Augustine Lyatonga Mrema: Mpiganaji!

mimi naamini kwamba kuna njia moja tu ya kuitoa ccm madarakani na hii inaweza kutokea kama vyama vya upinzani vyote vitaungana kusimamisha mgombea mmoja tu na viongozi wengine wakubwa wote waliobakia kwenye upinzani wakagombea ubunge kwenye majimbo yao husika.na hili litawezekana kama pia watakuwa wakali sana na tume ya uchaguzi hili ufanyike kwa haki sio kama miaka iliopita.
wananchi tuko tayari kwa mabadiriko kwani enough is enough with ccm na hakuna anayependa kutaabika wakati utajiri wa nchi yetu tunauona hivi hivi unaliwa na wachache.tatizo kubwa ni wao wapinzani kwani wameshindwa kutufanya tuamini kwamba wako tayari kutuongoza kwani wao wenyewe wanashindwa kujiongoza kwenye vyama vyao.
Kama wapinzani kweli wana uchungu na nchii hii basi waweke tofauti zao pembeni na wakubaliane kuweka mgombea mmoja na wakubwa waliobaki waingie bungeni.kwa njia naamini kama hawatofanikiwa mwakani basi 2015 nchi itakuwa yao.
swala la wapinzani kugawanyika sasa hivi ni wanaisaida ccm sana kwani mgawanyiko wao unagawanya kura pia na mwisho wa siku ccm ndio anaishia kuwa na kura nyingi kuliko wao.hakuna sababu yakusimamisha wagombea wa ubunge wa 4 au 5 kutoka upinzani kwenye jimbo moja,kwani hii inasaidia ccm zaidi.
kazi kwenu wapinzani kama kweli mnaipenda hii nchi na mnataka kutuletea maendeleo wananchi basi inabidi mjiunge mapema mno hili sisi wananchi tujue msimamo wenu huko vipi.

Kuungana ni wazo zuri sana, ila tatizo kuna vyama pandikizi, hivi hata mkiungana vitawavuruga zaidi. Niliwahi kuanzisha thread ambamo nilizungumzia Sitta kubaki CCM lakini afanye kazi ya upinzani; kama vile CCM inavyopandikiza vyama au wanachama/viongozi katika upinzani ili ipate siri zake na kuwavuruga kirahisi. Ebu kumbuka mgombea urais (toka upinzani) wa mwaka 2005 ambaye sasa amerudi CCM! Ni hatari, mnaweza kuungana na mkamuweka mgombea mmoja lakini karibu na mwisho wa kampeni anatangaza kurudi CCM; linakuwa ni pigo tosha!
Sisi wenyewe tumeshapambanua mpinzani wa kweli ni yupi, basi tumuunge mkono huyo huyo, hao wanaobaki wataamua wenyewe kuungana naye au kubaki walivyo!
 
Natofautiana na wengi humu. Mrema ushujaa wake uko wapi zaidi ya kujitoa CCM? Si huyu kwa sababu ya kupenda ukubwa ndiye aliyeharibu kila alipoenda? Huyu ndiye aliyekuwa tumaini kubwa la wanaotaka mabadiliko lakini akaichezea cooni hiyo turufu. Hapana, mimi sijaona bado ushujaa wake.

Amandla.......
Huo ulioutaja ni ushujaa wa kwanza - kujitoa CCM
Pili kumbuka alivyokamata dhahabu ya wakubwa pale airport (na hapa ndipo alianza kutofautiana nao).
Tatu, kumbuka alivyowasema waziwazi akina patel na mashamba ya mkonge - ni wale wale patel wa sasa! mpaka mzee wa Tanganyika akawaita ma*********
Kumbuka watu walivyosalimisha silaha katika vita dhidi ya ujambazi na namna alivyoendeleza mkakati wa sungusungu
the list is very long.
Hata Nyerere alikuwa anapiga kampeni akisema mchagueni Mkapa lakini hakuna mahali popote aliposema Mrema ni mbaya!
Kuanguka kwake katika NCCR Mageuzi ni akina Mabere ambao aliamini ni wapinzani wa kweli kumbe wapi; inasemekana walitaka hata kumuua mkutanoni Tanga kama si mlinzi wake kumkata mtama akaanguka na risasi ikapita!
Historia itamtaja kama shujaa kweli. Ngoja CCM ianguke uone ukweli uakavyojulikana!
Yuko wapi tuliyemuona kuwa shujaa wetu pale manzese na Ubungo Dr. Lamwai, si amejionyesha asivyokuwa shujaa! hao ndio walimdanganya mrema. Yuko wapi makongoro nyerere, si alirudi ccm - ni katika kundi lililokuwa na mrema nk. Nakubalina na aliyesema kuwa mrema aliamini kuwa kila aliyeko upinzani ni mpinzani wakweli kumbe wapi - wengine walikuwa ni vibaraka wa CCM kama ilivyojidhihirisha baadae.
Na hili ndilo linafanya muungano wa wapinzani usiwezekane maana unamuona leo ni mpinzani kesho anarudi CCM. Mrema ana udhaifu wake kama mtu lakini kwa upinzani ni mpinzani kweli maana hata akianza kuhutubia utaona alivyojawa na uchungu na nchi hii - akionyesha hivyo watu wanaambiwa eti ana jazba - siyo jazba, ni uchungu na uzalendo! Please...!
 
mimi naamini kabisa mrema alikosea kutoka ccm kwa wakati ule.
nia yake ya kutaka kuleta mabadiliko na kuwa kiongozi wa TZ ilikuwa nzuri, lakini njia ya jinsi ya kufika huko(kuwa kiongozi wa TZ) ndio ilikuwa mbaya.

saa ingine kama unataka kufika kileleni cha kazi yako/siasa au mambo mengine lazima utii amri za wakubwa wako hata kama ukubaliani nao.

kwa wakati ule mrema alikuwa kwenye nafasi nzuri sana na kama angebaki ccm, si mkapa wala kikwete wangeweza kusimama na mrema. sasa hivi tungekuwa tunamuongelea mrema kama x-president, na kama angekuwa rais 1995 basi angeweza kupambana na mafisadi/ufisadi wote....

hali kama ya mrema imejitokeza hivi karibuni kwa zitto (ingawa motive za zitto kugombea hazijulikani), lakini zitto alichokifanya amewasikiliza wazee wa chadema kwa ajili anajua time yake itafika. zito anachotakiwa kufanya ni kucheza vizuri na kuakikisha vitu vilivyompatia umaarufu anaviendeleza, kwa ajili katika wanasiasa TZ ambao ni +/- 5 ya umri wake yeye ndiye maarufu

je mrema angebaki ccm na kutii ya wakubwa wake sasa hivi tungekuwa tuna mwita X-president????

Hapana asingekuwa president kwanza Nyerere hakuwa amemuweka katika msururu wa aliokuwa amewaandaa, pili tayari kwa utendaji wake alishtofautiana na wakubwa (kukamata dhahabu airport, utapeli katika uwekezaji katika mashamba ya mkonge nk), hivyo asingeweza kupita katika NEC.
OK. Mrema hatakuwa rais lakini kujitoa kwake ccm kuliwafumbua macho wananchi na kuanza kuona kuwa upinzani ni jambo zuri. Kumbuka wakati wa kura za maoni kama vyama vingi vianzishwe au la, asilimia 20 tu ndio walisema vianze, lakini mrema alipotoka CCM, katika uchaguzi alipata around 40% Wonderful! - Na hii ni baada ya kuibiwa kura nyingi sana - kumbuka DSM majimbo yote wapinzani walikuwa wameshinda - saa nane usiku ikatangazwa kuwa uchaguzi wa DSM tu umefutwa! au mmesahau?
 
..sidhani kama Mrema alikuwa akiwa-treat wapinzani vizuri na kwa heshima.

..pia zilianza kuenea fununu kwamba Mrema naye anachukua kidogo-dogo toka kwa wafanyabiashara wakubwa.

