kibananhukhu
JF-Expert Member
- Jul 6, 2009
- 366
- 161
Kuna Waziri wetu mwingine alishikwaga nje na Risasi za AK45. Hii yote Ni tabia ya viongozi wapagani waoga wasiojiamini na hawajui kabisa wamekuja duniani kufanya nini.
"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na , baraghashia mbili zenye thamani ya Sh 50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.
Kweli mkuu. Anajaribu kutunga story to kuficha ukweli. But kuna mambo mengi hayaeleweki, hajaipanga vizuri story yake.sasa hizo silaha zimemsaidia nini kama anaibiwa kiulaini namna hiyo?hata angekua na kifaru wangemchapa tuu
Kuna mkuu huko juu ameelezea kua zote unazoziona hapo juu ni bei za serikali,so usishtuke sana!Aisee hizi barghashia zimepanda lini bei?
Buchanan
Huyu ndugu ni muheshimiwa na ni mtu wa hotuba kwahiyo sitashangaa sana kama atasema vinasa sauti ni kwaajili ya kujinasa sauti yake mwenyewe ya hotoba ili baada ya kusikiliza na kurudiarudia mara kwa mara (ku-rehearse) huku akisahihisha, atoke na toleo la hotuba nzuri na yenye mvuto zaidi.
Lakini: haiingii akilini hata kama alikuwa anasafari kwenda nje ya nchi hicho kiasi cha hela kutembea nacho mfukoni kwa tekinolojia iliyopo sasa bado ni kikubwa, silaha ya kivita anakaa nayo hotelini kwa nini? anamlinda nani? anajilinda dhidi nini/nani? kwa nini? kama anahitaji ulinzi mkali kiasi hicho si angepewa bodyguard? wakati anaibiwa alikuwa wapi? kama ana maadui wengi kiasi hicho mbona basi alikuwa mbali na silaha yake ya kivita?
SMG ni silaha inayojulikana kama "assault automatic weapon" ambayo kwa sheria za Tanzania ni vyombo vya majeshi ya serikali tu vinavyoruhusiwa kumiliki. Mtu binafsi huruhusiwi kuwa na "assault weapon". Hivyo tunataka IGP na Waziri wa ndani atupe majibu kamili kama Malima alikuwa na silaha hii kihalali, na huo uhalalishaji wa kumilikishwa "assault weapon" ulitoka wapi.
Wanajamii habari ya Jumapili. Ninaamini ni wazima na mnaendelea vizuri. Nimesoma gazeti la mwananchi la leo kwenye kichwa cha habari kinachoeleza kuibiwa kwa naibu huyu wa waziri naomba kunukuu sehemu hii
"Vitu alivyoibiwa ni pamoja na laptop tatu, aina ya Dell zenye thamani ya Sh5.6 milioni. Vinasa sauti viwili vya digitali na headphone zake zote ambavyo thamani yake ni Sh milioni moja, simu tatu, ya kwanza Nokia C6 ya Sh500,000, Nokia E200 ya Sh250,000 na Blackberry yenye thamani ya Sh5.5 milioni, alisema kamanda huyo na kuongeza:
Vitu vingine ni pete mbili za almasi zenye thamani ya Sh2.5 milioni, Dola za Marekani 4,000 ambazo ni sawa na Sh6.5milioni, fedha taslimu Sh1.5 milioni, kadi mbili za benki, mabegi matatu ya nguo, baraghashia mbili zenye thamani ya Sh50,000 na nyaraka mbalimbali za Serikali.
Kaimu kamanda huyo alisema kuwa polisi waliokwenda kufanya uchunguzi wa awali walibaini kuwa mtu aliyeiba vitu hivyo hakuwa amevaa viatu kutokana na nyayo za miguu yake zilizoonekana nje ya chumba alichokuwa naibu waziri huyo.
Hata hivyo, Kaimu Kamanda huyo ambaye pia ni Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Morogoro, alisema mwizi aliyeiba vitu hivyo hakuiba bastola na bunduki aina ya SMG alizokuwa nazo Naibu Waziri huyo ambazo zilikuwa sehemu ya wazi.""
Jamani naomba kujua huyu kiongozi silaha zote hizi ni za nini? Je viongozi wanaruhusiwa kuwa na sila za kivita na kutembea nazo kokote? hivi vitu vyote alikuwa anataka kuhama mkoa au nchi?
Naomba kuwasilisha!
Mtaji wa kimaisha alikuwa anamaanisha ukiwa nazo unakodisha kwa wazee wa kazi unapata mkwanja
Mkuu huyu jamaa alikuwa na madini yenye thamani kubwa..ndio maana inabidi atumie bunduki mbili kuyalinda!
mbaya zaidi yule malaya aliondoka na baadhi ya madini.
Kumbe ulikuwa hujui...mh. alikuwa patner na papaaa Muzamir young milionaire, papaa Musofee, Ally Aurora biashara yao
kubwa ni madini mangumashi wakiwaliza wazungu kila wakati...nilifikiri amepata ubunge na uwaziri ameacha hizo deal, kumbe bado!!
Ndugu zangu,
Mimi bado najiuliza hivi Malima alikuwa anamaanisha nini aliposema kwamba silaha mbili zilizokoswakoswa kuibwa ni mtaji mkubwa wa maisha. Binafsi kwa kiongoozi mkubwa kama yeye naona kama hakupaswa kuongea hivyo. Kama ndivyo anavyoamini basi nchi hii tuna laana kubwa sana. Sisi wananchi tunawezaje kumtofautisha yeye na hao wanaotumia zana hizo kama mtaji. Inavyoonekana, aliyeiba ni changudoa wake maana tangu lini changudoa akahitaji silaha.
Nitafurahi wanaharakati wakifungua kesi dhidi ya Malima ili atueleze silaha hizo anazitumia kwa biashara gani.
Comrade kama wewe ambavyo hujapata majibu ktk hiyo tafakuri yako jadidu nami pia nimegubikwa na maswali mengi sana.Nimesoma kwenye mwananchi kwamba siraha mojawapo ilikua SMG. nijuavyo SMG NI siraha ya kivita ambayo mtu binafsi haruhusiwi kuimiliki hapa Comrades naombeni ufafanuzi wenu.Ni vipi Bwn Adam amiliki siraha hii?