Mdee anasema wananchi wa Dar wakiona bajeti imepita au UDA imeuzwa wajue ni serikali ambayo imekataa kuwasikiliza wabunge wake. amemaliza na anapigiwa makofi na wabunge wote na hasa wa CCM
Kwa hali ilivyo hata mimi nilitegemea wangesitisha uchangiaji, hii inanipa wasiwasiKama hadi sasahivi bado mjadala unaendelea na waziri mhusika ama waziri mkuu hajaomba kuiondoa bajeti ili ikafanyiwe narekebisho stahiki, basi sina shaka yoyote kwamba bajeti hii itapitishwa.
Hizi kelele za wabunge wa ccm ni danganya toto, kapuya na idd simba ni wazawa wa ccm si rahisi kuwachinjia baharini, unless utokee muujiza.
Enzi za ba Mkapa haya yangetokea bungeni? Nani wa CCM angesimama hasiunge mkono hoja? Mapinduzi haya japo madogo yameletwa na nani? Nijuze
Je, hakuna mahusiano kati ya mapinduz haya na rais aliyeko madarakani?
yeye ni bora au mbovu ukilinganisha na ba mkapa?
Filikunjombe anasema bajeti hii anaipinga kwa moyo kwa nguvu zake zote, anaomba wabunge wao ni muhimili mwingine, sio serikali na wabunge wasiitetee serikali na amewaomba wabunge wa CCM waungane na wabunge wa upinzani leo wapinge bajeti hii.
Anasema wabunge wampe pole, kwani alitaka kuzama ziwa nyasa, miaka 50 ya uhuru wananchi bado wanasafiria mitumbwi, anahoji hii serikali kweli ni sikivu?