Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,018
- 144,377
Sakata la Bandari na kashifa nyingine zinaziendelea kuibuliwa kama hii ya kuwapa Waarabu hifadhi za misitu yetu na nyinginezo kama ya Ngorongo, zinakwenda kuimalliza vibaya CCM pamoja na mgombea wao wa uraisi ambae bila shaka atakuwa ni Mama Samia kwenye uchaguzi mkuu ujao wa 2025.
Kashifa hizi, mithili ya dhoruba kali baharini, zimekuja kuzamisha mtumbwi ambao teyari ulikuwa umetoboka na sasa unajaa maji(unazama).
Mama alikuwa teyari hakubaliki sana, na badala ya kufanya mambo ambayo yangemsaidia kukubalika, amefanya kinyume chake kupata hizi kashifa zinazoendelea kuibuliwa na wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na watu wa makundi mengine katika jamiii mfano viongozi wa dini.
Ukiacha hayo, wafuasi wa Mwendazake ndani ya chama chake nao ni tatizo kwake. Hivyo, baadhi ya kura za wana-CCM, Mama atakwenda kugawan na wapinzani jambo litalokwenda kumuweka katika hali mbaya zaidi.
Sio Samia tu kama mgombea uraisi atakaeathirika(naamini atagombea), bali hata wagombea ubunge wa CCM nao wataathirika kwa kuridhia ule mkataba mbovu wa bandari.
Kama ambayo kashifa za wizi na ufisadi wakati wa Kikwete zilivyoigharimu CCM kwenye chaguzi za 2010 na 2015, ndivyo ambavyo kashifa hizi zinazoendelea zitakwenda kuigharimu vibaya zaidi CCM katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2025.
Hali ikiendelea hivi, itakuwa ni vigumu sana kwa Mama Samia kupata asilimia 30 ya kura zote na CCM kupata wabunge zaidi ya 100 kote bara na visiwani.
Najua hatuna tume huru ya uchaguzi na wala CCM hawatakubali tuwe na tume huru, lakini huo ndio utakuwa uhalisia katika uchaguzi ujao(makaratasi yatawapa uhalisia hata kama watatangaza tofauti).
Walioko hatarini zaidi ni wagombe ubunge ambao sometimes huwa ni vigumu kupindua matokeo labda kama Mama afanya kama alivyofanya Mwendake kuwa ni lazima watangazwe washindi ingawa hii inahitaji roho ngumu na elements za ukatili mambo ambayo Mama yanaweza kumshinda.
Time will tell.