Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Wakuu kwema?
Askofu Mwamakula akiwa anahojiwa na mwandishi wa habari kutoka Jambo TV amesema anaona sasa sio muda sahihi wadau na vyama vya siasa kuanza kuwahukumu wabunge juu ya miswada ya sheria ya sheria za uchaguzi inayotarajiwa kurudi bungeni kusomwa tena baada ya kupokea maoni kutoka kwa wadau.
Mwamakula amesema kwa sasa baadaya ya wadau kutoa maoni Kamati, serikali na wabunge wana nafasi ya kurekebisha na kuboresha miswada hiyo, na kwamba kuwahukumu wabunge sasahivi wanaweza kusema muswada bado haujafika kwao, Kamati ikianza kunyooshewa mikono inaweza kusema bado wanapokea maoni na hawajatoa muhtasari, vipi kama maono yao yamefanyiwa kazi?
Serikali nayo ikianza kunyooshewa mikono sasa hivi wanaweza kusema wanasubiri maoni yakikusanywa ikienda pale bungeni wanaweza kuinyofoa miswada hiyo, na kwamba anaona kwa sasa bado sio muda sahihi wa kuwahukumu.
Akiongeza kuwa hapingi wanaokataa miswada hiyo isifike kabisa bungeni sasa hivi sababu ni maoni yao, wanatakiwa wasikilizwe na wasipuuzwe, lakini yeye anaona sio muda sahihi.