Bajeti 2011: Tanzania tunahitaji kufuta vyama vyote vya siasa tuanze upya!!

Ni kama taifa la wendawazimu flani hivi, maana hata huwezi kusema ni walevi kwa sababu mlevi akiamka asubuhi huwa anakuwa mzima na productive tena, sisi taifa tupo pale pale tunazunguka tu kama taili la gari, na wale wasomi wetu ndio bure kabisaa, mijina mikubwa lakini hakuna faida yoyote kwa taifa. Bunge limejaa ma-Doctor, Wanasheria, Wahandisi, mpaka Wachumi, lakini mpaka leo umeme hakuna, ujanja ujanja tu na ujinga ujinga na kutafuta majibu rahisi rahisi ndio vimetutawala hili taifa

Watanzania ni watu makini sana; tunachokosa ni mwelekeo wa nini tunakitaka na tumetawaliwa na woga wa kutaka mabadiiliko; Ni kweli bunge letu lina Madokta, wachumi na wahandisi kibaya ni kuwa idadi yao wamezidiwa na wabunge vilaza hao idadi ya ni kubwa na inatisha na ndio wanaoligeuza bunge kuwa rubber stamp, kinachafanyika wakati wa vikao vya wabunge CCM ikiletwa hoja ya kuipinga serikali hutokea mbunge mmoja kilaza anachosema CCM JUU vilaza wengine wakiitikia kwa shangwe hoja imekwisha. Tunahitaji viongozi wenye upeo wa kuelewa wajaribu kuiga nchi kama Ghana inavyopiga hatua, hatuna haja kuiga Rwanda; Kagame anatumia zaidi AK47 na JELA kuhakikisha watendaji wa serikali wanatekeleza majukumu yao lakini kama ikibidi na iwe hivyo.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
Serikali kuwa na ufainisi zaidi ktk kukusanya kodi lazima tuwe na Information Technology IT ambayo itaweza kulink TRA ktk private sectors. Kuna business transanctions nyingi ambazo zinafanyika bila ya TRA kujua, hilo ni tatizo.
Jambo jengine kubalance budget lazima ukate matumizi. Hata kama bunge wanao vikao vingi, lazima serikali ikate matumizi kwa njia yoyote in order to balance the budget.

- POWERFULL, mkuu ubarikiwe sana maana haya yako ndio mawazo tunayohitaji hili taifa, safi sana!

Willie @ NYC, USA.
 
kwani waliotufikisha hapo si ni pamoja na baba yako john samwel malecela na CCM yake[/QUOTE

Tutalilia CCM na viongozi wake mpaka lini? Suluhisho la matatizo ya watanzania lipo mikononi mwa watanzania.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
William, ukiangalia sana utaona tanzania ilikuwa haina watu wa kujenga uchumi ila nguvu za chama tuu.Wasomi tuliokuwa tunawategemea sana ni wale waliofuzu Kigamboni, Hombolo na Korogwe vyuo vya propaganda. Sasa kweli tunaweza kujenga nchi na wasomi kama hao?Asilima 90% ya watanzania ni wakulima, wavuvi, na wauza sokoni, hebu fikiria serikali itapata wapi hela kama hao watu hawalipi kodi.Wengi wa wasomi wetu wanaojiita ma DR utaona wamesomea kutukana matusi nchi za ulaya magharibi na kuandika meno ya propaganda tuu wala hawajali kutatua tatizo la unemployment. Posho za wabunge ina maana moja tuu,WAZEE TAIFA LA KESHO na SIO VIJANA!
 
Aidha unadharau sana watanzania/wananchi ambao mimi naona wanaonewa sana,au huelewi politicaleconomics za tanzania i.e a bit shallow or deeply misinformed.
Hayo mashirika kumi na tano yanayolipa kodi,hebu jaribu kufafanua yanalipaje hizo kodi?Asilimia ngapi ya bei ya bia,sigara kwa mfano ni kodi ambayo mwananchi huwa analipa indirectly?....mafuta?
usiseme naenda nje yatopic, just answer this please?
Sijaelewa unataka nini hapa kwa kunilazimisha kuwa nawadharau Watanzania. Nadhani unahitaji kurudi nyuma na kusoma posts zangu upya na upoint specifically wapi nadharau Tanzania. Nimezungumzia weak/poor institutions na ukweli zinaexists. Angalia takwimu za watoa rushwa zinatoka wapi kama si taasisi nilizotaja. Ningependa tujadili hizo politicaleconomics za Tz unazodai niko mis-informed.
Kwa kifupi kelele hizi zote zinasababishwa na taasisi zetu. Labda nikuonyeshe inakuwaje. Mtu anakwepa kodi. Polisi wanapewa taarifa ya siri kuna watu badala ya kusafirisha mafuta kwenda nje wanauza ndani ya nchi au wanachanganya na mafuta ya taa. Wanakwenda pale wanatulizwa na rushwa au kimemo. Wakijitahidi kufika mahakamani, watu wanafanya timing kwenye case inaunguruma for years. Mahakama ikijitahidi kuwa makini, TRA wanabipiwa kule waje na estimate ndogo ya kodi, watapewa cha juu baadae. Unaona tatizo hapo? Hapa nazungumzia mfumo wa kitaasisi ulivyo na mapungufu.
 
mimi nadhani kabla ya kufanya chochote katika nchi hii kwa sasa kitu cha kwanza ni katiba,
pili mfumo wa utawala wa nchi yetu ujulikane na viongozi wawe wana wajibika moja kwa moja kwa
wananchi na sio mtu aliyewateuwa,
baada ya hapo tuifute CCM kungoa mzizi wa fitina na wanachama wake wasajili chama kinachoeleweka
huu utakuwa mwanzo mzuri.
ila katiba kwanza la sivyo tutaatamia mayai ya mbuni

Mchango wangu ni wako sinto changia tena hii thread; maana umemaliza kazi yote.
 
- Unasema solution yangu kama ya Ralwings ya kuwaondoa viongozi wote wa zamani ilikuwa ni ya kitoto, sasa unasema unaweza linganisha sisi na Ghana? Ulimsikia Obama alisema nini alipokuwa bungeni Ghana, alisema hana muda wa kutembelea nchi za Africa ambazo hazina utawaal unaoheshimu sheria, nimesema solution ni kuondoa vyama vyote vya siasa nchini na kuanza upya na kutowaruhusu viongozi wote wa sasa kurudi tena, kama ni umauzi wa kitoto basi umeisaidia sana Ghana, ndio maana tunauhitaji kuliko wako wa kiutuuzima!

- Ya kuogopa baki nayo toka lini nimewahi kuogopa mtu? Vipi mkuu are you ok! mimi ninaogopa are you kidding me or what? Jadili taifa mkuuu achana na mimi siwezi kukusaidia anything maana mimi sio kiongozi ni mwananchi tu kama wewe mwenye haki ya kutoa moni yangu on anything! na anywhere!

Willie @ NYC, USA.

- Nimesema the best solution na kufuta vyama vyote vya siasa na kuanza upya!

Willie @ NYC, USA.
WJM una hakika na unachosema? Ni chama au serikali unayotaka iondolewe, kwa ufahamu wangu chama ni hawa makada wa kisiasa na serikali ni watendaji ambao kikatiba hawatakiwi kuwa makada wa chama na hawa ndio wanaoandaa bajeti na kubuni vyanzo vya kodi, hawa pia tuwaondoe? Tutabakisha kina nani? kwani hata vijana miongoni mwao ni wewe na tawi lako la NYC hamtoingia ktk hiyo serikali ya kufikirika na hata haya mawazo unayoyatoa sasa hivi ni ktk hayo yanayoikwaza hii nchi, kwani tunakuhesabu umo ndani ya system i.e. umeandaliwa(kama sikukosea).
 
- Nimesema the best solution na kufuta vyama vyote vya siasa na kuanza upya!

Willie @ NYC, USA.

You are still bluffing!!
Kufuta vyama vyote vya siasa na ongezeko la ukusanyaji kodi, bado unalalamika mkubwa!!!

Haya ebu weka mkakati wako hapa ili wewe, wale na mimi kama taifa tuweza kuufanyia kazi!!
Elezea ukishafuta vyama vyote, what next??

Tukifuta vyama vyote, ina maana wanachama wa sasa hawatoruhusiwa kuwa wanachama wa vyama vitakavyoundwa?!?!

Mkuu unavyotaka kutueleza ni kua mfumo wa sasa wa vyama siasa ndio chanzo cha makusanyo madogo ya kodi??

- Sawa sawa kwa sababu wakwepa kodi wengi ni wachangiaji wa hivi vyama vya siasa na ni vyote, ndio maana dawa ni kufuta na kuanza upya, waliomo sasa wote wakae pembeni!, kama Stern anavyowaambia wachezaji wa NBA kwamba wakijifanya wanajua sana anawesza kuwaondoa wote na NBA ikaanza upya bila wao!

Willie @ NYC, USA.
 
@Wabunge wengi wa ccm ambao wamepata fursa ya kuongea bungeni wamekuwa wanasema "bajeti hii imejaa matumaini, ni bajeti inayomajali mtanzania na itakayomkomboa mtanzania!". Mbunge yoyote anayeikosoa anaonekana kama hana uzalendo! In other words hii imefikia hapa kwa makusudi mazima ya viongozi wetu. sitaki kundika zaidi nataka niwekeze 2015. We have to clean the house.
 
- Maneno mazito sana!

Es!
 
Bajeti imejaa matumaini kwa wao waheshimiwa wabunge na si kwa watanzania; tutawezaje kuisafisha nyumba huku chaguzi zetu zimetawaliwa na RUSHWA? 2015 hadithi itakuwa ilie ile kama mianya iliyopo haitazibwa.

Chama
Gongo la Mboto DSM
 
FROM: Facebook: by William Malecela on Sunday, June 19, 2011 at 8:19am

@ NEW YORK: Hatimaye nimepata nafasi ya kuisoma bajeti nzima ya serikali kwa mwaka 2011/2012, na kwa kweli ninasikitishwa sana na uwezo mdogo sana wa uwajibikaji wa serikali yetu ambao chanzo chake ni uwezo mdogo sana wa uongozi walionao viongozi wetu. I mean hakuna uwajibikaji kwa viongozi wetu na vitengo vya dola ni hafifu sana na in some cases ni zero kabisa, yaani hakuna kabisaa. I mean leo Tanzania kipato cha serikali yaani taifa, 70% inategemea kodi kutoka kwa mashirika 15 tu yaliyopo nchini, meaning kwamba the rest of 30% ndio inatoka kwetu wananchi, no wonder hili taifa tunapigizana makelele tu maendeleo hamna, I mean taifa litaendelea vipi na ukusanyaji hafifu wa kodi kama huu? Malipo mengi ya watumishi wa serikali hayakatwi kodi, WHY? ni kwa sababu hili taifa tumejiaminisha siku nyingi sana kwamba we are poor na hatuwezi kujiondoa kwenye umasikini, tumeiamini serikali kutuondolea umasikini, serikali ambayo inaongozwa na sisi wenyewe ambao tulishakubali siku nyingi sana kwamba ni masikini tu ndivyo tulivyoumbwa, matokeo yake imekuwa ni National Insanity circling yaani kurudia njia zile zile kila siku kwa kutegemea matokeo tofauti.

- Miaka 50 ya Uhuru, mpaka leo bado tuna-ptoject bajeti ya taifa ambayo haifanani na kipato chetu cha taifa, tunategemea kutumia Shillingi Trillion 11, lakini uwezo wetu kitaifa ni kipato cha Shillingi Trillion 7 tu, hatuna jawabu la tutapata wapi hiyo gap ya Trillion 5, ingawa tumeruhusu kampuni kama ya Zaintel kutuchezea akili kwa kuuzwa kwa ujanja ujanja kwa Celtel and then to Airtel in the process taifa tumepoteza kodi ya karibu USD $ 312 Million, tumeruhusu Hotel ya Movenpick iliyoanza kama Sheraton, kutuchezea akili wee na kodi in the process tunapoteza kila mwaka kodi karibu USD $ 300 Million, kule kwenye madini ndiko usiseme tunapoteza karibu USD $ 800 Million kila mwaka and the list goes on and on! Sasa kwa sababu tumezoea kutafuta majibu rahisi kwa maswali magumu, tumewakalia koo Wabunge kwamba ndio wachawi wetu kwa sababu ya posho zao!

- Wabunge wanaolipwa jumla ya Shillingi Million 7 kwa mwezi, 2 zikiwa ni mishahara yao ya mwezi na Tano zikiwa ni gharama zao za usafiri na wafanyakazi wao ambao ni lazima wawe nao kwa ajili ya kuwakilisha majimbo yao ipasavyo kwenye taifa. Sasa tunalilia mbunge asilipwe tena posho ya Shillingi Elfu 70 kwa siku anapokuwa bungeni au kwenye vikao vya kibunge, tunataka atumie hela za msahahara wake, yaani ule wa Shillingi Millioni 2. Mbunge akae bungeni ashiriki vikao 73 vya bajeti, akilipia shillingi Elfu 50 kwa siku kwa malazi tu, vikao 73 ni sawa na miezi miwili, sasa jumlisha utapata Mshahara wa Shillingi Millioni 4 na gharama ya malazi tu kwa kipindi kizima cha bajeti ni karibu nusu ya hizo hela zake za ujira, na tunaambiwa kwamba hii ndio inaweza kutusaidia taifa kuokoa hela nyingi sana za kuweza kuliendeleza hili taifa!, hebu angalia hela tunazopoteza kwenye kodi ya madini kila mwaka ni karibu mara 10 ya posho ya wabunge inayoliliwa sana kwamba ndio tatizo letu la taifa!

