Bado natafakari kauli ya Malima kwamba zile silaha ni mtaji mkubwa wa maisha!

NdasheneMbandu

JF-Expert Member
Jan 2, 2012
940
308
Ndugu zangu,

Mimi bado najiuliza hivi Malima alikuwa anamaanisha nini aliposema kwamba silaha mbili zilizokoswakoswa kuibwa ni mtaji mkubwa wa maisha. Binafsi kwa kiongoozi mkubwa kama yeye naona kama hakupaswa kuongea hivyo. Kama ndivyo anavyoamini basi nchi hii tuna laana kubwa sana. Sisi wananchi tunawezaje kumtofautisha yeye na hao wanaotumia zana hizo kama mtaji. Inavyoonekana, aliyeiba ni changudoa wake maana tangu lini changudoa akahitaji silaha.

Nitafurahi wanaharakati wakifungua kesi dhidi ya Malima ili atueleze silaha hizo anazitumia kwa biashara gani.
 
Wanajamii habari ya Jumapili. Ninaamini ni wazima na mnaendelea vizuri. Nimesoma gazeti la mwananchi la leo kwenye kichwa cha habari kinachoeleza kuibiwa kwa naibu huyu wa waziri naomba kunukuu sehemu hii

Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni. Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh milioni moja, simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry yenye thamani ya Sh5.5 milioni,” alisema kamanda huyo na kuongeza:

“Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, fedha taslimu Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.”

Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.

Hata hivyo, Kaimu Kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu ya wazi
.""

Jamani naomba kujua huyu kiongozi silaha zote hizi ni za nini? Je viongozi wanaruhusiwa kuwa na sila za kivita na kutembea nazo kokote? hivi vitu vyote alikuwa anataka kuhama mkoa au nchi?

Naomba kuwasilisha!
 
Ndugu zangu,

Mimi bado najiuliza hivi Malima alikuwa anamaanisha nini aliposema kwamba silaha mbili zilizokoswakoswa kuibwa ni mtaji mkubwa wa maisha. Binafsi kwa kiongoozi mkubwa kama yeye naona kama hakupaswa kuongea hivyo. Kama ndivyo anavyoamini basi nchi hii tuna laana kubwa sana. Sisi wananchi tunawezaje kumtofautisha yeye na hao wanaotumia zana hizo kama mtaji. Inavyoonekana, aliyeiba ni changudoa wake maana tangu lini changudoa akahitaji silaha.

Nitafurahi wanaharakati wakifungua kesi dhidi ya Malima ili atueleze silaha hizo anazitumia kwa biashara gani.

Mkuu kwa kweli ile kauli kutoka kwa kiongozi wa Kitaifa........ilinishangaza sana........
 
Amechanganyikiwa,kulizwa na demu si mchezo ndugu,yeye aliamini amempa penzi moto2 kumbe CD alikua kikazi zaidi.
 
Comrade kama wewe ambavyo hujapata majibu ktk hiyo tafakuri yako jadidu nami pia nimegubikwa na maswali mengi sana.Nimesoma kwenye mwananchi kwamba siraha mojawapo ilikua SMG. nijuavyo SMG NI siraha ya kivita ambayo mtu binafsi haruhusiwi kuimiliki hapa Comrades naombeni ufafanuzi wenu.Ni vipi Bwn Adam amiliki siraha hii?
 
Kwanza anatembea na silaha zaidi ya moja, yeye ni nani?
Kwa kuwa kasema ni mtaji, hapana shaka ametupa mwanga wa nini anazifanyia silaha hizo
 
Ameibiwaje? silaha zilikuwa na shughuli gani sasa? si angetengua mtu kiuno!!!!! vuai kesha sema lolote? kamati ya ulinzi na usalama ishatoa msimamo wake juu ya mtu asoweza tunza silaha. nyaraka za serikali zilizoibwa mbona hazitaji!!!!!!!!
 
Huyu kaudanganya umma, kwani huenda alikuwa na nyaraka za serikali ambazo kuna wizi umefanyika. Ili kuua soo apitishie kwa kusema ameibiwa vitu vyake vyote. Kama serikali imekerwa na uongo huu, imfikishwe mahakamani ili aeleze kwa nini amiliki kizembe silaha ya kivita?
 
Mmmh yakweli haya? Alisema kweli silaha ni mtaji? Hivi nikweli alikua na smg!! Au watu wanampakazia? Hayajanielea haya!!
 
Mkuu Kelnmyg,
nilifikiri una maswali mengi sana, eg vinasa sauti vya nini, hiyo Blckberry ya TSh 5.5m/- mbona bei kubwa sana? etc? Anyway, mimi ni referee (Moderator) wenu, nawatakia mjadala mwema!
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Kwanza anatembea na silaha zaidi ya moja, yeye ni nani?
Kwa kuwa kasema ni mtaji, hapana shaka ametupa mwanga wa nini anazifanyia silaha hizo

Mkuu huyu jamaa alikuwa na madini yenye thamani kubwa..ndio maana inabidi atumie bunduki mbili kuyalinda!
mbaya zaidi yule malaya aliondoka na baadhi ya madini.
 
Hivi huyu jamaa ni mtu wa wapi? Laptop 3 za nn hajui flash disks au extenal hard disks?
Tatizo anaona watz wajinga wakat yy ndo mjinga
 
Anakuwa na madini kwenye mikoba yake ndo mana anatembea na SMG,usishangae badae ukaja kuambiwa alikuwa na grenade kwenye begi la nguo lililoibwa na kahaba
 
Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.

hapo kwenye red inamaana huyu mtu alikuwa nae chumbani,alivyo gundua mh.kaanza kukoroma,mwanadada kamtoka fastasta
 
Back
Top Bottom