Bajeti 2011: Tanzania tunahitaji kufuta vyama vyote vya siasa tuanze upya!!

Mkuu pamoja na kuwa una hoja ktk baadhi ya sehemu, lakini naona lengo lako kubwa ni kupambana na wapinga posho!! Sababu hata unavyoisemea posho ni kama watu wanapinga wabunge tu kuichukua, adhari za posho zimeelezwa sana lakini unaonyesha kuzifumbia macho kama vile hazipo, mkuu shibe ya hao wabunge ni sababu mojawapo inayawafanya wafumbie macho uozo ktk taasisi mbalimbali. Nitakupa mfano mmoja, Chenge alikuwa anapokea posho zote wakati aliposhiriki kuliibia taifa...! Na hii lugha yako ya kufuta vyama vyote ndiyo lugha ya ccm!! Kumbuka wakiwatisha wananchi kuwa wakichagua wapinzani amani itatoweka!! Kwa ccm ni wao au wakose wote... Lugha hii watanganyika wengi tumeishtukia...

- Haya ni maoni yako na ni haki yako kuwa nayo, mimi nimesema yangu sasa ni Taifa kwanza sio mimi, mimi sio kiongozi! na wala sigombei anything!

Willie @ NYC, USA.
 
- Well na huyu aliyewapa Chadema, Millioni 100 vipi naye TRA wamemfuata au bado? Mkuu unachohitaji ni kuweka maoni yako bila kulazimisha yangu yawe kama unavyotaka wewe, ninasema hivi ninazo info za kutosha sana kujua kwamba wakwepa kodi wanachangia vyama vyote vya siasa, kwa nini unashiriki mada ambayo ni baloney? ha1 ha! na wewe sio Baloney?

-
Mkuu ninasema hivi vyama vyote vya siasa vina matatizo, hakuna anayeona kwamba kutokusanywa kodi ni tatizo, hakuna taifa linaweza kuendelea bila kukusanya kodi!

Willie @ NYC, USA.

Kwanza, siwezi kukulazimisha maoni yangu yawe yako...wewe kama mtu mzima, basi utakua na tatizo kama unaweza kulazimishwa na mtu mwingine maoni yake yawe yako.

Pili, kama unazo hizo info, share with us ili tuwajue na tuweze kuchukua hatua kama vijana katika taifa letu. Hautakua mzalendo kama unaficha taarifa za watu wanaohujumu uchumi. Wewe ndiwe uliesema tatizo ni kwamba kodi hazikusanywi za kutosha, sasa kwa kukulia taarifa za juu ya ukwepaji wa kodi, unasaidia au unabomoa taifa?!?

Tatu, so far katika arguments zako sijaona ubaya wa vyama vingine zaidi ya kuona ubaya wa CCM! Unapoongelea ukusanyaji wa kodi, ilo ni jukumu la serikali iliyo madarakani! Unapoongelea namna ya kudeal na wakwepaji kodi, ili nalo ni jukumu la serikali iliyopo madarakani. Sasa, hiyo si ni serikali ya CCM!?!?

Mwisho, nakubaliana na wewe kabisa hakuna nchi inayoendelea bila kuwa na makusanyo makubwa ya kodi. Mwalimu alisemahivyo na mimi ninaamini hivyo. Jambo la nyongeza, CHADEMA hiki ndio kimekuwa kilio chao kwa muda mrefu: masuala ya kuondoa misahama ya kodi hususani kwenye makampuni ya madini; misahama ya kodi hisizidi asilimia 1 ya pato la taifa (sasa ipo asilimia 4!!) n.k. Haya ni mawazo ya serikali kivuli.
 
- Sikuyaona hayo, nimeona wakitaka kuongezeka kwa bajeti Shillingi Billion 450, ambazo hawasemi ziatatoka wapi sikuona mahali popote pakisemwa kwamba tuna tatizo la ukusanyaji kodi na ndio hoja yangu ya msingi, ni kwamba Tanzania hatukusanyi kodi inavyotakiwa ni tatizo la CCM na vyama vyote vya siasa nchini.

Willie @ NYC, USA.
 
Sijaelewa unataka nini hapa kwa kunilazimisha kuwa nawadharau Watanzania. Nadhani unahitaji kurudi nyuma na kusoma posts zangu upya na upoint specifically wapi nadharau Tanzania. Nimezungumzia weak/poor institutions na ukweli zinaexists. Angalia takwimu za watoa rushwa zinatoka wapi kama si taasisi nilizotaja. Ningependa tujadili hizo politicaleconomics za Tz unazodai niko mis-informed.
Kwa kifupi kelele hizi zote zinasababishwa na taasisi zetu. Labda nikuonyeshe inakuwaje. Mtu anakwepa kodi. Polisi wanapewa taarifa ya siri kuna watu badala ya kusafirisha mafuta kwenda nje wanauza ndani ya nchi au wanachanganya na mafuta ya taa. Wanakwenda pale wanatulizwa na rushwa au kimemo. Wakijitahidi kufika mahakamani, watu wanafanya timing kwenye case inaunguruma for years. Mahakama ikijitahidi kuwa makini, TRA wanabipiwa kule waje na estimate ndogo ya kodi, watapewa cha juu baadae. Unaona tatizo hapo? Hapa nazungumzia mfumo wa kitaasisi ulivyo na mapungufu.
Samahani i meant to quote mtoa mada!
 
- Sikuyaona hayo, nimeona wakitaka kuongezeka kwa bajeti Shillingi Billion 450, ambazo hawasemi ziatatoka wapi sikuona mahali popote pakisemwa kwamba tuna tatizo la ukusanyaji kodi na ndio hoja yangu ya msingi, ni kwamba Tanzania hatukusanyi kodi inavyotakiwa ni tatizo la CCM na vyama vyote vya siasa nchini.

Willie @ NYC, USA.
Mimi ni CCm damu,ila nimeona sehemu ambayo wamezungumzia misamaha ya kodi as a %age of GDP.Kuhusu kuuwa vyama vyote vya siasa,sioni umuhimu kwani watu ni walewale na wana uhuru wa kuhama na kuanzisha vyama vingine.
Sioni tofauti ya ghana na Tanzania kiuchumi,sijui unatumia data gani,ila from world bank.....wote tuko category sawa tu,hata mining act yetu ilikuwa replica ya mining act yao.....we are all sailing on the same dhow!....I don't know whats the big deal.
 
Mkuu William Toka New York!
Nimekugongea thanks kubwa kwa sababu leo umeweka unazi wa siasa za Bongo pembeni umeandika kile kinacholitafuna taifa. Kwa hakika hakuna taifa linaendelea kama linafanya mchezo katika matumizi mazuri ya rasilimali watu, ukusanyaji wa kodi katika nyanja zote, na utengenezaji wa mazingira ya kuzalisha chakula cha kutosha kwa watu wake. Leo kuna watanzania wengi tu bila idadi hawana uhakika wa mlo wa ugali na mchicha achilie mbali mlo kamili. Watu wengi na wengine wanashinda Jamvini kutoa maoni wanaishi kwa rushwa ya kuanzia sh 500 na kuendelea ili wapeleke dagaa nyumbani, serikali yetu hasa watawala wameamua kuuza nchi kwa dengu kidogo za kusukuma siku kama sio kununua gari na nyumba ya kuishi na kuhakikisha wana kianzio baa eti hao wanaitwa matajiri hapa kwetu. hii ni aibu kubwa. Taifa hili linahitaji mtu mwenye kichaa kidogo ili afanye unusual and unexpected decisions katika mfumo mzima wa uendeshaji wa taifa kama tunataka kujikwamua kutoka tulipo.
 
- Sikuyaona hayo, nimeona wakitaka kuongezeka kwa bajeti Shillingi Billion 450, ambazo hawasemi ziatatoka wapi sikuona mahali popote pakisemwa kwamba tuna tatizo la ukusanyaji kodi na ndio hoja yangu ya msingi, ni kwamba Tanzania hatukusanyi kodi inavyotakiwa ni tatizo la CCM na vyama vyote vya siasa nchini.

Willie @ NYC, USA.

Nyekundu: mkuu naona unataka ligi...masuala ya kupunguza misamaha ya kodi na kufanya misamaha ya kodi hisizidi asilimia 1 ya pato la taifa, mbona yamekua agenda kuu ya CHADEMA kwa muda. Hata wakati akiwalisha bajeti ya serikali kivuli, ndugu Zitto alisema haya ninayokwambia!!!

Kijani: bado hujanishawishi kua ilo ni tatizo la vyama vyote; so far umeargue kua wakwepaji kodi ndio wachangiaji wakuu wa vyama. Je, nani mwenye jukumu la kuhakikisha wakwepaji kodi wanalipa kodi na kuwajibishwa?!?!
 
- The big question hapa ni kwa nini hili taifa hatulipi kodi? Kwa nini hatupendi kukusanya kodi? bila kulipa kodi hili taifa tutaendelea kupigizana kelele mpaka mwisho wa Dunia na hakuna lolote la maana litakalofanyika, hata Mwalimu alilisema sana hili mwishoni mwa maisha yake kwamba taifa lisilo kusanya kodi haliwezi kwenda popote kimaendeleo!

Willie @ NYC, USA.
Maswali yako ni mazuri nimeyapenda, lakini nakushauri kwa nia njema utakapo anzisha tawi la CCM hapo New York city kazi ya kwanza iwe kuuliza na kujibu maswali hayo mwanana. Tangu lini serikali iliyoundwa na chama kinacho kumbatia rushwa na ufisadi ikawa na uwezo wa kukusanya kodi? Nioneshe mbunge mmoja tu wa CCM aliepita ndani ya chama na hatimaye jimboni kwake bila kutoa rushwa au kutembeza kanga na fulana ya kijani! Sasa kwanini unatupotezea muda kujadili vitu vilivyo wazi? Mawazo haya wapelekee akina Nape na Mukama na sio sisi. Kwanza wewe unauwezo wa kuongea na rais moja kwa moja, basi muulize maswali hayo.
 
Not necessarily....angalia hizi data.

Government revenue as a percentage of GDP

Quatar 2.2%
Kuwait 1.5%
UAE 1.4%
Tanzania 12%
Zimbabwe 49%
 
Nyekundu: mkuu naona unataka ligi...masuala ya kupunguza misamaha ya kodi na kufanya misamaha ya kodi hisizidi asilimia 1 ya pato la taifa, mbona yamekua agenda kuu ya CHADEMA kwa muda. Hata wakati akiwalisha bajeti ya serikali kivuli, ndugu Zitto alisema haya ninayokwambia!!!

Kijani: bado hujanishawishi kua ilo ni tatizo la vyama vyote; so far umeargue kua wakwepaji kodi ndio wachangiaji wakuu wa vyama. Je, nani mwenye jukumu la kuhakikisha wakwepaji kodi wanalipa kodi na kuwajibishwa?!?!

- Lakini unakumbuka majuzi Mwenyekiti wa Chadema aslipokubali kwamba mshahar wa Dr. Slaa haulipiwi kodi au umesahau na wao ndio wenye agenda ya kodi unasema au?

Willie @ NYC, USA.
 
Maswali yako ni mazuri nimeyapenda, lakini nakushauri kwa nia njema utakapo anzisha tawi la CCM hapo New York city kazi ya kwanza iwe kuuliza na kujibu maswali hayo mwanana. Tangu lini serikali iliyoundwa na chama kinacho kumbatia rushwa na ufisadi ikawa na uwezo wa kukusanya kodi? Nioneshe mbunge mmoja tu wa CCM aliepita ndani ya chama na hatimaye jimboni kwake bila kutoa rushwa au kutembeza kanga na fulana ya kijani! Sasa kwanini unatupotezea muda kujadili vitu vilivyo wazi? Mawazo haya wapelekee akina Nape na Mukama na sio sisi. Kwanza wewe unauwezo wa kuongea na rais moja kwa moja, basi muulize maswali hayo.

- Hukulazimishwa mkuu kujadili hoja, mimi najadili taifa naona unaijadili CCM, kwa nini usianziseh mada ya CCM na kodi, mimi yangu ni ya kufuta vyama vyote nchini!

Willie @ NYC, USA.
 
Mkuu William Toka New York!
Nimekugongea thanks kubwa kwa sababu leo umeweka unazi wa siasa za Bongo pembeni umeandika kile kinacholitafuna taifa.
Kwa hakika hakuna taifa linaendelea kama linafanya mchezo katika matumizi mazuri ya rasilimali watu, ukusanyaji wa kodi katika nyanja zote, na utengenezaji wa mazingira ya kuzalisha chakula cha kutosha kwa watu wake. Leo kuna watanzania wengi tu bila idadi hawana uhakika wa mlo wa ugali na mchicha achilie mbali mlo kamili. Watu wengi na wengine wanashinda Jamvini kutoa maoni wanaishi kwa rushwa ya kuanzia sh 500 na kuendelea ili wapeleke dagaa nyumbani, serikali yetu hasa watawala wameamua kuuza nchi kwa dengu kidogo za kusukuma siku kama sio kununua gari na nyumba ya kuishi na kuhakikisha wana kianzio baa eti hao wanaitwa matajiri hapa kwetu. hii ni aibu kubwa. Taifa hili linahitaji mtu mwenye kichaa kidogo ili afanye unusual and unexpected decisions katika mfumo mzima wa uendeshaji wa taifa kama tunataka kujikwamua kutoka tulipo.

- Sawa sawa mkuu hapo tupo wote!

Willie @ NYC, USA.
 
- The big question hapa ni kwa nini hili taifa hatulipi kodi? Kwa nini hatupendi kukusanya kodi? bila kulipa kodi hili taifa tutaendelea kupigizana kelele mpaka mwisho wa Dunia na hakuna lolote la maana litakalofanyika, hata Mwalimu alilisema sana hili mwishoni mwa maisha yake kwamba taifa lisilo kusanya kodi haliwezi kwenda popote kimaendeleo!

Willie @ NYC, USA.

Mkuu una soft copy ya bajeti nzima unipe link?
 
Mimi si mchumi na wala si mtaalam wa kodi ila naomba unifafanulie kitaalam yafuatayo:

1. Celtell kuwa Zein na then kuwa Airtel wamevunja sheria gani? na unaposema wametulia pesa kwa kutolipa kodi je unaweza kutufafanulia ni kodi ipi na kama kuna ukweli ina maana KITILYA wa TRA, watu wa TIC na wengine wanahusika viupi kwenye huu ukwepaji kodi?

2. Pia ninaomba unifafanulie sheraton wametuchezea akili vipi kwenye kubadili jina na kuwa Movenpick? Je wamevunja sheria gani ya Tanzania kubadili jina? na je wamevunja sheria ipi ya kodi in the process? Je unatuambia kuwa PCCB na idara husika za serikali hazina habari au vipi?

You cant be serious

hivi kwa akili zako unakaa kwenye computer na kuuliza maswali haya JF?

halafu unategemea majibu?

you must be living in planet Zog

kukaa kote humu huja jua style ya discussion humu?

maswali kama hayo hutojibiwa kwani unawaondoa watu kwenye mteremko waliozowea

you must be one delusional poster ambaye bado kalala
 
- Hapana hakuna anayemlipa mwingine humu kumfanyia utafiti wa ishus, unapewa mwanzo na wewe uende ujishugulishe ili uje useme your finding, lakini kuja hapa unafoka utafutiwe kila kitu na wengine na taifa ni lako mwenyewe ni a little too much, na wewe fanya utafiti basi japo kidogo uje useme your findings!

Willie @ NYC, USA.
 
- Ukienda google utaikuta original ya serikali kabisaa, wala haina taabu wewe bonyeza google kule!

Wiilie @ NYC, USA.

Mkuu simaanishi ile hotuba ya Waziri aliyoisoma bungeni. I mean bajeti yenyewe. The real thing. Namesikia iko kwenye vi booklets vinne hivi kama sijakosea. That's is the one I am looking for Mkuu.
 
- Unasema solution yangu kama ya Ralwings ya kuwaondoa viongozi wote wa zamani ilikuwa ni ya kitoto, sasa unasema unaweza linganisha sisi na Ghana? Ulimsikia Obama alisema nini alipokuwa bungeni Ghana, alisema hana muda wa kutembelea nchi za Africa ambazo hazina utawaal unaoheshimu sheria, nimesema solution ni kuondoa vyama vyote vya siasa nchini na kuanza upya na kutowaruhusu viongozi wote wa sasa kurudi tena, kama ni umauzi wa kitoto basi umeisaidia sana Ghana, ndio maana tunauhitaji kuliko wako wa kiutuuzima!

- Ya kuogopa baki nayo toka lini nimewahi kuogopa mtu? Vipi mkuu are you ok! mimi ninaogopa are you kidding me or what? Jadili taifa mkuuu achana na mimi siwezi kukusaidia anything maana mimi sio kiongozi ni mwananchi tu kama wewe mwenye haki ya kutoa moni yangu on anything! na anywhere!

Willie @ NYC, USA.

Willie,
Ujue kuwa Rawlings aliweza kufanya aliyofanya kule Ghana kwa sababu alipindua nchi tena alikwenda hata against wakubwa wake jeshini ambao walikuwa pia wamenogewa na ulaji kama walivyokuwa politicians. The fact kwamba Rawlings aliweza tena mara mbili ilikuwa ni combination ya luck, na timing ya hali ya juu sana. Ili kufanya unalopendekeza la kufuta vyama vyote ni lazima atakayetoa mwongozo awe nje ya vyama vyote - in other words, jeshi tu ndiyo linaweza kufanya hivyo. Is that what you are suggesting? Na kama ni hivyo, tuambie straight basi.
 
- Lakini unakumbuka majuzi Mwenyekiti wa Chadema aslipokubali kwamba mshahar wa Dr. Slaa haulipiwi kodi au umesahau na wao ndio wenye agenda ya kodi unasema au?

Willie @ NYC, USA.

Yes ni kweli alisema hayo lakini unategemea huyo Dr. Slaa apeleke kodi kule TRA au ni wajibu wa TRA chini ya sheria zilizowekwa na uongozi uliopo kumwendea Dr. Slaa na kudai hiyo kodi. Mimi sielewi kuna uhusiano gani kati ya weak collection ya kodi na vyama vya upinzani at this point. Kama wale wanaotakiwa wai-collect hiyo kodi hawafanyi hivyo si wajibu wa serikali iliyopo kuchukua hatua? Kimsingi najiunga na wengi hapa kukubaliana na hoja kuwa kodi hazikusanywi inavyopasa lakini wewe unaelekea kutaka vyama vyote vichukue lawama - hiyo inatoa impression kwamba unaogopa kukilaumu CCM. Najua unasema huogopi mtu Willy na pengine ni kweli, lakini unavyong'ang'ania kuvilaumu vyama vingine vya siasa kwenye issue kama hii unatufanya hata wengine tunaokuona jasiri kuwa na wasiwasi.
 
Back
Top Bottom