Barua ya Adam Malima kumpinga Spika!

Status
Not open for further replies.
Mwanakijiji,
sijasikiliza mahojiano, lakini inaelekea Spika alikuwa anajaribu kumsaidia Adam Malima. Kwa mujibu wa Spika, ilionekana kwamba ushahidi wa tapes alizotoa Malima ulikuwa haulingani na matamshi yake ndani ya Bunge? Kwa kanuni za Bunge hilo ni kosa.

Zaidi, hii kamati[majority] ilifikia vipi uamuzi kwamba Adam Malima hana makosa? Vilevile hao dissenters waliandika nini kwa Spika?

Hili suala inabidi kuliangalia toka ALL ANGLES. Labda mahojiano ya Malima na KLH yanaweza kutufumbulia hiki kitendawili.
 
Jinamizi la Nidhamu ya Chama, litamkaba Malima!

Na. M. M. Mwanakijiji

Aliyedhania kuwa sakata la Mhe. Malima na mfanyabiashara Bw. Mengi limekwisha alidhania vibaya. Tulioadhani kuwa baada ya uamuzi wa spika wa tarehe 8 Februari, 2007 ambapo aliamua kuitisha mkutano wa usuluhishi kati ya watu hao wawili mashuhuri tumejikuta tumedanganywa kuachwa solemba. Suala hili kwa sababu fulani bado liko hai na halioneshi ni jinsi gani litamalizika hii karibuni. Siku chache zilizopita Mhe. Samuel Sitta (Spika) amesema kuwa suala hili kwa vile linamhusisha na yeye na inaonekana kuna watu hawakuridhika na maamuzi yake basi litazungumzwa tena Bungeni. Kabla hata kikao hicho hakijasikiliza, mmoja wa wahusika wakubwa wa suala hili Mhe. Adam Kighoma Ali Malima (Mkuranga - CCM) ameandika barua ya kutoridhishwa na uamuzi wa spika na hususan kutoridhishiwa kwake na utaratibu mzima aliotumia spika kufikia uamuzi huo wa kuitisha usuluhishi. Bw. Malima ameandika barua hiyo kwa Katibu Mkuu wa CCM ili kuweza kupata nafasi ya kusikilizwa malalamiko yake na hivyo kutafuta suluhisho la kichama zaidi kuliko lile lililopatikana au kupendekezwa na Spika. Bw. Malima amehisi kuonewa na kutotendewa haki.

Msingi mkubwa wa uamuzi wa Mhe. Malima kuandika barua hiyo ni kujaribu kutafuta njia muafaka ambayo itawaweka sawa viongozi hawa wa CCM na hivyo kwa kutumia vikao vya chama hicho basi kujaribu kulimaliza jambo hili kwa heshima na taadhima bila kuendeleza malumbano yasiyo ya lazima. Kwa maoni yake ni kuwa kwa vile yeye ni Mbunge wa CCM na Spika ni Spika anayetoka CCM basi uongozi wa juu wa chama chao unaweza kabisa kutafuta muafaka na kusikiliza hoja za Bw. Malima na hivyo kupata usuluhishi utakaokubalika na pande zote. Kwa maneno mengine, Bw. Malima ana imani na taratibu za chama katika kushughulikia migogoro ya wanachama wake. Bw. Malima anaamini kabisa kuwa kwenye vikao vya huko Dodoma basi kutapatikana suluhisho hilo ambalo litazingatia ukweli wa mambo halisi na hasa kutengua uamuzi wa spika.

Tatizo ni kuwa kabla ya kuandika barua hiyo, Bw. Malima hakuambiwa kuhusu lile jinamizi kubwa lililoko CCM, jinamizi ambalo linaweza kula na kumaliza, ingawa mara nyingi linakula na kubakisha. Ni jinamizi hilo lililowakaba kina Maalim Seif na Shaaban Mloo wakatimuliwa, ndilo jinamizi lililomkaba Mrema akatimka, na ndilo jinamizi hilo hilo lililowapa watu mishtuko ya moyo kila likitokea. Hili jinamizi ni chombo kikubwa kabisa ndani ya CCM ambacho kinawafanya watu wanyamaze na kunywea kama wamemwagiwa maji toka Makambako!! Bw. Malima hajajiandaa kusimama mbele ya jinamizi hilo.

Kabla sijaendelea ni bora niwatajie jina la jinamizi hilo, kwa wengi jinamizi hilo huitwa "nidhamu ya chama". Nidhamu hii ya chama ndio imehakikisha kuwa kuna kuonekana umoja na mshikamano ndani ya chama na ndilo lililohakikisha uwepo wa makubaliano ya pamoja na uwajibikaji wa pamoja ndani ya chama. Jinamizi hilo ndilo limesimamia kwa kiasi kikubwa nidhamu ya uongozi ndani ya Chama cha Mapinduz na hivyo kukifanya chama hicho kuonekana kuwa na umoja unaokosekana katika vyama vingi vya upinzani. Hili ndilo jinamizi ambalo Bw. Malima anatarajia kuweza kulishawishi hadi kukubali hoja zake. Juhudi za Bw. Malima ni kama juhudi za kushawishi jini lililofunguliwa kwenye chupa lisikumeze wakati lina njaa ya miaka 100 ya kifungo! Kwa yeyote anayechunguza masuala ya kisiasa ya Tanzania na ni mchambuzi aliyebobea kama wenu mtiifu, Bw. Malima hana nafasi ya kushinda au kujenga hoja ikakubalika mbele ya jinamizi hilo.

Njia pekee ambapo Bw. Malima anaweza akaondoka akiwa na sura ya ushindi ni pale ambapo vikao vya juu vya CCM vitakapoamua kukataa kusikiliza hoja zake na kumlazimisha kulirudisha suala hili Bungeni. Kwa vile suala hili limeanzia Bungeni na kuhusisha wabunge kwa viongozi wa CCM kuamua kulizungumzia pembeni na kulitolea maamuzi itakuwa ni kosa kubwa kwao na kufanya jambo ambalo CCM halina mamlaka nayo, nalo ni kuichukua kesi toka Bungeni na kuizungumza kwenye vikao vya Chama. Kama CCM inatambua uzito wa Katiba, haiwezi hata chembe kukubali kulisikiliza shauri hili hadi pale taratibu zote za Bunge zitakapofikia kikomo. Kwa vile Spika ameshasema wazi kuwa jambo hili litazungumzwa na Wabunge katika kikao kijacho, kitu chochote ambacho viongozi wa CCM watafanya na vikatafsiriwa kama kujadili suala hili nje ya Bunge, basi itaonekana ni kiburi cha hali ya juu cha CCM kuweza kuingilia shughuli za Bunge. Ni kwa sababu hii peke yake CCM itakaa kulizungumza jambo hili.

Endapo itatokea kuwa CCM itaamua kusikiliza shauri hili na kujaribu kuwaita Mhe. Malima na Mhe. Sitta ili kutafuta suluhisho, basi atakayeshindwa atakuwa ni Bw. Malima. Hili halina ubishi. Jinamizi hilo litamkaba, litamkunja, na kumpa ndoto mbaya mheshimiwa huyo kijana mpaka ajute kwa nini alilipeleka shauri hilo kwenye vikao vya CCM. Akitoka kwenye vikao hivyo ni bora akimbilie kupimwa msukumo wa damu! maana wengi hujihisi wamekimbizwa mchakamchaka na jinamizi hilo. Mhe. Malima atashindwa mbele ya nidhamu ya chama. Nitakuambia kwa nini.

Kwanza kabisa, kwa Mbunge kijana kama yeye kumshtaki mbunge mwenye sifa kama za Sitta ni kujtakia mabaya. Bw. Sitta ana nafasi ya pekee na ya kuonewa wivu. Bw. Sitta kwa kutumia watu mbalimbali ndani ya CCM aliweza kupanga na hatimaye kufanikisha mapinduzi ya kumng'oa Spika mkongwe nchini Bw. Pius Msekwa kitu ambacho watu wengi hawakutarajia ukizingatia umaarufu wa Bw. Msekwa. Kuangushwa kwa Msekwa na baadaye uthatibiti wa Spika kutetea maslahi ya Wabunge kumemfanya Bw. Sitta kuwa gwiji wa mambo ya Bunge. Mtandao uliomsaidia kumweka Sitta madarakani bado una nguvu na kama Bw. Malima alikuwa hajajiandaa kupambana nao (wengi wako kwenye vyombo vinavyosimamia nidhamu ya chama) basi atashangazwa ni jinsi gani watakuja kumtetea Bw. Sitta.

Jambo la pili ni kuwa historia ya Bw. Malima na CCM siyo historia ya mtoto aliyelelewa na kukulia ndani ya Chama. Bw. Malima alitoka chama cha Upinzani ambacho baba yake inadaiwa alishiriki kukiunda na hata kupata kwake nafasi ya kugombea Ubunge CCM kulikuwa ni kwa kubebwa na CCM kwani kwenye kura za maoni alishika nafasi ya tatu. Hivyo, kuna baadhi ya "wakubwa" ndani ya CCM wanaona kitendo cha "ubishi" cha Malima kuwa ni masalio ya roho ile ya upinzani, roho ya kuhoji, na roho ya kukosoa. Kuna baaadhi ya watu wanaweza kumuona Bw. Malima kama siyo "mwenzao" licha ya kuwa na kadi ya chama kimoja nao. Historia hii inaweza kumuumiza kweli Bw. Malima kwani jinamizi hili la CCM halisahau kirahisi hivyo!! Hili jinamizi linakumbukumbu kali kama nini na halichelewi kuiita kumbukumbu hiyo pale inapohitajika.

Jambo la tatu ambalo bila ya shaka litamwangusha Bw. Malima mbele ya jinamizi hilo la CCM ni maneno yake mwenyewe katika barua hiyo. Kwa jinsi ilivyoandikwa barua hiyo "inamshtaki" spika mbele ya viongozi wa juu wa CCM. Kitendo cha Malima kutokukubali maoni na "busara" za Spika na kuacha jambo hili limalizwe kimya kimya na kitendo cha yeye kuendelea kuhoji maamuzi hayo ya spika, kwa viongozi wanaolisimamia jinamizi hilo, Bw. Malima anaonekana mwenye utovu wa nidhamu. Ingawa nia yake ni njema na sababu alizoa zina mvuto wa mantiki, lakini kitendo cha yeye kubishana na spika hadharani na baadaye kuandika barua ya uchongezi dhidi ya spika ni utovu mkubwa wa nidhamu ambao viongozi wa juu wa CCM hawawezi kuvumilia, kufumbia macho, na kutokufuatilia. Hata kama CCM itaamua kurudisha suala hili Bungeni, Bw. Malima ameshatiwa alama na viongozi hao. Kama kulikuwa na nafasi ya Uwaziri au Unaibu nafasi hiyo imepeperuka kwani kumpa nafasi hiyo itaonekana kumzawadiwa kwa kitendo cha kumuumbua spika.

Jambo ambalo Bw. Malima anaweza kufanya ili kujiepusha na jinamizi hilo ni kuondoa mara moja barua hiyo na kukubali usuluhishi wa spika. Akiendelea kung'ang'ania msimamo wake wa kuona kuwa ameonewa na hivyo "kupigania" haki yake mbele ya dubwasha hilo, kwa hakika Bw. Malima atakuwa amejimaliza mwenyewe kisiasa. Sitashangaa wapinzani wakianza kumrushia ndoana!! Pamoja na hayo yote, maajabu duniani hutokea, Daudi alimwua Goliathi! tusishangae kama Bwana Malima akalishinda jinamizi hilo, kwani wanaolisimamia ni binadamu kama yeye!! akijenga hoja vizuri anaweza kulifanya jinamizi litoe machozi na kumsamehe, kwani hata Simba huzaa na kuna mahali niliwahi kuona picha ya simba amepewa kikombe cha chai!! Bw. Malima anaweza kutushangaza. Tusubiri tuone.
 
Mzee Mwana KJJ

Nimesikia mahojiano yako lakini nimegundua kwamba jama kasoa lakini hana ajualo maana hata kujibu maswali hawezi .

Malima kashindwa kujibu swali kama kawahi kufanya kazi kwa Manji katika maisha yake na kakwepa kujibu swala la yeye kukihama Chama chake cha sasa .

Kibaya zaidi nimegundua kwamba CCM iko juu hata zaidi ya Bunge ndiyo maana sasa Malima is twisting the issue na anakimbilia kwenye chaka kubwa .

Pole sana Wadanyika
 
Niliwahi kusema haya pindi tu spika alipotoa uamuzi wake. Sasa yangu macho na masikio!
 
Nani anajua who is behind Malima?Na hiyo jeuri ameipata wapi ya kwenda kuonana na jinamizi?Je Unafikri jamaa amekurupuka?Aliwezaje kupitishwa ilhali alishindwa kura za maoni?
 
KNKCU, jibu la swali liko litajulikana hivi karibuni.. ila msishangae akajikuta akisimama peke yake!!
 
Nimezungumza na Katibu Mkuu wa CCM Mhe. Makamba na amehakikisha kuwa barua ameipokea na bado hajaitolewa uamuzi. Kwa mtazamo wake amesema kuwa Bw. Malima amefanya jambo sahihi la kuleta suala hilo chamani na yeye kama Katibu Mkuu ataamua hatua za kufuata kama ni kulipeleka jambo hilo kwenye Kamati ya Wabunge wa CCM kujadiliwa au kulileta kwenye vikao vingine vya chama.
 
Hili ndiyo linanipa picha ya kujenga dhana kwamba Malima hayupo pekee yake na Huenda hata hilo swala la kuandika barua kuna waliomtuma afanye hivyo,Ninaukumbuka urafiki wa makamba na Manji wakati alipokuwa mkuu wa mkoa wa DSM hadi ilifikia huyo Mzee Kumpigia Debe Manji kule kigamboni/Temeke alisema wa mchague Manji kwani yeye huwa anatoa sana na hata amewatengezea baadhi ya Bara Bara Kule Temeke Sasa nikiunganisha Katibu Mkuu Makamba+ Malima=Manji................Nisiowafahamu sijui ni wangapi.........................!
 
It is scary!
 
Sikujua kama CCM ina wasomi lakini wengi ni vilaza akiwemo Malima .Pia Makamba ni msanii hana ajualo yeye na hapa ndipo tutaona Tanzania kama Chama kinaweza kuzima Bunge na kuamua vinginevyo . Kweli naamini kwamba CCM ikishindwa kwa kura watapigana vita na kuua watu hovyo .
 
Mwanakijiji,

Nakubaliana na wewe na kama nilivyotangulia kusema awali tumeuona tu mwanzo wa jambo hili lakini mwisho wake safari bado ni ndefu sana. Kibaya zaidi safari yote hii ni kwa gharama zetu sisi tax payers.

Sina uhakika kipi kilianza baina ya barua ya Mh Malima kwa katibu Mkuu na uamuzi ( kama alivyonukuliwa)wa spika kuwa jambo hili litajadiliwa tena bungeni, kwa madai kuwa hata yeye spika amevunjiwa heshma yake. Lakini nilicho na uhakika nacho ni, kama litarudi bungeni then barua ya Mh Malima itakuwa haina maana yeyote kwani kama alivyoweka wazi mwanakijiji itakuwa ni kinyume na utararibu kujadili mambo ya bunge vichochoroni.

Itawezekana tu kulijadili jambo hili kwa kutumia utaratibu wa CAUCUS. Huu ni utaratibu unautumika ktk bunge na hata katika vikao visivyo vya bunge ambapo wabunge wa chama kimoja wanakutana kabla ya kikao rasmi cha bunge na wanaweka mkakati namna ya kwenda kujenga hoja kwa dhidi ya wabunge wa vyama vingine. Na hata wabunge wa vyama vingine wana Caucus ya kwao. Na kwa kuwa barua imekuwa addressed kwa katibu mkuu ambae kwa bahati nae ni Mbunge wanaweza kulimaza kichama huko huko.

Kwa muktadha huo basi, ningependa kutofautiana na Mzee Mwanakijiji kuwa katika jambo hili kuna jinamizi ambalo litamuangukia Mh Malima. Kwa bahati mbaya sana mifano aliyoitoa Mwanakijiji haishabahiana na sura halisi ya jambo hili, na imejikita katika misingi dhaifu legevu sana. Mifano ya Maalim Seif, Shaaban Mloo na Augustine Mrema haifanani kabisa na kesi hii. Mrema alikuwa na frustration zake baada ya kung'olewa uwaziri na ndani na naibu waziri mkuu na kuwa waziri kazi. Wakati vuguvugu la vya vingi na haraka yake kwenda Magogoni akaona itakuwa short cut kwenda opposition indeed it turned to be a wrong cut! same as Seif na kiherehere chake cha kutaka kuwa the 1st Mpemba kuwa rais znz. aliposhindwa na marehemu Abdulwakil akawa mwingi wa kufanya subortage na kwa kuwa marehem Mwalimu alikuwa ni master wa ma intrigue akamng'oa yeye na wapambe wake akina Mloo, Pandu, Hamad Rashid etc. Hivyo nadhani majinamizi hayo hayafanani na hali ya Mh Malima hususan kwa kuzingatia Mh Malima alishapitia kwenye majinamizi uliyoyadai ( yeye baba yake walihama ccm )

Hili la wana CCM kupelekana kwenye vikao na wakatoka salama sio jipya na sio jinamizi kama ulivyodai. Labda tu nikupe mfano Mzee Malecela alikatwa mara mbili kwenye mbio zake za kutafuta urais, hii ya mwisho pale white house Dodoma ndio ilikuwa mbaya zaidi kwani Mwalimu hakuwepo na waliomkata ni Kamati Kuu.

Siku ya pili yake kwenye NEC Mzee Malecela alikata rufaa na miongoni mwa madai yake ni kuwa chama kiliwezaje kumuamini kumpa umakamu wa Mwenyekiti kwa miaka yote hiyo hadi leo Kamati kuu inakata jina lake lisiende kwenye NEC. Mh Mzindakaya alijaribu kumtetea sana walau wapeleke jina lake kwenye NEC halafu liende Mkutano mkuu na kama hafai waamue wajumbe wa mkutano mkuu.

Jitihada zote hizo hazikusaidia na akapigwa chini. Je Mwanakijiji jinamizi hapo lilikuwa bado ndani ya chupa? Mfano mwingine ni Mh Shibuda aligombana na wana CCM wenzie karibu wote kanda ya ziwa, wakati wanakuja kwenye mkutano wakamshusha Dodoma kama Kuku!, leo Mh Shibuda ni Mbunge na actually aligombea urais!. je jinamizi hapo lilikuwa bado kwenye chupa?

Huyu Mh Sita spika walipokuwa wanagombea jimbo la urambo kabla halijagawiwa mara mbili na Mh Kapuya walifikishana mpaka kamati kuu. Na ugomvi wao mpaka leo haujaisha kama wana forum mtakumbuka Sitta alipopata U-spika alienda jimboni Urambo na Escot car ya polisi aliyoichukua kwa RPC Tabora kimwerumweru mbele Mh yupo nyuma kuwaonyesha watu wa Urambo kuwa yeye zaidi kuliko Kapuya! Wiki inayofuata Mh Kapuya akajibu mapigo akatua na dege la jeshi full mkoko Militaly Police (MPs) lundo!. Je jinamizi hapa lilikuwa bado kwenye chupa?

Hii hoja ya kuwa Mh Malima alikuwa upinzani na anapimana ubavu na heavy weight la ccm haina mashiko. Mh William Ngeleja ambaye sasa ni naibu waziri wetu wa madini na nishati alikuwa NCCR piga ua toka alipokuwa mlimani pale. Kana kwamba hiyo haitoshi Ngeleja katika mchakato wa ubunge kambwaga mkongwe mzee Shija na to make the matter even worse katika mchakato wa urais wa Muungano alikuwa kambi ya Sumaye! na leo ni naibu waziri ktk wizara nyeti kabisa. Hivyo Mwanakijiji hoja ya Mh kunyimwa uwaziri au unaibu nayo haina mashiko msingi wake ni legevu na lemavu sana.

All said and done kwa maslahi ya taifa na kwa busara zilizojaa CCM naamini watalimaliza amiccably.

Mungu Ibariki Tanzania
 
Masatu, inawezekana hoja zote hazitakuwa kama hivyo. Lakini, kama nilivyosema mwishoni mwa hoja yangu kuwa maajabu hutokea na uliyoyasema ni kweli yametokea. Ila hili la Malima na Spika mfano wake hakuna. Sitashangaa badala ya vikao vya CCM kulizungumzia wataamua kulizungumza kwenye Caucus ya Wabunge wa CCM. Vinginevyo tunakoeleka pabaya
 
Mwanakijiji na Masatu!
Hili swala hawawezi kulipeleka Bungeni moja kwa moja Lazima watatafuta kichaka cha kukimbilia na kichaka hicho ni wabunge wa CCM Kukaa kwenye chaka lao ndani ya bunge chini ya wanachokiita Kamati ya wabunge wa CCM,Unajua ni kwanini ?wanaavoid uwepo wa wapinzani kama litapelekwa moja kwa moja bungeni na sasa wanataka kujitia wanalifanya kichama zaidi Na hata kama wataamua kulirudisha Bungeni ni Baada ya wao kukaa kwenye kichaka chao na kukubaliana nini wafanye kwa pamoja Kama Chama ndani ya Ukumbi wa Bunge.
 
Tatizo kubwa na nilikuwa nimemuuliza Mhe. Makamba kama watalizungumza kwenye vikao vya chama nje ya Bunge. Hakukataa moja kwa moja lakini amesema yeye ndiye Katibu wa Chama na barua aliandikiwa yeye hivyo ni yeye ataamua ni wapi panapofaa kulizungumzia.
 
Masatu!

Mhh wewe mwisho! utakuwa ama kada CCM au ni M-NEC, hii ya Sitta V Kapuya ni mpya kwangu na niko hoi!. Anyway good analysis bro
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom