?? ni mtoto wa Malima, mtoto wa Mbowe, mtoto wa flani ndio wanapata kazi huko..

FD
 
Fikiraduni,

Sijakupata hapo, una question Mh Malima kupewa kazi BOT? Mtoto wa Mbowe kafikaje huku tena jaman1? yaani thread haitimii mpaka mumtaje Mbowe? au ndio tishio kwenu? kama wapinzani mbona wapo wengi tu akina Lipumba, Mbatia, Mziray, Mapalala nk.

Muacheni Mbowe alone mfimfanye daraja la kuhalilisha ufisadi wenu na CCM yenu.
 
mpaka kieleweke, naona umeongeza chumvi katika kidonda. Rejea maneno yangu hapo juu, changanya na yako, utapata bonge la "mkorogo" ambao ni sumu kali. YAANI NAOGOPA HATA KUANDIKA LAKINI, mambo ni makubwa kuliko uwezo wa kompyuta tunazotumia. Hapo mambo haya yanahusu, PESA NA MADARAKA ya WATU, mambo ambayo kote duniani yanagharimu ajira na hata maisha ya watu. MWENYEZI MUNGU TUNUSURU, maana tusijesikia watu sasa ndani ya CCM wameamua kuchukua FOMU ZA URAIS 2010 na si 2015. Hiyo nayo itakuja kuwa hoja inayojitegemea. LISEMWALO LIPO. MZOEA VYA KUNYONGA VYA KUCHINJA HAVIWEZI. Watu sasa udenda unawatoka na 2015 ni mbali sana kwao. KAZI KWENU wana U2 munaosoma nyaraka za humu ndani kama kweli munazingatia maslahi ya TAIFA, wakati ni huu
 
Halisi: Usalama wa taifa??!! That used to be the easiet and cheapest way to evade criticism, kumbe bado inatumika!!?
 
Kyaruzi,

Huwa wanaonielewa wanajua simpendi wala kumchukia mtu, cheki kokote pale kama nilikuwa namkandia Mbowe... NO, kwahiyo hukunitendea haki kutafsiri niliyoandika kwasababu hukuelewa kama ulivyosema.

Nimemtaja Malima (CCM) na Mbowe (Chadema), sasa wapi nimekuwa biased na CCM???!!!!. Ok mimi ni mwanachama hai wa CCM, so what???!!

Ngoja nikusaidie mheshimiwa: Nilikuwa na maana kuwa watoto au familia au ndugu au marafiki wa wakubwa au vigogo au majina makubwa au wafanya biashara wakubwa au koo kubwa ndio wanapewa kazi BOT???.

Umeelewa sasa mheshimiwa?

Asante.
 
mkjj,
hongera kwa mahojiano yako na mh malima.
maoni,naomba wakati mwingine muulize mtu swali la moja kwa moja, na kama anakwepa mmbane pale pale.kuhusu swali la kazi akulijibu inavyopaswa.malima ajakanusha wala kukubali kuwa yeye ni mfanyakazi wa manji.
naungana na mzee es kuwa malima ni mfanyakazi wa manji
 
Naona wadau mmewakazania watu wawili tu, yaani Malima na Mengi. Kwa maoni yangu naona kuwa aliyelikuza suala hili ni mheshimiwa Spika mwenyewe Samuel Sitta.

Spika alitataka aenekane ni mzuri kwa pande zote kitu ambacho kwa kweli hakiwezekani; ukweli ni kwamba katika mtafaruku huu mwenye haki alikuwa apate haki yake kwa kuzingatia kanuni za Bunge. Baada ya kuona kuwa Malima amepotosha ukweli ilitakiwa amuadhibu kwa kufuata kanuni na sheria za Bunge full stop! Malima angekata rufaa baadaye na yasingetokea yalitotokea; kodi zetu kwa mamilioni yameteketea bure! Ni vema Spika ukumbuke kuwa huwezi kuwa mwema kwa watu wote, uvuguvugu wako ndiyo unaokuponza hapo, maana si Malima wala Mengi aliyekuomba uwe msuluhishi wao matokeo ndiyio hayo kujipachika usuluhishi bila kuombwa.

Mheshimiwa spika, bado unayo safari ndefu, kuteleza si kuanguka; jifunze, jipange upya safari bado ndefu!
 
mkjj,
hongera kwa mahojiano yako na mh malima.
maoni,naomba wakati mwingine muulize mtu swali la moja kwa moja, na kama anakwepa mmbane pale pale.kuhusu swali la kazi akulijibu inavyopaswa.malima ajakanusha wala kukubali kuwa yeye ni mfanyakazi wa manji.
naungana na mzee es kuwa malima ni mfanyakazi wa manji

nimekusikia, lakini kama alivyosema yeye suala lake halikumhusu Mengi na wala yeye hakumtaja Mengi. Ni kweli kama walivyosema wengine aliyeboronga suala hili ni Spika ambaye ameonesha udhaifu mkubwa sana wa kushughulikia masuala yanayohusu wana CCM wenzake. Spika Sitta amekuwa mahiri kupiga mkwara wapinzani na kuchukua hatua dhidi yao lakini katika hili la Malima ameboronga vibaya sana na historia itamhukumu vilivyo.

Hata hivyo, upande mwingine ni uamuzi wa Malima kukimbilia CCM kutafuta msaada. Nafikiri atajutia uamuzi huu. Kwa maoni yangu angeamua kutumia Bunge hilo hilo kutafuta haki yake.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom