eliasmisinzo
JF-Expert Member
- Aug 13, 2021
- 1,260
- 1,320
MAGUFULI: Ni kichaa peke yake anayeweza kuushabikia mkataba wa aina hii, Sasa tunaanza kuona vichaa wakishabikia mkataba wa Kimangungo, afadhali Mangungo alikuwa hajui kusoma miaka hiyo ya 1876, lakini leo waliosaini ni wasomi halafu Chief Mangungo asiyejua kusoma anakuwa afadhali!Habari zenu wanaJF wenzangu,
Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.
Fikiria kiongozi mkubwa wa chama cha siasa anafika Kariakoo, badala ya kuwaeleza watu sera za chama chake, badala ya kuwaeleza watu namna watakavyofaidika, au taifa litakavyosonga mbele kimaendeleo na huduma bora kwa wananchi kutokana na sera hizo endapo chama chake au chao kitafanikiwa kushika dola.
Yeye anakuja na upepo wa bandari kwa kuwaeleza watu maneno mawili matatu ya kuuponda mkataba wa bandari bila kuonesha sehemu anayodai kuwa haifai, baada ya hapo anaanza kuomba michango na baadae akishachangiwa chake anatokomea anapokujua yeye kununua nyama, mchele, mafuta na mahitaji mengine ya lazima huku waliomchangia wengi wao wakienda kula dagaa na ugali usiku ule.
Sasa mtu mwenye akili unajiuliza kama mtu ana njaa hadi anaamua kuwakamua wale anaodai kwamba anawasaidia, je atashindwa kupokea hongo atakayohongwa na kundi lenye lengo la kumtumia kupush ajenda zao mbele.
Kama anachukua hadi elfu ya masikini muuza pilipili wa Kariakoo atawezaje kukataa milioni 1 au 2 ya wale wapitisha madawa ya kulevya bandarini, wezi wa vifaa vya magari na mizigo mbali mbali bandarini, wakwepa kodi na ushuru wa bandarini?
Jibu utapata kwamba jamaa amehongwa ili awapambanie waliomuhonga, na hizo za Kariakoo anazitumia kununua mahitaji yake ya siku. Ndio maana tunasema hawa viongozi wanapambana kwa sababu ya njaa zao na wakishapata chao wanatokomea kula na familia zao. Mnaosubiri kupata maendeleo kupitia viongozi hawa, hamna tofauti na mtu anaesubiri nazi ianguke kutoka juu ya mkungu.