Askofu Basileus Ezekiel Mabumba: Lowassa asipokuwa Rais 2015 mniue!

Inawezekana, tusimshangae mtoa maada, maana siku hizi kuna raisi hata wa walevi, naye huenda akawa rais wa mafifadi nchini kulingana na pesa aliowaibia watanzania anaweza kuongoza.
 
Ingekuwa Askofu amemsemea mtu wa CDM, hoja ya makundi fulani kukosa imani na chama zingekuwa kibaoooooo!

Sijui Rejao, Ritz, Zomba mnasemaje mgombea ndani ya CCM anapigiwa debe na aaskofu?
 
Ni kweli inawezekana Lowasa ana unafuu katika utendaji kazi kati ya mfumo wa kizembe, wizi, ufisadi na kuharibu nchi wa ccm. Lakini tujue kuwa mwerevu kati ya wajinga haikufanyi wewe kuwa mwerevu ila mjinga kidogo kati ya wajinga. Tusijidanganye hata angekuja Clinton leo akaingia ccm akapewa ugombea urais, akashinda hawezi kubadilisha chochote ndani ya chama hicho kilichooza kuanzia mizizi hadi majani. Sasa huyu ambaye ni sumu mojawapo inayoozesha huo mti unaoitwa ccm lakini ni sumu kidogo kati ya sumu zote atabadilishaje mfumo aliourabu mwenyewe? Sumu itageukaje kuwa dawa. CCM kamwe haiwezi kumtoa kiongozi anayetufaa kama tunataka kuondokana na matatizo tuliyokuwa nayo licha ya rasilimali lukuki.
Juzi hapa nilikuwa na waziri mmoja wa zamani anamtetea sana Lowasa na ndivo inavoonekana kwa wana ccm wengi kuwa Lowasa anafaa kuwa kiongozi wa nchi. Alichokiri ni kuwa Lowasa alipata pesa zake kwa rushwa hasa alipokuwa waziri wa ardhi. Lakini mimi nasema hakuna tena uongozi utakaotoka ccm utakaobadilisha nchi yetu vinginevo kama tunaridhika na maendeleo, shule zetu, elimu yetu, utunzaji wa rasilimali zetu na hali zetu za maisha basi tuwachague tena hawa wezi.
 
Maamuzi ni ya watanzania kuamua sio watu wachache lakini nitapendezwa kama Rais ajaye awe Edward Lowasa coz mamuzi yake ni magumu na tanzania inahitaji kiongozi kama huyu Nawatupia lawama usalama wa taifa kwa kuhusika na kulejesha nyuma kazi ya huyu kiongozi mwenye nguvu ndani ya serikali na hakika watendaji kamwe hawata musahau kabisa.
 
Hivi jamani me naomba niulize,Huyu askofu angesema ameoteshwa slaa atakuwa raisi 2015 mngemkashifu hivi??
 
Nijuavyo viongozi wa Dini hawatakiwa kujihusisha na shughuli zozote za siasa au ushabiki wa aina yeyote, nashangaa huyo Askofu ni Anafanya kazi ya Mungu au askofu wakala wa baba wa Uongo? Pia kuna mambo mengi ya kusaidia serikali na jamii baada ya kukaa kufukiri na kuomba na kuwakilisha pamoja na kufikiri nao wameingia kwenye ushabiki usio na tija wala maana kwa wakati huu. Mpaka hapo nahakika ameshakufa kwa kujinenea yeye mwenyewe. Akumbuke KIAPO chake na Mungu anamuona ktk yote.

uaskofu si kuvaa kola wengine makanjanja tu
 
Nina wasiwasi na Uaskofu wake.....isije kuwa ni wale wa Nigeria. Wachaa waendelea kujipaka pilipili machoni
 
by daway who is nyerere? Si mtu kama mim wewe vipi sio kila aliosema yeye ni sheria mengine aliongea kwa interest zake binafsi.na chuki zake za kizanaki hasa kwa mtu aliyeona atamfunika nani asiyemjua huyu dikteta na mroho wa madaraka
usiwe mpumbavu wewe, hata kama lowassa anakupa cash lakini sidhani anakupa cash yingi kiasi hicho mpaka kuandika ujinga kuhusu baba wa taifa. lowassa aliingia kwenye siasa [ubunge na uwaziri ]1990 alafu 1995 alikua tajiri. baba wa taifa hakumtaka lowassa kwasababu
1] lowassa ni fisadi [tajiri]
2] lowassa anatamaa ya madaraka alipata ubunge 1990 alafu 1995 akautaka urais
3] lowassa anatabia ya ukabila na udini. tabia hii haitakiwi hapa tanzania
4] lowassa anatabia ya kulipa visasi. kama hamkuelewana nae siku za nyuma huyu mtu akusahau.
5] lowassa alivunja sheria za chama 1995.
 
Hahahahaaaaaaaa.........kufa kabisa kuliko kusubiri akikosa kuwa rais. Mungu kamwe hashindani na mwanadamu
 
Hapo hawata sema chochote!
Ingekuwa Askofu amemsemea mtu wa CDM, hoja ya makundi fulani kukosa imani na chama zingekuwa kibaoooooo!

Sijui Rejao, Ritz, Zomba mnasemaje mgombea ndani ya CCM anapigiwa debe na aaskofu?
 
Hii ni nchi huwezi kukurupuka tu na kudai wewe uwe RAIS ,kuna maadili ,tutampima na kumwangalia anawaza nini kuhusu tanzania au anawaza monduli tu.ameitumikiaje tanzania katika nyadhifa zake au amejitumikia yeye ,ana msimamo gani kitaifa ni mkurupakaji. anawachukulia vipi watanzania anaridhika na hali waliyonayo ,uchumi kama ni mchumia tumbo huyo hatufai hata askofu molel akijiua sawa tu .rais tunayemtaka hajakidhi viwango .
 
Back
Top Bottom