Awamu ya tatu ya mgomo wa madaktari 23 June, 2012

Predictable as Rambo, with another clip
Snoop Dogg - Up Jump The Boogie
 
Hili ni zengwe jipya. jana tu yule ''mchumi wa daraja la kwanza na mtumishi aliyetukuka wa BOT'' alisema kwenye zile trilioni 10 za matumizi ya kawaida kuna hela za madaktari ili wasigome.

Huu ujumbe sijui kama kwenye CCM caucus wameupata.
Kama naona jinsi CCM watakavyoumbuka huko bungeni na kwenye hili swala hakuna cha ''muongozo wa spika'' au ''taarifa kwa spika''.

Ah Tanganyika yangu weeeeee. nchi haina mwenyewe, full fujo tuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu

FFU na nyie hamgomi hata kwa siku mbili tu??
 
Mwaka huu huyu kilaza asipo jiuzuru!
Madaktari migomo!
Wanafunzi migomo!
Walimu migomo!
Wafkz wa Reli soon!
TUCTA nawona walee!
Huyu kweli dhaifu hebu gomeni
bwana vasco apunguze safari kidogo.
 
Then watu wanakaa bungeni kuongea maneno ya khanga na ubishani wa kisiasa na kuacha mambo ya msingi kama haya. Sasa Mwigulu Nchemba yeye kama mjanja aje na hoja ya kuwatetea madaktari sio anajiita mchumi 1st class huku wananchi wakiteketea. Uchumi utakuwaje endapo wananchi watakuwa hawana afya njema kutokana na mgomo wa madaktari!!!
 
Yafuatayo ni madai ya madaktari na majibu yaliyotolewa na serikali.

Kupandisha mishahara,
Bajeti ni finyu, kuwaongezea madaktari mishahara kutaongeza migogoro ktk secta nyingine,

Bima ya kijani kwa watumishi wa afya
serikali itaendelea na mazungumzo na mifuko hii, ili kuona kama wataboresha.

Risk allowances
serikali itatoa chanjo ya homa ya Ini(Hepatitis B) tu, nayo watapewa kwa awamu kutokana na ufinyu wa bajeti
.

Hardship allowances
S
erikali inaboresha miundombinu katika sehemu zenye maisha magumu,

House allowances
serikali inajenga nyumba ktk halmashauri 70 za watumishi wa umma hata madaktari wakiwemo.Hata hivyo sio madaktari wote watapata.

Malipo ya kuitwa kazini usiku
S
erikali itaendelea kuliopa Tsh 25000 kwa daktari bingwa, 20000 kwa madaktari na Tsh 10000 kwa kada nyingine mpaka hapo bajeti itakaporuhusu.

Madaktari kukopeshwa magari
wafanyakazi wa serikali kuu wataanza mpango huo ktk bajeti ya 2011/2012.

Hapo kwenye red kumenistua. Madaktari wanakuwa very exposed na magonjwa ya kuambukiza kwa sababu ya mazingira wanayofanya kazi, lakini serikali bado kweli inajivuta. Inakuwaje serikali 'maskini' iwe na uwezo wa kununua magari yenye thamani ya Tshs 5 trillion?
 
Rais dhahifu mpaka wajanja wanautumia udhahifu wake kumwingiza mkenge kwa kumpa ushauri wa kimagumashi! Kweli cha Mjinga huliwa na mwerevu.
 
Yafuatayo ni madai ya madaktari na majibu yaliyotolewa na serikali.

Kupandisha mishahara,
Bajeti ni finyu, kuwaongezea madaktari mishahara kutaongeza migogoro ktk secta nyingine,

Bima ya kijani kwa watumishi wa afya
serikali itaendelea na mazungumzo na mifuko hii, ili kuona kama wataboresha.

Risk allowances
serikali itatoa chanjo ya homa ya Ini(Hepatitis B) tu, nayo watapewa kwa awamu kutokana na ufinyu wa bajeti.

Hardship allowances
S
erikali inaboresha miundombinu katika sehemu zenye maisha magumu,

House allowances
serikali inajenga nyumba ktk halmashauri 70 za watumishi wa umma hata madaktari wakiwemo.Hata hivyo sio madaktari wote watapata.

Malipo ya kuitwa kazini usiku
S
erikali itaendelea kuliopa Tsh 25000 kwa daktari bingwa, 20000 kwa madaktari na Tsh 10000 kwa kada nyingine mpaka hapo bajeti itakaporuhusu.

Madaktari kukopeshwa magari
wafanyakazi wa serikali kuu wataanza mpango huo ktk bajeti ya 2011/2012.

mlikuwa wap kuyaweka wazi toka zaman ili uma na madr wengne wajue kinachoendelea,,,,???
 
hii ni dalili za udhaifu wa serikali ya Jakaya Mrisho Kikwete.
 
nawaunga madaktar mkono kwa 100%..haiwezekani ikulu ikarabatiwe kila mwaka kwa mabilioni ya shilingi..2011/12-6bn,2012/13-6bn..jamani nchi yetu ni maskini alafu inatumia 12bn kukarabat ikulu within 2 yrs..?
 