- Ni kama taifa la wendawazimu flani hivi, maana hata huwezi kusema ni walevi kwa sababu mlevi akiamka asubuhi huwa anakuwa mzima na productive tena, sisi taifa tupo pale pale tunazunguka tu kama taili la gari, na wale wasomi wetu ndio bure kabisaa, mijina mikubwa lakini hakuna faida yoyote kwa taifa. Bunge limejaa ma-Doctor, Wanasheria, Wahandisi, mpaka Wachumi, lakini mpaka leo umeme hakuna, ujanja ujanja tu na ujinga ujinga na kutafuta majibu rahisi rahisi ndio vimetutawala hili taifa!

IT IS ABOUT TIME SASA TUKAFUTA VYAMA VYOTE VYA SIASA HILI TAIFA, TUANZE UPYA!

MUNGU AIBARIKI TANZANIA!

William Malecela @ New York City; USA.

Mimi si mchumi na wala si mtaalam wa kodi ila naomba unifafanulie kitaalam yafuatayo:

1. Celtell kuwa Zein na then kuwa Airtel wamevunja sheria gani? na unaposema wametulia pesa kwa kutolipa kodi je unaweza kutufafanulia ni kodi ipi na kama kuna ukweli ina maana KITILYA wa TRA, watu wa TIC na wengine wanahusika viupi kwenye huu ukwepaji kodi?

2. Pia ninaomba unifafanulie sheraton wametuchezea akili vipi kwenye kubadili jina na kuwa Movenpick? Je wamevunja sheria gani ya Tanzania kubadili jina? na je wamevunja sheria ipi ya kodi in the process? Je unatuambia kuwa PCCB na idara husika za serikali hazina habari au vipi?
 
- POWERFULL, mkuu ubarikiwe sana maana haya yako ndio mawazo tunayohitaji hili taifa, safi sana!

Willie @ NYC, USA.

- Sawa sawa kwa sababu wakwepa kodi wengi ni wachangiaji wa hivi vyama vya siasa na ni vyote, ndio maana dawa ni kufuta na kuanza upya, waliomo sasa wote wakae pembeni!, kama Stern anavyowaambia wachezaji wa NBA kwamba wakijifanya wanajua sana anawesza kuwaondoa wote na NBA ikaanza upya bila wao!

Willie @ NYC, USA.

Sasa naanza kuelewa....kumbe unataka CCM na serikali ya CCM ifutwe!!!

Kwa uzoefu tu mkubwa, hao wakwepa kodi ndio wachangiaje wakubwa wa CCM. Mkwepa kodi hata siku moja hawezi kuchangia chama kingine zaidi ya CCM. Na hii imeshajidhihirisha mara nyingi pale mfanyabiashara anapochangia chama kingine, basi TRA na TISS watamsulubisha huyo mfanyabiashara kwa lundo la kodi ambazo watamwambia anadaiwa. Na hili lilitokea Mwanza,ambapo marehemu Majige (alikua mfanyabiashara mkubwa) aliichangia CUF mwaka 1995 katika uchaguzi wa jimbo la Sumve (kwa Ndassa); baada ya uchaguzi na Ndassa kushinda, TRA walimzonga msukuma wa watu mpaka akaja kufa kwa presha.

Hivyo unavyosema vyama vyote vifutwe kwa madai vinachangiwa na wakwepaji kodi, hauko sahihi.

Ndio maana argument yako ya kufuta vyama vyote vya siasa na kuanza upya, still it sounds like baloney!
 
Aidha unadharau sana watanzania/wananchi ambao mimi naona wanaonewa sana,au huelewi politicaleconomics za tanzania i.e a bit shallow or deeply misinformed.
Hayo mashirika kumi na tano yanayolipa kodi,hebu jaribu kufafanua yanalipaje hizo kodi?Asilimia ngapi ya bei ya bia,sigara kwa mfano ni kodi ambayo mwananchi huwa analipa indirectly?....mafuta?
usiseme naenda nje yatopic, just answer this please?
Kwanza kabisa nikuombe msamaha kwa ku-quote post yako,I meant to quote post ya mleta mada ambaye personally namuona yuko very misinformed.Nakubaliana na wewe kuhusu law enforcement,due to low wges nadhani na wananchi wengi kurely on a parallel(informal) sector.
Ila mkuu anaposema wananchi hawalipi kodi,ni mashirika kumi na tano tu ndiyo yanayolipa kodi,huo ni udanganyifu kwani hizo kodi ambazo mashirika yanalipa kwa serikali huwa ni mzigo kwa wananchi through pricing.......kwani hiyo hatujui nayo?
 
