Awamu ya 5 na sekta binafsi, kuna tusilolijua

Binafsi niliumia sana kufa kwa Fastjet. Kwa serikali zinazojali uwekezaji, wale akina Masha (Fastjet) wangepewa BAILOUT, then waendelee na biashara, waje walipe baadaye wanapozalisha faida. Naamini lingetendeka hili basi wangeendelea na biashara na huenda wangefika maeneo mengi sana ya nchi hii ikiwemo Chato.
Subiri nayo Precision Air itashughulikiwa muda si mrefu. Maana inaonekana kwenye ruti za Kilimanjaro Precision inajaza wakati ATCL inakuwa nusu empty
 
Binafsi niliumia sana kufa kwa Fastjet. Kwa serikali zinazojali uwekezaji, wale akina Masha (Fastjet) wangepewa BAILOUT, then waendelee na biashara, waje walipe baadaye wanapozalisha faida. Naamini lingetendeka hili basi wangeendelea na biashara na huenda wangefika maeneo mengi sana ya nchi hii ikiwemo Chato.
Fastjet ipo Zimbabwe inapiga Kazi kwa nusu bei Kama kawaida, itarudi jamaa akiondoka
 
Wewe ni Mtanzania hasa 100%, kila kitu ni lazima ufikiri kuna foul play, mtu akifa kuna mkono wa mtu, Muhindi akushitakiwa anaonewa, hivi nikuulize hao matajiri wako kama Manji wakati anakopa hakusaini na kuahidi kulipa?

Na kama halipi madeni wengine watapata wapi pa kukopa kwa maana kama kila anayekopa akigoma kulipa? Na huko Kanada unakodai ameenda akikopa hatolipa lipa deni?

Mshangao wako Sawa Sawa na wangu. Watanzania tuna safari ndefu kujikwamua na umasikini wa fikra
 
RIP Salum Shamte, ulituhumiwa na kutupwa rumande bila fursa ya kusikilizwa. But Karma is real, let's wait
6 tycoon dies with 2 year
 
Attachments

  • Screenshot_20210106_112405.jpg
    Screenshot_20210106_112405.jpg
    86.1 KB · Views: 1
Awamu ya 5 imejitahidi sana kujenga miundo mbinu ya uchumi kama Stiglers Gorge Hydro Electric Power, Standard Gauge Railway na barabara mbali mbali zinazounganisha mikoa.

Kwa upande wa sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo inayopaswa kutumia hiyo miundo mbinu hali siyo nzuri. Kwa uchache tu nimeona kama kuna kitu sisi kama wananchi hatukijui.

Maana wale watu wote viongozi wa sekta binafsi na wafanya biashara wakuu ama hatunao au wanapata misukosuko mikubwa kama ifuatavyo;

1. Reginald Mengi pengine huyu ni natural death.

2. Yusuf Manji kawa harassed, kanyang'anywa biashara zake kama ile Tigo mwishowe kakimbilia Canada.

3. Ali Mufuruki alikufa kiajabu ajabu tu eti kwa Pneumonia, sawa bana.

4. Shamte Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation yuko rumande kwa mashtaka ya kutakatisha fedha.

5. Simbeye ndiye naye last week ame resign kama Executive Secretary wa hiyo Tanzania Private Sector Foundation.

6. Mohamed Dewji alikuwa kidnapped na inadaiwa akarudi baada ya kulipa ransom.

7. Peter Zacharia wa Tarime alitaka kutekwa ila akawawahi kwa bastola. Then wakamkamata na kumfungulia mashtaka ya kutaka kujeruhi??

Yaweza kuwa ni wasiwasi wangu tu lakini ikiwa ni systematic process ya kuwa eliminate matajiri then tutajikuta tumejenga miundo mbinu ila tuna sekta binafsi DHAIFU. Na ndipo MDORORO wa UCHUMI utatokea.

Kamwe Serikali haiwezi kufanya biashara na tusitegemee sana makampuni ya kigeni kama kina DANGOTE au VODACOM. Tujenge tabaka la matajiri wetu
Nchi makini hutengeneza oligarchy (matajiri wake), kwetu hapa tunawafunga jela kwa sababu hawako ktk chama chetu.

Usiwaone akina Abrahamovic, billgates, wametengenezwa.
 
Nchi makini hutengeneza oligarchy (matajiri wake), kwetu hapa tunawafunga jela kwa sababu hawako ktk chama chetu.

Usiwaone akina Abrahamovic, billgates, wametengenezwa.
Tulifanya makosa makubwa sana mwaka 2015 kumkabidhi nchi huyu MAGUFULI
 
Kuna wakati mtu anaweza kuiba hela lkn kumbe walio ndani ya mfumo ndio walimpa ruhusa.

Maridhiano yalitakiwa yafanywe tangu kipindi kile ajira za watu zingekuwepo hadi leo.

Sasa unaweka magofu kwa manufaa ya nani? Wakati waliofanya tufike hapo wapo ndani ya utawala.

Hivi leo unapoenda kufanya mlimani city magofu kwa kuwa utawala kabla ya jpm uliingia mkataba mbovu na wa south africa anaeumia ni nani?
 
RIP Salum Shamte, ulituhumiwa na kutupwa rumande bila fursa ya kusikilizwa. But Karma is real, let's wait
Karma niliyoiyaja hapa mwaka jana tayari imechukua nafasi. Mtu kafukiwa Jana huko Chato
 
Aliyeapa atakaebakia mjini ni mwanaume matokeo yake ye ndo kakimbia jiji.
Siyo kakimbia JIJI tu, pamoja na kulindwa na majeshi, Polisi na Askari Maalum wa wa Burundi. Vilevile gari lenye mitambo ya internet jammer, wale Askari wenye detectors kwenye laptop na helicopter juu amekufa kwa COVID19, na kufukiwa kwao Chato jana sisi wenye JIJI tumebaki tunadunda.

Mungu ana nguvu na anasikia
 
RIP Salum Shamte, ulituhumiwa na kutupwa rumande bila fursa ya kusikilizwa. But Karma is real, let's wait
Karma dhidi ya Salum Shamte ilikwishamkumba Mwendazake. Na tushukuru Mungu mdugu zake wameachiwa jana kwenye Uongozi wa Rais SSH
 
Wewe ni Mtanzania hasa 100%, kila kitu ni lazima ufikiri kuna foul play, mtu akifa kuna mkono wa mtu, Muhindi akushitakiwa anaonewa, hivi nikuulize hao matajiri wako kama Manji wakati anakopa hakusaini na kuahidi kulipa?

Na kama halipi madeni wengine watapata wapi pa kukopa kwa maana kama kila anayekopa akigoma kulipa? Na huko Kanada unakodai ameenda akikopa hatolipa lipa deni?
Ili kiongozi la misukule ya dikteta magufuli sikuizi sijui lipo wapi
 
Bashite ndiye mshika mikoba aliyeandaliwa kuwa tajiri namba moja nchini kuyalinda maslahi ya baba yake wa kufikia. Mali anazomiliki Bashite ni zile anazomshikia baba yake uchwara. Nyie wengine mkifa na mfe tu.
Mungu hadhihakiwi, kaanza kufa Mwendazake na mali kaziacha. Naye Makonda dawa yake inachemka, ni suala la muda tu
 
Kwa kiasi fulani nimekuelewa,Ila ungetoa ushauri gani serikali ichukue kuimarisha sekta binafsi.
pilipili--mbuzi jibu la swali lako ni hayo aliyoyafanya Rais SSH ndani ya siku 100. Utawala wa Sheria, kutobambikiza kesi kwa wafanya biashara, kukusanya kodi ya haki na siyo kwa task force, kufungua diplomasia ya kimataifa.

Mungu kaipenda sana Tanzania kwa kutuonyesha jinsi MADIKTETA wanavyoharibu uchumi wa nchi kwa miaka 5 na siku 114. Magufuli alikuwa anatupeleka pabaya sana

KAMWE TUSIRUHUSU HILI LIJIRUDIE, Tumuombe Rais SSH amalize mchakato wa Katiba Mpya ya Rasimu ya Warioba
 
Back
Top Bottom