Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,529
- Thread starter
- #81
Hatutafuti Malaika, bali mtu ambaye ana msimamo tofauti na status quo, tu ambaye yuko tayari kusimama na kuukana mfumo mbovu.
Kama kuna kitu kinachotushinda Watanzania, ni kukubali pale tunapokosea. Kukubali makosa ni Uungwana na si dallili ya Udhaifu. Ni dalili ya Uwajibikaji na si dalili ya kushindwa kazi.
Lowassa anajulikana kuwa ni mchapa kazi mzuri sana. Lakini udhaifu wake siku zote ni kukataa kuwajibika kulikoongozana na tamaa.
Mrema naye ni mchapa kazi ambaye si systematic, lakini kuchacharika chacharika kwake, kulikuwa na impact to an extent, sema kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala, yakamkuta yale yale ya Sokoine kuchunguza Mawaziri wenzake wakati wa vita vya Uhujumu na vikao vya Chama na Serikali vikaamua walio Mawaziri au wakubwa wengine waachwe.
Hili la kulindana na kuoneana haya ni tatizo sugu, mpende msipende. Yule ambaye atatoka ne ya mstari, Uhai wake na maisha yake pamoja na kipato, yanakuwa yamo mashakani na kuwekwa herani.
Tanzania inahitiaji mwendawazimu, ili tuanze kupata mabadiliko. Tulikuwa na Mwanafalsafa Nyerere, tukachechemea, akaja Mzee wa Busara Mwinyi, tukamhujumu, kisha akaja Mtaalam Mkapa, tukazugika na kuingia mkenege kuwa kulipwa kwa madeni yetu basi kila kitu kilikuwa kinaenda vyema, na sasa tuna Mtanashati cool guy and laid back, na tunaona kigugumizi cha kunyoosha mfumo kwenda kwenye mstari unaotakikana.
Leo hatuhitaji eti msomi au mwenye maono, tunahitaji mtu ambaye ataia kila mtu matumbo joto na kuanza kuchacharika, mtu ambaye ata micro manage nchi katika kila kitu ili kuongeza ufanisi, kuleta uwajibikaji na kuamsha nidhamu ya kweli si nidhamu ya woga au ya kinafiki.
Mrema anasimama kama kichaa anayehitajika kwa Tanzania, akiwa na timu nzuri ya washauri na akapangwa sawa, Mrema anaweza kuleta mabadiliko makubwa kuliko tuliyoyatarajia.