..tena nakumbuka alikuwa na urafiki mkubwa na wahindi familia ya kina Bora mpaka kufikia kufungua mgahawa wao hapa mjini.

..siamini kama Mrema ni mwana-demokrasia wa kweli. vilevile si mtu anayeshaurika. kuna masuala mengi sana alikuwa akishauriwa na Prof.Baregu lakini aliyapuuza na mwisho wake tunaujua.

..waanzilishi wa NCCR walichoshwa na tabia na vituko vya Mrema na zaidi suala la kutokushaurika na hicho ndicho chanzo cha mgogoro mkubwa ndani ya chama hicho.

NB:

..mkiona kama taifa tunaanza kumlilia mwanasiasa wa aina ya Mrema mjue tuna hali mbaya ya kusikitisha.
Tafuta yaliyotokea katika mkutano wa NCCR mageuzi Tanga ndipo utaona utapeli wa akina marando na si mrema. Wakati mrema anasema tukakiuze chama kwa wananchi hadi chini kabisa, marando akasema hatuhitaji chama kikubwa namna hiyo! (then hicho kisingekuwa chama, labda pressure group)
Sisi wenyewe ndio tulimwambia toka huko maana hao hawana dhamira ya kweli ya upinzani, ndipo akatafuta chama kilichokuwa kidoogo sana TLP akajiunga nacho kwani asingeweza kuanzisha chake (wangemzengwe) na pia hiyo ingeongeza utitiri wa vyama.
 
Kamakabuzi,

..sasa alipofika TLP kwanini hakujenga chama toka chini kama alivyokuwa amedhamiria kwa NCCR?

..mimi nadhani Mrema ana mapungufu makubwa kwamba hawezi kufanya kazi vizuri na viongozi wenzake.

..karibu kila chama alichokwenda amekuwa mtu wa vituko-vituko tu.

..nadhani hata CCM wangempa madaraka Mrema leo hii wangekuwa wamesambaratika.
 
Labda nitakuwa na upungufu wa misamihati lakini nadhani Mrema alikuwa na Guts. Neno shujaa ni lazima liambatane na busara, strategies za kushinda au kufikisha ujumbe vitu ambavyo viko kwenye short supply tukimzungumzia ndugu Mrema.

.

- Mkuu Zakumi, heshima mbele sana, maana hapa tupo ukurasa mmoja.

Respect.

FMEs!
 
Kweli amekuwa mtu exeptional pamoja na kwamba tulimwazia tofauti, hakuna aliye kamili lakini yale mazuri zaidi yanapoonekana hatuna budi kuyasema. Mrema amekuwa mpinzani mahiri wa kwanza Tanzania, tukiachana na mabaya yaliyomtokea, ukweli utabaki kwamba alikuwa mzalendo wa ukweli na hata Mwalimu angeibuka leo hii angemwambia mwanangu shika hili rungu hawa wangu walikuwa wanafiki nikiwa hai.

An innocent person never dies in his own house
 
Kweli amekuwa mtu exeptional pamoja na kwamba tulimwazia tofauti, hakuna aliye kamili lakini yale mazuri zaidi yanapoonekana hatuna budi kuyasema. Mrema amekuwa mpinzani mahiri wa kwanza Tanzania, tukiachana na mabaya yaliyomtokea, ukweli utabaki kwamba alikuwa mzalendo wa ukweli na hata Mwalimu angeibuka leo hii angemwambia mwanangu shika hili rungu hawa wangu walikuwa wanafiki nikiwa hai.

An innocent person never die in his own house
 
Zakumi,

..by the time Mrema anakwenda upinzani, serikali ya CCM ilikuwa very unpopular.

..kulikuwa na migomo karibu ktk kila taasisi kuanzia waalimu, madaktari,wanafunzi chuo kikuu, na hata wanajeshi inasemekana walikuwa very frustrated.

..kwa msingi huo kujitoa ktk serikali ambayo tayari imekosa umaarufu na imepoteza uhalali machoni mwa wananchi sidhani kama ni tendo la kishujaa, au kuwa na guts hata kidogo.

..Mrema alikuwa humohumo akiuma na kupuliza, akiwatikisa wana CCM wenzake ili apate ulaji zaidi--kumbuka alivyokamata dhahabu na kuishia kuwa Naibu Waziri Mkuu, sasa mwisho walipokosana ktk ulaji/mgao ndiyo akaamua kujitoa.

..Mrema alikuwa maarufu kushughulikia matatizo ya wizara nyingine wakati wizarani kwake mambo ya ndani kumedorora.

..katika kipindi chake cha uwaziri wa mambo ya ndani usafirishaji madawa ya kulevya ulikithiri nchini. utoroshwaji wa nyara za serikali kupitia viwanja vya ndege na bandarini uliongezeka kwa kiwango kikubwa. noti bandia zilisambaa nchi nzima. uingizwaji bidhaa za magendo mipakani, na kwa kiwango kikubwa kupitia ktk jimbo lake la uchaguzi, ulikithiri.
 
Si kweli Zakumi,si kweli kwamba neno shujaa lazima liambatane na maneno hayo niliyo ya highlight...Once again ume categorize namna ya ushujaa unaotaka mtu flani awe nao bila kuzingatia historia halisi. Mkwawa ni shujaa,ali committ suicide,si kila mtu anaamini kuwa ku committ suicide ni ushujaa and so forth...Tujadili kama grat thinkers wa kweli na tuweke porojo pembeni. Kwa mtu kama Mrema alikuwa na mtaji wa kisiasa,na mtaji huo ni wafuasi,hata hao wenye kutaka mabadilko watayapata vipi kama hakuna wananchi wenye kusapoti?Mabadiliko ya katiba yatapatikana vipi kama huta wamobilize wananchi towards that agenda?Hao mnaodai walikuwa na agenda nzuri si kweli,wote walikuwa wakiwamezea mate wananchama kwani the more you have the better off you are.

Hilo la ushujaa ni pana, however thread heading inasema "Mpiganaji" we can discuss both,personally base on the real situation on the ground at the time,Mrema is still a hero,hiyo ni bila kutumia vigezo vyangu binafsi kama wewe ulivyofanya kwa kusema eti neno shujaa lazima liambatane na busara na winning strategies,ukweli ni kwamba si kweli kuwa kila shujaa huwa anatafuta ushindi. Kwa kufanya mambo amabayo si wengi wanaweza kuyafanya ama ku ya accomplish ni characteristic ya ushujaa,na hilo liko wazi miongozi mwa wanasiasa wetu....Hakuna anayethubutu kuutema ulaji by anymeans.

Kutaka kumsingle out Mrema kuwa aliyazuia mabadiliko ya katiba ni upotoshaji...Alifanya kazi yake lakini kikwazo ni wengi wetu,na bado pia hadi sasa kikwazo cha vita ya ufisadi ni wengi wetu.

Kabla ya kuendelea itabidi niweke sawa. Mkwawa alikuwa na strategic nyingi sana zikionyesha umakini wake kama kiongozi. Kwanza alikuwa na vikosi vya wapepelezi, vilivyompa taarifa ya maendeleo ya wajerumani na kuweza kuandaa majeshi yake.

Pili aliweza kupigana ana kwa ana na kushinda vita ya kwanza. Aliposhindwa vita ya pili alianza Guerrilla warfare iliyochukua zaidi ya miaka mingi.

Commit suicide kulitokana na ukweli kuwa alikuwa THE LAST SOLDIER STANDING. Characteristcs za Mkwawa hazipatikani kwa viongozi wetu wa sasa.

Tukirudi kwenye mada. Ni lazima yawepo maelezo ya nani mpiganaji. Mpiganaji ni mtu anayepigania kitu (Rebel With A Cause). Hama sivyo upiganaji utakuwa fashion statement kama tunavyoona sasa.

Mrema kwa kutokuwa na mipangilio alilipotezea taifa muda tu.
 
Mkwawa alikuwa na strategic nyingi sana zikionyesha umakini wake kama kiongozi. Kwanza alikuwa na vikosi vya wapepelezi, vilivyompa taarifa ya maendeleo ya wajerumani na kuweza kuandaa majeshi yake.

There you sound like the socialist Companero...Lol
 
Wakati naendelea kulumbana na FMES na Mzee Mwanakijiji kuhusu wajibu wa Wapiganaji, Vita ya Wapiganaji na ni nani anafaidika na Upiganaji,

1. jina moja linakuja mukichwa na dhamira inaniambia kuwa hukukweli alikuwa ni mpiganaji.

2. Mrema pamoja na udhaifu wake wa kuchemka kwa nguvu ya soda, kuwa na elimu duni na kufanya mambo kwa pupa,

3. Kitendo chake cha kutoka CCM ni kwa kuwa aliweka Utaifa na Utanzania mbele na si maslahi yake binafsi au ya chama.

4. Naomba mwenye kumbukumbu nzuri, atukumbushe ni kwa nini Mrema aliamua kuasi ndani ya Baraza la Mawaziri na hata kuamua kuachana na CCM na kuingia upinzani?

5. Nakumbuka tetesi ni kuwa alikataa kukubaliana na uamuzi wa Baraza la Mawaziri (collectively responsibility) kufumbia macho wizi wa fedha BOT ama kupitia mfuko wa EPA au CIS na aligangamaa kuwa ataanzisha uchunguzi na kupeleleza kilichotokea. Alipoambiwa alifumbie macho, akaghadhibika na kukataa kukaa upande mmoja na Baraza la Mawaziri na Serikali na hivyo kuasi na kulazimika kujivua/kuvuliwa uwaziri na mwishowe kujitoa CCM.

- Kama kawaida na propaganda za kuwa-mislead wananchi ili wakubali kudanganywa milele, Mrema alitoka CCM kwa sababu moja tu muhimu nayo ni pale CCM, NEC ilipokutana na kuamua kwamba hawatamsimisha mgombea asiye na Degree japo moja, Mrema hakuwa na degree na alitaka kugombea urais under CCM,

- Akaenda kwa Scandnavians ambao walikuwa wameshachoshwa na CCM na jinsi walivyotumia misaada yao mingi vibaya toka uhuru wakamuahidi kumpa a strong support ya hali na mali Mrema, ndio akajitoa na infact they came through na promise yao, kwa kumpa hela nyingi sana katika kumsaidia kushinda ubunge wa Temeke,

- The same thing Scandnavians did a try on Mama Tibaijuka na Mama Mongella, lakini CCM wakashituka mapema na kuwazuia hawa kabla hawajafika mbali.

- One thing ninaweza kukikubali in Mrema, ilikuwa ni gutts za kusema ukweli anaopewa na forces kutoka ndani ya watawala katika mazingara magumu sana kisiasa then ambapo Mkapa hakuwa tayari kusikia anything tofauti na anachotaka,

- Eti Mrema awe mfano wa wapiganaji wakweli kwa taifa letu kwa sasa na in the future, ninasema no way kwa sababu Mrema always depended on all his ugly information kutoka kwa viongozi wa CCM kama Mzindakaya, ambaye na yeye alikuwa anazitumia hizo info (alizokuwa akipewa na wakubwa zaidi kama Salmin, ambaye alitaka sana kuwa Rais wa jamhuri ya muungano), kutafuta mlo tu na alipopewa mlo na Mkapa akatulia.

- Baadaye hawa hawa viongozi wakubwa wakaanza kumtumia Mtikila, na kumtupa Mrema kutokana na kukosekana kwa results walizozitaka na ndipo hata umaarufu wake ukaenda chini, matatizo yake na wenziwe kule NCCR yalianzia kwenye ruzuku kwa kuchonganishwa na wale wale waliokuwa wakimtumia kutoka ndani ya CCM na nothing else, sasa kwa shujaa wa taifa kama tunavyoambiwa kugombea hela na wenzake na hata kuishia kujiunga na chama kingine eti kweli unaweza kua ushujaa wa kuigwa na wengine na hasa wapiganaji waliobaki? Mimi nilifikiri mashujaa wa kweli hutunukiwa ushujaa kutokana na results ya kazi zao binafsi katika kusaidia wengine, ni nini hasa the results za ushujaa wa Mrema kwa taifa hili toka atoke CCM?

- Eti ni shujaa gani wa dunia kuacha Mrema kama tunavyojaribu kuambiwa hapa, ambaye alikua kazi yake kusubiri kupewa habari damaging on watawala tu na yeye kuzipigia kelele tu na akaishia kuwa shujaa wa lile taifa?

- Kama ni ushujaa basi Mrema alikuwa kwa kukubali kutumiwa na magomvi ya power between watawala, na kutumiwa sana na outside forces, against watawala maana kama Castro ni shujaa, sasa tunamuwekaje Mrema kwenye kundi moja naye? Ndio maana ninaita hii na zingine nyingi humu JF ni njama tu za makusudi kwanza kujaribu kuficha uozo wa Chadema uliojitokeza hivi karibuni na hatimaye kuwahadaa wananchi kwamba matatizo yapo CCM tu na hasa wapiganaji wa CCM

- Sijui lini wa-Tanzania tutajifunza kwamba any mis-leading political theories za kujaribu kuwahadaa wananchi siku zote zitaishia kurudisha mis-leading results, na ndio maana taifa letu limekwama hata baada ya 15 years za kuwa na vyama vingi vya siasa, ni kwa sababu hivi vyama vingi vilianzishwa na mis-leading theories kama hizi za kumtukuza Mrema kuwa ni shujaa, tunahitaji kuamuka wakuu na huu usingizi mzito sana tuliolaaniwa nao wa-Tanzania.

Eti Mrema anaweza kuka ameza moja na mashuja wa kweli kama kina Samora, Castro, Che-Guevara, Lumumba, na the rest of real mashujaa is the biggest myth of either our time kama sio the century, I mean how do you became a political hero of the land bila ya kuwa a threat to the establishment?

- Baadhi ya viongozi wa CCM wangemtumiaje Mrema a threat to their bread yaani the very CCM's establishment? It does not make any sense, ingawa inaweza kuwa ni acceptable na a very popular thinking, ndani ya a home of Great Thinkers!

Respect.

Kamanda FMEs!
 
Mrema bwana anajijua mwenyewe hata haeleweki...uchaga umemjaa sana. Mi nafikiri tuwe wa kweli maana mrema hakuna anachokifanya zaidi ya kuota urais ndo maana chama chake hakijafika popote kisa majungu yake ya kung'ang'ania cheo kikubwa. Hana tofauti na Mbowe
 
Zakumi,

..by the time Mrema anakwenda upinzani, serikali ya CCM ilikuwa very unpopular.

..kulikuwa na migomo karibu ktk kila taasisi kuanzia waalimu, madaktari,wanafunzi chuo kikuu, na hata wanajeshi inasemekana walikuwa very frustrated.

..kwa msingi huo kujitoa ktk serikali ambayo tayari imekosa umaarufu na imepoteza uhalali machoni mwa wananchi sidhani kama ni tendo la kishujaa, au kuwa na guts hata kidogo.

..Mrema alikuwa humohumo akiuma na kupuliza, akiwatikisa wana CCM wenzake ili apate ulaji zaidi--kumbuka alivyokamata dhahabu na kuishia kuwa Naibu Waziri Mkuu, sasa mwisho walipokosana ktk ulaji/mgao ndiyo akaamua kujitoa.

..Mrema alikuwa maarufu kushughulikia matatizo ya wizara nyingine wakati wizarani kwake mambo ya ndani kumedorora.

..katika kipindi chake cha uwaziri wa mambo ya ndani usafirishaji madawa ya kulevya ulikithiri nchini. utoroshwaji wa nyara za serikali kupitia viwanja vya ndege na bandarini uliongezeka kwa kiwango kikubwa. noti bandia zilisambaa nchi nzima. uingizwaji bidhaa za magendo mipakani, na kwa kiwango kikubwa kupitia ktk jimbo lake la uchaguzi, ulikithiri.

Jokakuu:

Nashukuru kwa kunipa elimu nzuri kuhusu Ndugu Mrema. Nilikuwa mshabiki sana wa Mrema wakati wa uchaguzi wa mwaka 1995. Aliposhindwa kwenye uchaguzi huo nilikata tamaa na siasa za Tanzania na kwa zaidi ya miaka miwili niliachana na debates za siasa.

Lakini miaka ilivyoendelea baada ya uchaguzi niliona kuwa ana kasoro za namna fulani ambazo zilifanya yeye kuwa ni tatizo na sio solution.
 
Zakumi,

..binafsi nilikuwa NCCR lakini Mrema alivyokwenda huko nikakosa imani na chama kile.

..kama ulivyoelekeza mwanzoni, kwamba bila kuwepo mfumo thabiti wa checks and balance, basi tutaendelea na huu mduara wa ufisadi milele na milele.

..mfumo wetu wa sheria na checks and balance ni so weak kiasi kwamba kiongozi wa Tanzania kutokushiriki ktk ufisadi ni kama suala la hiari au opptional.

..sasa ndio maana unakuta viongozi wanaingia madarakani wakiwa wasafi, na wanazungumza kwa ukali dhidi ya rushwa, lakini baadaye wanaona mazingira yanawaruhusu na wao kushiriki ufisadi kwa hiyo wanatumbukia humo.
 
- Kama kawaida na propaganda za kuwa-mislead wananchi ili wakubali kudanganywa milele, Mrema alitoka CCM kwa sababu moja tu muhimu nayo ni pale CCM, NEC ilipokutana na kuamua kwamba hawatamsimisha mgombea asiye na Degree japo moja, Mrema hakuwa na degree na alitaka kugombea urais under CCM,

- Akaenda kwa Scandnavians ambao walikuwa wameshachoshwa na CCM na jinsi walivyotumia misaada yao mingi vibaya toka uhuru wakamuahidi kumpa a strong support ya hali na mali Mrema, ndio akajitoa na infact they came through na promise yao, kwa kumpa hela nyingi sana katika kumsaidia kushinda ubunge wa Temeke,

- The same thing Scandnavians did a try on Mama Tibaijuka na Mama Mongella, lakini CCM wakashituka mapema na kuwazuia hawa kabla hawajafika mbali.

- One thing ninaweza kukikubali in Mrema, ilikuwa ni gutts za kusema ukweli anaopewa na forces kutoka ndani ya watawala katika mazingara magumu sana kisiasa then ambapo Mkapa hakuwa tayari kusikia anything tofauti na anachotaka,

- Eti Mrema awe mfano wa wapiganaji wakweli kwa taifa letu kwa sasa na in the future, ninasema no way kwa sababu Mrema always depended on all his ugly information kutoka kwa viongozi wa CCM kama Mzindakaya, ambaye na yeye alikuwa anazitumia hizo info (alizokuwa akipewa na wakubwa zaidi kama Salmin, ambaye alitaka sana kuwa Rais wa jamhuri ya muungano), kutafuta mlo tu na alipopewa mlo na Mkapa akatulia.

- Baadaye hawa hawa viongozi wakubwa wakaanza kumtumia Mtikila, na kumtupa Mrema na ndipo hata umaarufu wake ukaenda chini, matatizo yake na wenziwe kule NCCR yalianzia kwenye ruzuku na nothing else sasa kwa shujaa wa taifa kama tunavyoambiwa kugombea hela na wenzake na hata kuishia kujiunga na chama kingine eti kweli unaweza kua ushujaa wa kuigwa na wengine na hasa wapiganaji waliobaki?

- Eti ni shujaa gani wa dunia kuacha Mrema kama tunavyojaribu kuambiwa hapa, ambaye alikua kazi yake kusubiri kupewa habari damaging on watawala tu na yeye kuzipigia kelele tu na akaishia kuwa shujaa wa lile taifa?

- Kama ni ushujaa basi Mrema alikuwa kwa kukubali kutumiwa na magomvi ya power between watawala, na kutumiwa sana na outside forces, against watawala maana kama Castro ni shujaa, sasa tunamuwekaje Mrema kwenye kundi moja naye? Ndio maana ninaita hii na zingine nyingi humu JF ni njama tu za makusudi kwanza kujaribu kuficha uozo wa Chadema uliojitokeza hivi karibuni na hatimaye kuwahadaa wananchi kwamba matatizo yapo CCM tu na hasa wapiganaji wa CCM

- Sijui lini wa-Tanzania tutajifunza kwamba any mis-leading political theories za kujaribu kuwahadaa wananchi siku zote zitaishia kurudisha mis-leading results, na ndio maana taifa letu limekwama hata baada ya 15 years za kuwa na vyama vingi vya siasa, ni kwa sababu hivi vyama vingi vilianzishwa na mis-leading theories kama hizi za kumtukuza Mrema kuwa ni shujaa, tunahitaji kuamuka wakuu na huu usingizi mzito sana tuliolaaniwa nao wa-Tanzania.

Eti Mrema anaweza kuka ameza moja na mashuja wa kweli kama kina Samora, Castro, Che-Guevara, Lumumba, na the rest of real mashujaa is the biggest myth of either our time kama sio the century, I mean how do you became a political hero of the land bila ya kuwa a threat to the establishment?

- Baadhi ya viongozi wa CCM wangemtumiaje Mrema a threat to their bread yaani the very CCM's establishment? It does not make any sense, ingawa inaweza kuwa ni acceptable na a very popular thinking, ndani ya a home of Great Thinkers!

Respect.

Kamanda FMEs!

FMES:

Nilikuwa kwenye tawi la benki pale mnazi mmoja na jamaa wa NCCR wakaja kuchukua pesa za ruzuku kwenye akaunti yao. Walikuwa viongozi wa juu kama sita na kwa kutoaminiana kila mtu alipiga dole gumba.

Kama chama cha upinzani kinashindwa kutunza akaunti yake, je wataweza wakipewa nchi?

Mimi sina mapenzi na CCM, lakini watu wengi hata hapa JF wana-underestimate CCM. Haya ni makosa makubwa sana. Viongozi wa juu wa CCM wanaweza kufanyiana fitina lakini wanaweza kukaa sahani moja na kupanga dili.
 
Zakumi,

..binafsi nilikuwa NCCR lakini Mrema alivyokwenda huko nikakosa imani na chama kile.

..kama ulivyoelekeza mwanzoni, kwamba bila kuwepo mfumo thabiti wa checks and balance, basi tutaendelea na huu mduara wa ufisadi milele na milele.

..mfumo wetu wa sheria na checks and balance ni so weak kiasi kwamba kiongozi wa Tanzania kutokushiriki ktk ufisadi ni kama suala la hiari au opptional.

..sasa ndio maana unakuta viongozi wanaingia madarakani wakiwa wasafi, na wanazungumza kwa ukali dhidi ya rushwa, lakini baadaye wanaona mazingira yanawaruhusu na wao kushiriki ufisadi kwa hiyo wanatumbukia humo.

Na mpaka sasa juhudi za nchi ni kutafuta the next Nyerere, mtu ambaye si fisadi kwa hiari. Zoezi hili ni matokeo ya bahati nasibu. Cha muhimu ni checks and balance na zaidi tuwe transparency katika shughuli ya umma.
 
Mrema bwana anajijua mwenyewe hata haeleweki...uchaga umemjaa sana. Mi nafikiri tuwe wa kweli maana mrema hakuna anachokifanya zaidi ya kuota urais ndo maana chama chake hakijafika popote kisa majungu yake ya kung'ang'ania cheo kikubwa. Hana tofauti na Mbowe

Mrema ana matatizo yake lakini sioni kama yanaingiliana na kabila lake.
 
Back
Top Bottom