Awamu ya 5 na sekta binafsi, kuna tusilolijua

Kwa kiasi fulani nimekuelewa,Ila ungetoa ushauri gani serikali ichukue kuimarisha sekta binafsi.
Hivi utaishauri nini Serikali inayoua sekta binafsi? Jiulize Fast Jet iliyotutendea mema wakati ATCL iko muflisi kulikuwa na sababu kweli ya kuifungasha virago?

Angalia Serikali imeanza kufanya petty businness kama SUMA JKT kulinda majengo na kufanya ckearing and forwarding??

Ushauri wangu ni kuwa wavumilivu mpaka mwisho wa awamu hii. Duniani kote Serikali kazi yake ni kutengeneza sera na mazingira ya biashara kisha kusimama (Regulatory) na siyo Kufanya Biashara. This is wrong
 
Sekta binafsi ndiyo mwaajiri mkubwa wa wafanyakazi. Kadri sekta binafsi inavyo sinyaa ndivyo ambavyo uchumi wa nchi unavyoporomoka.
Thus Jamii makini ukiwa mjamaa katu sahau hata kupata umonita darasani,kwa hofu utawaletea umasikini. Wajamaa wote hawana confidence ya kuongoza matajiri na wasomi ni lzm wawashushe waishi kishetani, wao wanaamini Kila aliyefanikiwa ni mwizi hizi ni ideology za kifukara.
 
Hivi utaishauri nini Serikali inayoua sekta binafsi? Jiulize Fast Jet iliyotutendea mema wakati ATCL iko muflisi kulikuwa na sababu kweli ya kuifungasha virago?

Angalia Serikali imeanza kufanya petty businness kama SUMA JKT kulinda majengo na kufanya ckearing and forwarding??

Ushauri wangu ni kuwa wavumilivu mpaka mwisho wa awamu hii. Duniani kote Serikali kazi yake ni kutengeneza sera na mazingira ya biashara kisha kusimama (Regulatory) na siyo Kufanya Biashara. This is wrong

Ni Heri Nyerere tunaweza mlaumu alifanya makosa ya kiuchumi bila kujua, kuliko arudiaye makosa ya Nyerere.Uchumi wa kijamaa ulishindwa kila mahali duniani kutuletea ujamaa nyakati hizi ni sawa na kuendesha gari rivas kwenda mwanza.

Muhimu kuangalia ideology za watu kabla ya kuwapa lesseni ya udereva.
 
Awamu ya 5 imejitahidi sana kujenga miundo mbinu ya uchumi kama Stiglers Gorge Hydro Electric Power, Standard Gauge Railway na barabara mbali mbali zinazounganisha mikoa.

Kwa upande wa sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo inayopaswa kutumia hiyo miundo mbinu hali siyo nzuri. Kwa uchache tu nimeona kama kuna kitu sisi kama wananchi hatukijui.

Maana wale watu wote viongozi wa sekta binafsi na wafanya biashara wakuu ama hatunao au wanapata misukosuko mikubwa kama ifuatavyo;

1. Reginald Mengi pengine huyu ni natural death.

2. Yusuf Manji kawa harassed, kanyang'anywa biashara zake kama ile Tigo mwishowe kakimbilia Canada.

3. Ali Mufuruki alikufa kiajabu ajabu tu eti kwa Pneumonia, sawa bana.

4. Shamte Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation yuko rumande kwa mashtaka ya kutakatisha fedha.

5. Simbeye ndiye naye last week ame resign kama Executive Secretary wa hiyo Tanzania Private Sector Foundation.

6. Mohamed Dewji alikuwa kidnapped na inadaiwa akarudi baada ya kulipa ransom.

7. Peter Zacharia wa Tarime alitaka kutekwa ila akawawahi kwa bastola. Then wakamkamata na kumfungulia mashtaka ya kutaka kujeruhi??

Yaweza kuwa ni wasiwasi wangu tu lakini ikiwa ni systematic process ya kuwa eliminate matajiri then tutajikuta tumejenga miundo mbinu ila tuna sekta binafsi DHAIFU. Na ndipo MDORORO wa UCHUMI utatokea.

Kamwe Serikali haiwezi kufanya biashara na tusitegemee sana makampuni ya kigeni kama kina DANGOTE au VODACOM. Tujenge tabaka la matajiri wetu
Biashara ziko hoi. Capital inaporwa kwa kisingizio cha kukusanya kodi. Am shocked with what I see going on around
 
Ni Heri Nyerere tunaweza mlaumu alifanya makosa ya kiuchumi bila kujua, kuliko arudiaye makosa ya Nyerere.Uchumi wa kijamaa ulishindwa kila mahali duniani kutuletea ujamaa nyakati hizi ni sawa na kuendesha gari rivas kwenda mwanza.

