Oxlade-Chamberlain
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 8,635
- 2,198
mimi naamini kwamba kuna njia moja tu ya kuitoa ccm madarakani na hii inaweza kutokea kama vyama vya upinzani vyote vitaungana kusimamisha mgombea mmoja tu na viongozi wengine wakubwa wote waliobakia kwenye upinzani wakagombea ubunge kwenye majimbo yao husika.na hili litawezekana kama pia watakuwa wakali sana na tume ya uchaguzi hili ufanyike kwa haki sio kama miaka iliopita.Ninauhakika Mrema bado ana nafasi ya pekee sana. Katika Project X mojawapo ya mambo tunayoangalia ni nani atampinga JK mwakani kwa ufanisi mkubwa. Huyu tutamtengeneza na mojawapo ya majina matatu tunayoyaangalia ni la Mrema.
wananchi tuko tayari kwa mabadiriko kwani enough is enough with ccm na hakuna anayependa kutaabika wakati utajiri wa nchi yetu tunauona hivi hivi unaliwa na wachache.tatizo kubwa ni wao wapinzani kwani wameshindwa kutufanya tuamini kwamba wako tayari kutuongoza kwani wao wenyewe wanashindwa kujiongoza kwenye vyama vyao.
Kama wapinzani kweli wana uchungu na nchii hii basi waweke tofauti zao pembeni na wakubaliane kuweka mgombea mmoja na wakubwa waliobaki waingie bungeni.kwa njia naamini kama hawatofanikiwa mwakani basi 2015 nchi itakuwa yao.
swala la wapinzani kugawanyika sasa hivi ni wanaisaida ccm sana kwani mgawanyiko wao unagawanya kura pia na mwisho wa siku ccm ndio anaishia kuwa na kura nyingi kuliko wao.hakuna sababu yakusimamisha wagombea wa ubunge wa 4 au 5 kutoka upinzani kwenye jimbo moja,kwani hii inasaidia ccm zaidi.
kazi kwenu wapinzani kama kweli mnaipenda hii nchi na mnataka kutuletea maendeleo wananchi basi inabidi mjiunge mapema mno hili sisi wananchi tujue msimamo wenu huko vipi.
Last edited: