Bajeti 2011: Tanzania tunahitaji kufuta vyama vyote vya siasa tuanze upya!!

@New York, mimi nilishakudharau tangu majuzi, kwahiyo ulikuwa unajadili kitu ambacho haukifahamu wala haujui hiyo bajeti ni % ngapi pesa za ndani na % ngapi ni msaada wa wafadhili wa nje.
Sikutegemea mtu wewe yule yule kuja tena hapa jamvini na thread kama hii. huu ni uchovu wa mawazo na ni madhara ya elimu za ujanja ujanja za kuunga unga, na ninaona afadhali mara 1000 ya ccm hawa waliopo madarakani kwa sasa waendelee kutunyonya kuliko watu wa aina yako mnaodhani Tanzania ndio nchi ya kuja kufanya majaribio ya uongozi ili mtuibie.
 
USD 1,412,000,000 x 1500 = TShs. 2 trillion ambazo ndizo Wazungu wataturudisha kwa kisingizio cha Government Budget Support wakati walituibia kupitia makampuni yao
 
- Hukulazimishwa mkuu kujadili hoja, mimi najadili taifa naona unaijadili CCM, kwa nini usianziseh mada ya CCM na kodi, mimi yangu ni ya kufuta vyama vyote nchini!

Willie @ NYC, USA.
Where do you put the demarcation, utajadilije taifa bila CCM? kwani ni nani aliye unda serikali hii isiyowajibika?Kama nikufuta vyama vyote ulikuwa na maana gani kuweka thread hapa kuhusu tawi la CCM New York naukakomalia wiki nzima?Nakwambia waelekeze watu wako wa CCM waache kukumbatia rushwa wajipange kukusanya kodi. Wacha kutuchosha na majibu yako ya nyodo ati hatujalazimshwa kujadili hoja zako za kilimbukeni. Eti hoja yako ni kufuta vyama! naanza kupata mashaka na uelewa wako wa mambo, kwani vyama ndio vinakusanya kodi? Narudia tena kwa msisitizo mawazo na ushauri wako wapelekee Nape na Mukama wengine unatuchosha bure.
 
Yes ni kweli alisema hayo lakini unategemea huyo Dr. Slaa apeleke kodi kule TRA au ni wajibu wa TRA chini ya sheria zilizowekwa na uongozi uliopo kumwendea Dr. Slaa na kudai hiyo kodi. Mimi sielewi kuna uhusiano gani kati ya weak collection ya kodi na vyama vya upinzani at this point. Kama wale wanaotakiwa wai-collect hiyo kodi hawafanyi hivyo si wajibu wa serikali iliyopo kuchukua hatua? Kimsingi najiunga na wengi hapa kukubaliana na hoja kuwa kodi hazikusanywi inavyopasa lakini wewe unaelekea kutaka vyama vyote vichukue lawama - hiyo inatoa impression kwamba unaogopa kukilaumu CCM. Najua unasema huogopi mtu Willy na pengine ni kweli, lakini unavyong'ang'ania kuvilaumu vyama vingine vya siasa kwenye issue kama hii unatufanya hata wengine tunaokuona jasiri kuwa na wasiwasi.

- Serikali ya CCM haikusanyi kodi na wale vyama vingine tunaowalipa ruzuku kuwakosoa CCM na wao wamenyamaza kimyaa sasa unashangaa nini ninaposema kwamba tufute vyama vyote maana wote ni mzigo kwa taifa!

Willie @ NYC, USA.
 
Willie,
Ujue kuwa Rawlings aliweza kufanya aliyofanya kule Ghana kwa sababu alipindua nchi tena alikwenda hata against wakubwa wake jeshini ambao walikuwa pia wamenogewa na ulaji kama walivyokuwa politicians. The fact kwamba Rawlings aliweza tena mara mbili ilikuwa ni combination ya luck, na timing ya hali ya juu sana. Ili kufanya unalopendekeza la kufuta vyama vyote ni lazima atakayetoa mwongozo awe nje ya vyama vyote - in other words, jeshi tu ndiyo linaweza kufanya hivyo. Is that what you are suggesting? Na kama ni hivyo, tuambie straight basi.

- Duh! hapana haya ni mawazo yako, mimi ninachosema kinaeleweka sana siwezi hata siku moja kulilia kuongozwa na jeshi, never!

Willie @ NYC, USA.
 
@New York, mimi nilishakudharau tangu majuzi, kwahiyo ulikuwa unajadili kitu ambacho haukifahamu wala haujui hiyo bajeti ni % ngapi pesa za ndani na % ngapi ni msaada wa wafadhili wa nje.
Sikutegemea mtu wewe yule yule kuja tena hapa jamvini na thread kama hii. huu ni uchovu wa mawazo na ni madhara ya elimu za ujanja ujanja za kuunga unga, na ninaona afadhali mara 1000 ya ccm hawa waliopo madarakani kwa sasa waendelee kutunyonya kuliko watu wa aina yako mnaodhani Tanzania ndio nchi ya kuja kufanya majaribio ya uongozi ili mtuibie.