Sasa naanza kuelewa....kumbe unataka CCM na serikali ya CCM ifutwe!!!

Kwa uzoefu tu mkubwa, hao wakwepa kodi ndio wachangiaje wakubwa wa CCM. Mkwepa kodi hata siku moja hawezi kuchangia chama kingine zaidi ya CCM. Na hii imeshajidhihirisha mara nyingi pale mfanyabiashara anapochangia chama kingine, basi TRA na TISS watamsulubisha huyo mfanyabiashara kwa lundo la kodi ambazo watamwambia anadaiwa. Na hili lilitokea Mwanza,ambapo marehemu Majige (alikua mfanyabiashara mkubwa) aliichangia CUF mwaka 1995 katika uchaguzi wa jimbo la Sumve (kwa Ndassa); baada ya uchaguzi na Ndassa kushinda, TRA walimzonga msukuma wa watu mpaka akaja kufa kwa presha.

Hivyo unavyosema vyama vyote vifutwe kwa madai vinachangiwa na wakwepaji kodi, hauko sahihi.

Ndio maana argument yako ya kufuta vyama vyote vya siasa na kuanza upya, still it sounds like baloney!

- Well na huyu aliyewapa Chadema, Millioni 100 vipi naye TRA wamemfuata au bado? Mkuu unachohitaji ni kuweka maoni yako bila kulazimisha yangu yawe kama unavyotaka wewe, ninasema hivi ninazo info za kutosha sana kujua kwamba wakwepa kodi wanachangia vyama vyote vya siasa, kwa nini unashiriki mada ambayo ni baloney? ha1 ha! na wewe sio Baloney?

- Mkuu ninasema hivi vyama vyote vya siasa vina matatizo, hakuna nayeona kwamba kutokusanywa kodi ni tatizo, hakuna taifa linaweza kuendelea bila kukusanya kodi!

Willie @ NYC, USA.
 
- Sawa sawa kwa sababu wakwepa kodi wengi ni wachangiaji wa hivi vyama vya siasa na ni vyote, ndio maana dawa ni kufuta na kuanza upya, waliomo sasa wote wakae pembeni!, kama Stern anavyowaambia wachezaji wa NBA kwamba wakijifanya wanajua sana anawesza kuwaondoa wote na NBA ikaanza upya bila wao!

Willie @ NYC, USA.
Kuuliza si ujinga.Ningependa kujua USA unasoma au unafanya kazi
 
Mimi si mchumi na wala si mtaalam wa kodi ila naomba unifafanulie kitaalam yafuatayo:

1. Celtell kuwa Zein na then kuwa Airtel wamevunja sheria gani? na unaposema wametulia pesa kwa kutolipa kodi je unaweza kutufafanulia ni kodi ipi na kama kuna ukweli ina maana KITILYA wa TRA, watu wa TIC na wengine wanahusika viupi kwenye huu ukwepaji kodi?

2. Pia ninaomba unifafanulie sheraton wametuchezea akili vipi kwenye kubadili jina na kuwa Movenpick? Je wamevunja sheria gani ya Tanzania kubadili jina? na je wamevunja sheria ipi ya kodi in the process? Je unatuambia kuwa PCCB na idara husika za serikali hazina habari au vipi?

- Yaaani kweli mkuu unataka mimi nifungue hii mada halafu tena nikufanyie yote hayo na wewe utafanya nini kulisaidia taifa lako mkuu mbona tumezoea sana kufanyiwa kila kitu, yaani wewe mkuu huwezi kujituma hata kidogo? ukatafuta hizo info?

Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu pamoja na kuwa una hoja ktk baadhi ya sehemu, lakini naona lengo lako kubwa ni kupambana na wapinga posho!! Sababu hata unavyoisemea posho ni kama watu wanapinga wabunge tu kuichukua, adhari za posho zimeelezwa sana lakini unaonyesha kuzifumbia macho kama vile hazipo, mkuu shibe ya hao wabunge ni sababu mojawapo inayawafanya wafumbie macho uozo ktk taasisi mbalimbali. Nitakupa mfano mmoja, Chenge alikuwa anapokea posho zote wakati aliposhiriki kuliibia taifa...! Na hii lugha yako ya kufuta vyama vyote ndiyo lugha ya ccm!! Kumbuka wakiwatisha wananchi kuwa wakichagua wapinzani amani itatoweka!! Kwa ccm ni wao au wakose wote... Lugha hii watanganyika wengi tumeishtukia...
 
Back
Top Bottom