Askofu Basileus Ezekiel Mabumba: Lowassa asipokuwa Rais 2015 mniue!

Ndugu zangu watanzania Nyerere hakuwa mungu wa Tanzania na si kweli kuwa bila nyerere Taifa la Tanzania lisinge pata uhuru,mie naona kuwa mtu ukiwa msomi Lowassa anafaa kuwa rais wa tz. Rais wa uchina wa kwanza aitwae Maotse Dong aliendesha fitna hadi kumfunga Den shaopin na kuua vijana wake, baada ya kifo chake miaka ya 1970's Den shao pin aliusaka urais na kuupata na kuondoa mifumo dume ya kijamaa na kula kiapo kuwa endapo mipango yake ikingonga mwamba anyongwe hati mae mipango yake ilifanikisha 1978 china ilifungua milango wageni waliingia uchumi ukakuwa hadi sasa china inaongoza kiuchumi Je lowassa pamoja na kashfa zote atashindwa? ifike mahali tusitumie mambo ya Nyerere kama S.I. UNIT za future leaders. Jamani tuacheni fitna tujue nani wa kutuongozaa.
Kwa hiyo hata wezi, vibaka, mafisadi na wahuni kama Lowasa wakabidhiwe tu nchi maadamu wana mipango ya "kuiendeleza" nch? Waambieni hao maaskofu wamteue kuwa "Rais" wa familia zao au wa jumuia zao!
 
NDUGU ZANGU HUYO ASKOFU NI NANI. NINACHOJUA MWAKA 2015 watanzania ndio watakaoamua nani anakuwa Raisi wao si askofu wala nani, inawezekana askofu ana maslahi yake atueleze ni kwanini anasema lowassa atakuwa raisi amefanya utafiti wapi, au ni ndoto. Ni watanzania pekee ndiyo watakaoamua. Pia suala la utajiri si kikwazo kwa mtu kuwa kiongozi. Hakuna sheria inayozuia, na wala nyerere si msahafu au biblia kwamba kila atakachosema sisi tukubaliane nacho. Kama ni utabiri arekodi kwenye kanda ili tuje tumuulize kwani huwa hawachelewi kugeuka kwamba tuliwaquote vibaya. Labda angetabiri Raisi kutika nje ya CCM.
 
Wanabodi, tuwaheshimu maskofu ni watu makini na wasomi sio watu wa kukurupuka.
 
maaskofu bwana hapo ashapanda mbegu tayali kwa waumini zaidi ya 6000 tunaopinga jf hatufiki 300.
Kwanza huyu el si mgonjwa huyu kwanini asiachane na siasa tuu.
 
Huwa ninaamini kuwa viongozi wa dini ni waalimu katika mambo ya kiroho. Mara nyingi huwa ni watu waliobobea katika kufundisha kwa usahihi mambo wanayoyasimamia. Huyu wa sasa ananiprove wrong kwa imani yangu. Huenda hafai hata kuwa mwalimu. This is a crazy prediction.
 
askofu wa kanisa lisilo na mfumo...

accountant -- yeye
director of finance -- yeye
procurement -- yeye
kufungua tender na offer -- yeye
kusign hundi -- yeye
kupeleka sadaka benki -- yeye

ha ha ha...... kazi ipo kabla ya 2015.
 
NAWASALIMU, kiongozi mkuu wa kanisa la LAST GLORY CHURCH la hapa nchini,BASILEUS EZEKIEL MAKUMBA amesema amepokea ujumbe kutoka kwa MUNGU unaoleza kuwa aliyekuwa waziri mkuu EDWARD NGOYAY LOWASA atakuwa rais mwaka ujao wa mchaguzi mkuu na kama,na kuapa yupo tayari auwawe na watanzania kama kauli yake haitatimia. my take: lowasa ndiye chaguo sahihi kwa ccm na watanzania 2015 ana weledi wa kutosha.kwenu wadau
 
Back
Top Bottom