- Genius! tunajadili taifa hapa sio wewe wala mimi binafsi ndio unapokosea hapo unahangaika sana nakuona sana. ila unapoteza muda wako talking about kukudharau, sijui kama unaelewa vizuri on my side nilivyokushusha hadhi yaani ungejua, maana hata simu yako sitakuja kupokea tena jinsi nilivyokudharau kuna jamaa alionya mapema sana kuhusu mahusiano na wewe, finally nimejionea mwenyewe, karibu sana!

Willie @ NYC, USA.
 
Bill,
Sijaelewa title ya thread yako.....tufute vyama tuanzae upya?....wanachama si walewale?
 
Where do you put the demarcation, utajadilije taifa bila CCM? kwani ni nani aliye unda serikali hii isiyowajibika?Kama nikufuta vyama vyote ulikuwa na maana gani kuweka thread hapa kuhusu tawi la CCM New York naukakomalia wiki nzima?Nakwambia waelekeze watu wako wa CCM waache kukumbatia rushwa wajipange kukusanya kodi. Wacha kutuchosha na majibu yako ya nyodo ati hatujalazimshwa kujadili hoja zako za kilimbukeni. Eti hoja yako ni kufuta vyama! naanza kupata mashaka na uelewa wako wa mambo, kwani vyama ndio vinakusanya kodi? Narudia tena kwa msisitizo mawazo na ushauri wako wapelekee Nape na Mukama wengine unatuchosha bure.

- Mbona unahangaika sana nimekwamba jinsi ninavyokudharau wala huna sababu ya kujadili na mimi, I mean mbona bado upo tu na mjadala na wewe umesema ulishanidharau! ha! ha! kwani unalazimisha sana mjadala uwe kuhusu mimi kuliko taifa vipi mkuu?

- Ninasema hivi vyama vyote vimeshindwa kukusanya kodi, ni vyema tuokaondokana na vyote, tukaanza upya, wewe unasema nini achana na mimi siwezi kukusaidia anything!


Willie @ NYC, USA.
 

Ninasema hivi vyama vyote vimeshindwa kukusanya kodi, ni vyema tuokaondokana na vyote, tukaanza upya, wewe unasema nini achana na mimi siwezi kukusaidia anything!

Willie @ NYC, USA.
Hivi kuna chama kingine kina kusanya kodi ukiondoa hii serikali ya Magamba?
 
Bw. MALECELA nakubaliana na sehemu kubwa ya hoja zako lakini wafanyakazi hakuna hata mmoja anayeweza kukwepa kulipa kodi. Kodi zao zinafyekwa juu kwa juu katika mishahara yao, vile vile hakuna uwiano sahihi wa kodi anayolipa mfanyakazi na kodi anayolipa mfanya biashara kwa mfano mfayanyakazi mwenye mshahara wa TZS 2,000,000/= analipa kodi isiyopungua 500,000/= kwa mwezi sawa na TZS 6,000,000/= kwa mwaka. Mfanyabiashara mwenye turnover ya TZS 24,000,000/= kwa mwaka kodi yake haizidi 500,000/= kwa mwaka, hebu angalia imbalance hii katika kulipa kodi.

Labda kama unazungumzia zaidi zile posho za vigogo ambazo mfanyakazi wa kawaida hahusiki nazo, Wapo wafanyakazi hawapati hata safari moja nje ya kituo kwa mwaka mzima.

Kwa maoni yangu, wafanyabiashara wengi hawalipi kodi wakubwa kwa wadogo na hata wakilipa kuna loopholes nyingi sana za kuwafanya wasilipe kodi stahiki lakini vile vile kodi walizowekewa ni kidogo mno ikilinganishwa na wafanyakazi. Sisemi wafanyakazi wapunguziwe kodi bali uwepo uwiano sahihi kwa mapato ya kila kundi kwa maendeleo ya taifa letu, vinginevyo tutaendelea kukinga bakuli kwa nchi zenye walipa kodi mahiri huku sisi tukiacha mapato yakiishia mifukoni mwa mafisadi.
 
Ni swala la muda tu kama ilivyo hesabu za kutoa, time has come for a new leadership.tujiandae vizuri kupembua siasa zetu kwa miaka hii mitano ambayo kwangu mimi na baadhi ya watu itakuwa ni migumu sana coz bajeti haina kitu kabisa katika swala la maendeleo.tusifanye makosa tena mwaka 2015 kizazi chetu kitatulaumu.thanks
 
Wilium,

Nashukuru kwa maelezo yako. Ishu kubwa hapa si posho za wabunge na posho kwa wafanyakazi wa serikali wote wakiwemo wabunge. Tunafahamu kuwa kazi ya mbunge ni kuwawakilisha wananchi. Je kama ili afanye hiyo kazi ni lazima tumpe posho, analipwa mshahara wake ni wa kazi gani? Na hii inatokana na wao kutofanya unayoyasema kwenye post yako uzembe wote huo unatokana na wabungo kuwa wazembe ukiwaondoa wachache wa CDM.

Hii bajet yenyewe unayosema si wote wameisoma na utakuta kuna uwongo mwingi na usanii kibao lakini wao hawaoni hayo mambo yote ndio maana imefika mahali ili kuwaonyesha kwamba wananchi tuko serious na uzembe wao kama waajiri wao tunaaza kupunguza posho kama hawawezi waontoke waingie watu ambao wanaweza kufunga mikanda kwa angalau miaka mitata tukasoge mbele.

Embu niambie mchango wa mbunge kama Rwakatare, Megji, Komba, etc na wengine wengi ni kwenda kusinzia mle tu hawana cha kuchangia wala nini.

Mwisho naomba ufute kauli, miaka hamsini uzembe umefanya na CCM na si CDM wala CUF kwa hiyo ni muda wa kuiondoa CCM na kuiweka chama ha upinzani na si kufuta vyama vyote.

Thanks Natoa hoja
 
- Genius! tunajadili taifa hapa sio wewe wala mimi binafsi ndio unapokosea hapo unahangaika sana nakuona sana. ila unapoteza muda wako talking about kukudharau, sijui kama unaelewa vizuri on my side nilivyokushusha hadhi yaani ungejua, maana hata simu yako sitakuja kupokea tena jinsi nilivyokudharau kuna jamaa alionya mapema sana kuhusu mahusiano na wewe, finally nimejionea mwenyewe, karibu sana!

Willie @ NYC, USA.

Ahahahahahahahahhh!! mwee! Yaani mimi nikupigie simu kwa lipi? Wewe ni mtu ambae tunakutana hapa kwenye forum basi, na kama kuna watu huwa wanakupigia simu ni hao hao magamba wenzako.

For ur information sikutaka kuliweka hili wazi, lakini ningeomba nikueleze wazi, mimi nafanya kazi na watalii, tena watalii wawindaji, ambao wewe hata ukae Marekani milele hutoweza kukaa nao meza moja.

Na for more info, wageni wetu 70% wanakuja na private jet zao wenyewe tena Gulf stream, mimi nikiamuwa kuja kutembea USA nitakuwa ni mgeni wa most of American Rich Families, hii itakuwa ngumu kwangu kuja kuonana na wabeba box kama wewe, maana sitokuwa karibu na immigrant society.

By the way ningekuwa nahitaji ukaribu na wewe labda tungekuwa tayari ni marafiki kwenye facebook.
 
William,

Natumai Mwalimu ni mojawapo wa viongozi waliokuwa na nafasi bora zaidi kuweka mfumo imara wa kodi na kuusimamia. Kutokana na kauli yako kuwa hata mwalimu mwishoni mwa maisha yake alisisitizaa umuhimu wa taifa kukusanya kodi unaweza kuona alikuwa anakirii makosa yake ila kwa kulaumu waluioshindwa.

Nakubaliana na wewe sanaa kwenye kukosekana kwa uwajibikaji na majibu rahisi kwenye maswali magumu. Lakini ndugu haya yote yamelelewa na mfumooo huu uliopo toka uhuru. Inasahangaza kama ulivyokiri tuna wasomi bungeni lakini buree kabisaa..kwa nini????????? elimu yetuu taitizo au wahitimu wetu tatizoo??????
 
Chama cha Siasa ni mkusanyiko wa watu wanaoongoozwa na katiba wenye lengo la kuongaoza. Chama cha siasa kinakufa au kupoteza uhalali wake wa kuwepo pale kinapokosa wafuasi. Msajili wa chama cha siasa anaouwezo kisheria kukifuata chama cha siasa ambacho kitavunja sheria ya uanzishwaji wa vyama pamoja na miongozo yake. Pamoja na Mambo ya msingi uliyo yaelezea sijaelewa Unamaanisha nini unaposema tunahitaji kuvifuta vyama vya siasa.
 
hivi kweli wananchi tukianza kulima miogo yetu na tujitenge kabisa na shughuli za serikali na tukaunda kaumoja chetu na kuacha kuwasikiliza kabisa viongozi wetu na watoto wao wanaotaka kuja kututawala kitatokea
 
Bado natafuta misimamo ya William Malecella,
Huwa ananishangaza sana kujua ni nini anatetea na nini ana amini. Huwa anaingia na kutoka na kunifanya nimuone au nisijue ni nini hasa misimamo yake.

Labda kwenye post mia zaidi nitamwelewa. Ila kwa sasa nashangaa tu. Najaribu kutafakari je kavua gamba au kavishwa gamba sasa linamchanganya. Huwa kuna wakati anakuja na mada nzuri na changamoto ila hapo hapo anaogopa ukweli magamba huwa yanafikiri kinyume nyume.


Bado nasoma nikikuelewa ni kuwa unatetea nini nami nitajumuika.
 
Back
Top Bottom