Muhimu kuangalia ideology za watu kabla ya kuwapa lesseni ya udereva.
Hata China na Russia wametoka kwenye Ukomunisti. Wana mifumo ya kuwawazesha matajiri wazawa kama akina Abromavich wa Russia au Jack Ma wa China
 
Awamu ya 5 imejitahidi sana kujenga miundo mbinu ya uchumi kama Stiglers Gorge Hydro Electric Power, Standard Gauge Railway na barabara mbali mbali zinazounganisha mikoa.

Kwa upande wa sekta binafsi ambayo ndiyo injini ya maendeleo inayopaswa kutumia hiyo miundo mbinu hali siyo nzuri. Kwa uchache tu nimeona kama kuna kitu sisi kama wananchi hatukijui.

Maana wale watu wote viongozi wa sekta binafsi na wafanya biashara wakuu ama hatunao au wanapata misukosuko mikubwa kama ifuatavyo;

1. Reginald Mengi pengine huyu ni natural death.

2. Yusuf Manji kawa harassed, kanyang'anywa biashara zake kama ile Tigo mwishowe kakimbilia Canada.

3. Ali Mufuruki alikufa kiajabu ajabu tu eti kwa Pneumonia, sawa bana.

4. Shamte Mwenyekiti wa Tanzania Private Sector Foundation yuko rumande kwa mashtaka ya kutakatisha fedha.

5. Simbeye ndiye naye last week ame resign kama Executive Secretary wa hiyo Tanzania Private Sector Foundation.

6. Mohamed Dewji alikuwa kidnapped na inadaiwa akarudi baada ya kulipa ransom.

7. Peter Zacharia wa Tarime alitaka kutekwa ila akawawahi kwa bastola. Then wakamkamata na kumfungulia mashtaka ya kutaka kujeruhi??

Yaweza kuwa ni wasiwasi wangu tu lakini ikiwa ni systematic process ya kuwa eliminate matajiri then tutajikuta tumejenga miundo mbinu ila tuna sekta binafsi DHAIFU. Na ndipo MDORORO wa UCHUMI utatokea.

Kamwe Serikali haiwezi kufanya biashara na tusitegemee sana makampuni ya kigeni kama kina DANGOTE au VODACOM. Tujenge tabaka la matajiri wetu

Matajiri wengi ni MAFISADI wakubwa mno.
Chukulia mfano Yusuph Manji, anakopa bilioni 10 toka NSSF ananunua na kurabati quality plaza na na Ubungo Godowns, miezi mitatu baadae anawauzi NSSF Ubungo Godowns kwa bilioni 50 then anawauzia PSPF ile Quality Plaza kwa karibia 40 bilioni, jumla ni takriban bilioni 90
Halafu anabaki Kama mpangaji pale Quality bila kulipa mpaka deni linafikia bilioni 13!!!
Au angalia ule Mradi wa dege eco village, mtu kakopa NSSF anenda kununua ekari 300 Kisha anarudi kuuwauzia haohao NSSF kwa Bei ya milioni 800 kwa eka moja Kama hisa kwenye mradi na anakuwa main shareholder..
Manji huyu kachota Dola milioni 29 kupitia kashfa ya kagoda, karibu bilioni 27 za kibongo.
Manji huyu ndio kachukua viwanja vya waislamu na kuuwauzia hao security funds..
Bado Kuna issue ile ya Coco Beach
Kifupi huwezi kuwa na matajiri wanaopata utajiti wao kwa njia za kina Manji..
Ni kuaibika
Ni kudharaulika
Ni kujitukanisha
Ni kashfa

Washughulikiwe
 
Attachments

  • Screenshot_2021-01-05-08-29-56-32.jpg
    Screenshot_2021-01-05-08-29-56-32.jpg
    103.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_2021-01-05-07-50-47-75.jpg
    Screenshot_2021-01-05-07-50-47-75.jpg
    196.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_2021-01-05-07-50-47-75.jpg
    Screenshot_2021-01-05-07-50-47-75.jpg
    196.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_2021-01-05-08-25-17-09.jpg
    Screenshot_2021-01-05-08-25-17-09.jpg
    75.7 KB · Views: 1
Hata China na Russia wametoka kwenye Ukomunisti. Wana mifumo ya kuwawazesha matajiri wazawa kama akina Abromavich wa Russia au Jack Ma wa China
China sheria ya ufisadi ni kwa wote watawala na watawaliwa.Huku ni fimbo kwa wasio na chapa 666,na wasiotaka kuunga juhudi
 
Hivi utaishauri nini Serikali inayoua sekta binafsi? Jiulize Fast Jet iliyotutendea mema wakati ATCL iko muflisi kulikuwa na sababu kweli ya kuifungasha virago?

Angalia Serikali imeanza kufanya petty businness kama SUMA JKT kulinda majengo na kufanya ckearing and forwarding??

Ushauri wangu ni kuwa wavumilivu mpaka mwisho wa awamu hii. Duniani kote Serikali kazi yake ni kutengeneza sera na mazingira ya biashara kisha kusimama (Regulatory) na siyo Kufanya Biashara. This is wrong
Binafsi niliumia sana kufa kwa Fastjet. Kwa serikali zinazojali uwekezaji, wale akina Masha (Fastjet) wangepewa BAILOUT, then waendelee na biashara, waje walipe baadaye wanapozalisha faida. Naamini lingetendeka hili basi wangeendelea na biashara na huenda wangefika maeneo mengi sana ya nchi hii ikiwemo Chato.
 
Matajiri wengi ni MAFISADI wakubwa mno.
Chukulia mfano Yusuph Manji, anakopa bilioni 10 toka NSSF ananunua na kurabati quality plaza na na Ubungo Godowns, miezi mitatu baadae anawauzi NSSF Ubungo Godowns kwa bilioni 50 then anawauzia PSPF ile Quality Plaza kwa karibia 40 bilioni, jumla ni takriban bilioni 90
Halafu anabaki Kama mpangaji pale Quality bila kulipa mpaka deni linafikia bilioni 13!!!
Au angalia ule Mradi wa dege eco village, mtu kakopa NSSF anenda kununua ekari 300 Kisha anarudi kuuwauzia haohao NSSF kwa Bei ya milioni 800 kwa eka moja Kama hisa kwenye mradi na anakuwa main shareholder..
Manji huyu kachota Dola milioni 29 kupitia kashfa ya kagoda, karibu bilioni 27 za kibongo.
Manji huyu ndio kachukua viwanja vya waislamu na kuuwauzia hao security funds..
Bado Kuna issue ile ya Coco Beach
Kifupi huwezi kuwa na matajiri wanaopata utajiti wao kwa njia za kina Manji..
Ni kuaibika
Ni kudharaulika
Ni kujitukanisha
Ni kashfa

Washughulikiwe
Hapo ni government corrupt huyo manji alichukua hela nssf kwa nguvu,kupora, kuvunja safe ya pesa au ni sababu ya serikali iliyoooza.
 
Kuna ahadi iliyotolewa na haijawahi tenguliwa "kufanya chochote kwa tajiri,kuwafanya waishi kama shetani".
Tuyaishi matamko haya kwa miaka 5 mingine!
 
Matajiri wengi ni MAFISADI wakubwa mno.
Chukulia mfano Yusuph Manji, anakopa bilioni 10 toka NSSF ananunua na kurabati quality plaza na na Ubungo Godowns, miezi mitatu baadae anawauzi NSSF Ubungo Godowns kwa bilioni 50 then anawauzia PSPF ile Quality Plaza kwa karibia 40 bilioni, jumla ni takriban bilioni 90
Halafu anabaki Kama mpangaji pale Quality bila kulipa mpaka deni linafikia bilioni 13!!!
Au angalia ule Mradi wa dege eco village, mtu kakopa NSSF anenda kununua ekari 300 Kisha anarudi kuuwauzia haohao NSSF kwa Bei ya milioni 800 kwa eka moja Kama hisa kwenye mradi na anakuwa main shareholder..
Manji huyu kachota Dola milioni 29 kupitia kashfa ya kagoda, karibu bilioni 27 za kibongo.
Manji huyu ndio kachukua viwanja vya waislamu na kuuwauzia hao security funds..
Bado Kuna issue ile ya Coco Beach
Kifupi huwezi kuwa na matajiri wanaopata utajiti wao kwa njia za kina Manji..
Ni kuaibika
Ni kudharaulika
Ni kujitukanisha
Ni kashfa

Washughulikiwe
Hizi property zote ulizotaja Yusuf Manji hakujichukulia bali aliidhinishiwa na Mamlaka za Kiserikali. Kama tungekuwa na Rule of Law tungewawajibisha na Watumishi wa Seikali waliohusika kumpa hizo properties. Kinyume chake tumemshtaki kwa kutumia heroine na kuwaleta Wahindi kufanya kazi bila vibali!!!

Hapo ndipo kuna shida
 
Back
Top Bottom