Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,812
- 11,989
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria, Dkt. Joseph Mhagama amesema maandamano sio suluhu ya kupata muafaka wa maoni ya Muswada wa Sheria ya Uchaguzi na kuongeza kuwa tayari maoni hayo yameshapokelewa na kupelekwa Bungeni na kamati yake inaendelea kuyachakata.
Amesema “Hali ni tofauti na baadhi ya Wadau wengine wanavyodhani wakiwemo CHADEMA, Sheria za Uchaguzi zinazotungwa na Sheria za Uchaguzi zinazofanyiwa marekebisho hazitazingatia maandamano yanayoendelea au yaliyopangwa, zitazingatia maoni ya Wadau waliofika mbele ya Kamati za Bunge na kwa nafasi hiyo maana yake ni Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria.
“Kanuni ya 77 Kanuni Ndogo ya Pili na Kanuni ya 136 Kanuni ndogo ya 9 ya Kanuni ndogo za Bunge Toleo la Mwaka 2023, inataka baada ya Serikali kuwasilisha Miswada Bungeni, Bunge linazipeleka kwenye Kamati mahususi Miswada hiyo na pia inawaalika Wadau wote wenye maslahi na miswada hiyo ya Sheria kuja mbele ya Kamati kulishauri au kuisaidia Kamati kuhusu hoja mbalimbali zilizopo kwenye miswada.
“Kwa kuzingatia hilo, Spika alitoa Tangazo akaita Wadau, Muswada huu ulipata mwitikio mkubwa, Wadau walioshiriki kwa siku nne ni 1,707 zikiwemo Asasi za Kiraia zaidi ya 400, Viongozi Wakuu wa Dini na CHADEMA pia walikuja kupitia BAWACHA, Umoja wa Vijana (BAVICHA) na Katibu Mkuu John Mnyika.
“Tumeshangazwa na maamuzi ya chama kimoja kati ya vyama 13 vilivyokuja kutoa maoni kuna na maazimio ya kufanya maandamano.
“Pia Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu wa CHADEMA wanajua utaratibu wa utungwaji wa Sheria, Miswada imeshatoka Serikalini na ipo Bungeni, Bunge ndilo lenye mamlaka ya kutunga Sheria, wanajua Bunge halipokei maoni kiholela.
“Bunge lina wawakilishi wa Watanzania wote, Bunge ndilo litajadili kifungu kwa kifungu, kipi kipite na kipi kisipite, wanachokifanya kwa sasa ni kuwavuruga Watanzania kutaka kulivuruga Bunge lisitekeleze wajibu wake, wanachokifanya ni kama kuwadharau watu wote waliotoa maoni mbele ya Kamati, kwamba maoni yao ni bora kuliko maoni mengine ya wote.