TISS inabidi mumshauri vizuri huyo bosi wenye mwenye kichwa kigumu wakati legelege, ishu kama hizi mtambue kuwa kuna watu wa "human Right watch" wanahesabu na kuchukua data za idadi ya watu wanaokufa kutokana na akili za mcheza ngoma, sasa anapotoka kwenye power msishangae anapelekwa kwenye mahakama ya ICC kujibu roho za watu alizozichukua wakati wa utawala wake kutokana na uzembe na ulegelege wa kiutendaji. Kuweni makini ku-handle ishu kama hizi mtamponza bosi wenu...
 
Madaktari simamieni maslahi yenu, kama kujitoa mmejitoa sana.
Kama nyie wenye vipato vidogo mmevumilia, ni wakati wa serikali kuwajibika. Nitawashangaa sana watu watakaosema hamna utu,hawajui adha mnazozipata. Mimi ni mgonjwa hapa nilipo na nawahi mapema hospitali kesho ili nipate nguvu kuwasupport kwa nguvu zote!
 

Tatizo linalo wakumba madaktari katika kudai maslahi yenu ni kuwa hampo kitu kimoja, ama kuna wenzenu wanao wazunguka katika madai yenu ili kuyadhoofisha kama ilivyo kwa mwenzenu Imani Kondo 'marcopolop'! Wengine kati yenu watagoma kwa maslahi ya wote, wengine wataendelea na kazi kwa maslahi ya wagonjwa wasioenda kutibiwa India.

Nashauri mjiunge muwe kitu kimoja nchi nzima, then mje n maamuzi ya madaktari woote, tofauti ya hapo wengine wanagoma wengine wapo job is Ze Origino Komedy..ondoeni wanafki kati yenu.

Kibanga Msese
 
Safari madaktari wakigoma serikali ndipo itatutambua sisi wananchi wa hali ya chini kwani tumeshachoka na vifo vya ndugu zetu mpaka sasa, hamuwezi kutuambia tena eti madaktari wamekurupuka wakati walishawapa muda wa kutosha kushughulikia madai yao, udhaifu wenu hukohuko nyumbani kwenu
 
Kweli Mkuu,maana ,walijadiliana pasipo kuweka wazi ni yapi ambayo walikuwa wamaeyaongea,kwahiyo ni vema wakatuambia walikubliana mamabo gani na wakuu wa nchi,alafu tujue tunawaunga mkono au lah!
 
Hakika muda umefika, serekali mimekuwa sirikali. Sirikali hii inaonyesha tena ni jinsi gani isivyowajali watumishi wake na wananchi wake kwa ujumla. Anzeni madaktari, waalimu tunafuatia.
 
Hakika muda umefika, serekali mimekuwa sirikali. Sirikali hii inaonyesha tena ni jinsi gani isivyowajali watumishi wake na wananchi wake kwa ujumla. Anzeni madaktari, waalimu tunafuatia.:llama:
 
Ipo haja ya watanzania kukutana Jangwani tarehe 23/06/2012 kuhoji watawala waliopo madarakani sasa ni kwaajili ya nani na maslahi ya nani....Nawalika wote. Tusipoziba ufa huu tutakuta nyumba yetu (Tanzania) imeanguka tuanze kudai uhuru mwingine baada ya miaka 50
 
Hatujapata mapendekezo ya upande wa serikali ili tupime uzuri na ubaya wa maoni yake. Ni vigumu kutolea maamuzi kwa maoni ya upande mmoja. Ikumbukwe kuwa mgogoro ni wa pande mbili: Serikali na Madaktari. Upande wa madaktari hauwezi kuwa HAKIMU kwa shauri lake yenyewe. Madaktari hawawezi kusema kwa uhakika kuwa Serikali imekosa hiki au kile, jambo hili kwa maoni yangu haliwezi kuwa sawa.
Madaktari wamekuwa wakisisitiza kutaka kugoma kila mara, lakini jamii na maadili ya taaluma ya udaktari yana wazuia. Hivyo kila wakipata kisingizio cha aina yoyote wanahamaki kutaka kutimiza azma yao ya kutaka kumuumiza bila huruma mlalahoi mnyonge. Hii haikubaliki hata kidogo kama malaria. Madaktari mnatuonea bure sisi wanyonge huku mkiwa tayari mlikula fedha zetu kwa kuwasomesha. Hawa mnaodhani mnawaadhibu hawapati adhabu hiyo. Lakini pia uchumi wetu bado ni mdogo, ikiwa Viongozi wanaonekana kufuja mali isivyohalali isiwe kigezo cha kudai zaidi hata ya uwezo halisi wa nchi. Hata leo hii tukimteua mwiungoni mwenu Daktari mmoja aende Ikulu hataweza kuwalipa madaktari kadri ya madai yao. Nakubaliana maslahi ya madaktari yanaweza kuboreshwa, lakini uboreshaji ni mchakato, huwezi kuboresha maslahi kwa usiku mmoja.
 
Back
Top Bottom