Asilimia 90 ya watanzania tumeshagundua kwamba hawa viongozi wamehongwa kwa ajili ya bandari

Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.

Fikiria kiongozi mkubwa wa chama cha siasa anafika Kariakoo, badala ya kuwaeleza watu sera za chama chake, badala ya kuwaeleza watu namna watakavyofaidika, au taifa litakavyosonga mbele kimaendeleo na huduma bora kwa wananchi kutokana na sera hizo endapo chama chake au chao kitafanikiwa kushika dola.

Yeye anakuja na upepo wa bandari kwa kuwaeleza watu maneno mawili matatu ya kuuponda mkataba wa bandari bila kuonesha sehemu anayodai kuwa haifai, baada ya hapo anaanza kuomba michango na baadae akishachangiwa chake anatokomea anapokujua yeye kununua nyama, mchele, mafuta na mahitaji mengine ya lazima huku waliomchangia wengi wao wakienda kula dagaa na ugali usiku ule.

Sasa mtu mwenye akili unajiuliza kama mtu ana njaa hadi anaamua kuwakamua wale anaodai kwamba anawasaidia, je atashindwa kupokea hongo atakayohongwa na kundi lenye lengo la kumtumia kupush ajenda zao mbele.

Kama anachukua hadi elfu ya masikini muuza pilipili wa Kariakoo atawezaje kukataa milioni 1 au 2 ya wale wapitisha madawa ya kulevya bandarini, wezi wa vifaa vya magari na mizigo mbali mbali bandarini, wakwepa kodi na ushuru wa bandarini?

Jibu utapata kwamba jamaa amehongwa ili awapambanie waliomuhonga, na hizo za Kariakoo anazitumia kununua mahitaji yake ya siku. Ndio maana tunasema hawa viongozi wanapambana kwa sababu ya njaa zao na wakishapata chao wanatokomea kula na familia zao. Mnaosubiri kupata maendeleo kupitia viongozi hawa, hamna tofauti na mtu anaesubiri nazi ianguke kutoka juu ya mkungu.
MAGUFULI: Ni kichaa peke yake anayeweza kuushabikia mkataba wa aina hii, Sasa tunaanza kuona vichaa wakishabikia mkataba wa Kimangungo, afadhali Mangungo alikuwa hajui kusoma miaka hiyo ya 1876, lakini leo waliosaini ni wasomi halafu Chief Mangungo asiyejua kusoma anakuwa afadhali!
 
Naona bado akili yako haipo huru. I mean kuna mwanasiasa fulan anaitumia kwa masilahi yake na familia yake huku wewe mwenyewe ukiwa haujui kama akili yako inatumiwa.
Achana nao hao. Hata Akina Nape wako kwenye hiyo set. Division 4 ya point 28 sijui 29 ya Nape hakudtahili hata kumfanya somee Ualimu kama Mjomba wake Majaliwa.
 
MAGUFULI: Ni kichaa peke yake anayeweza kuushabikia mkataba wa aina hii, Sasa tunaanza kuona vichaa wakishabikia mkataba wa Kimangungo, afadhali Mangungo alikuwa hajui kusoma miaka hiyo ya 1876, lakini leo waliosaini ni wasomi halafu Chief Mangungo asiyejua kusoma anakuwa afadhali!
Naona unajifariji kwa comment ya kichovu. Ni hivi.. kwa sasa yale mambo ya kukwepa ushuru na kodi yanakufa kibudu. Kila mtu atahitajika kulipa kodi ili serikali ikusanye mapato.

Na ule mtindo wa vijana kuamka asubuhi kwenda kushinda bandarini kusubiri deal haramu pia hayatokuwepo 😂😂

Hakika raisi Samia ni kiboko, afu tunachompendea watanzania ni ile style yake ya kufanya kile anachoamua kufanya kwa faida ya nchi na watanzania. Hata kama magenge ya wahuni yataongea mpaka damu itoke mdomoni yeye hajali upuuzi wao.
 
Wapingaji wa maendeleo ndio mafisadi majizi.Mwizi hufikiria kila mtu ni mwizi kama yeye.
Wanaopinga ufisadi uliofanyika na DpWORLD ili kupewa Bandari wana ushahidi kuwa pesa imetembea tena pesa ndefu!!
Kwa Mfano mmoja tu ambao kama watu wazalendo wa TISS wamo humu wajalibu kufuatailia ili kuthibitisha pasipo shaka ; Kuna waziri mmoja mwanamama amenunua nyumba SYKES CLOSE mbezi beach ufukweni kwa bei ya $$$ 550,000 na amelipa cash!! Sasa ndugu zangu jiulizeni huyu mwanadada amezipataje hizo fecha za kununua nyumba na kulipa csh na sisi mishahara ya mawaziri wetu pamoja na marupu rupu yao hawawezi kuwa na ziada ya pesa hiyo!! Lazima kuna njia ya haramu imetumika kuzipata hizo pesa. Hivi sasa nae yuko mikoani akitetea DpWorld!
 
Mr Dudumizi

Msipotoshe mambo hakuna mtu mwenye akili anaye tetea TICTS waendelee ; mkataba wao wa miaka 27 umekwisha wamefunga vilago!
Tatizo ni terms za contract ya kimangungo Samia aliyosaini hata kabla ya kupata idhini ya bunge kuwapa DpWorld bandari zetu!!! Nobody questions their capability, it is the terms under which they will operate basi!! Samia ndio anasema ameziba masikio liwalo na liwe lakini DpWORLD will operate under the signed terms na hayo ndiyo wananchi hawakubaliani nae!!
 
Habari zenu wanaJF wenzangu,

Ndugu zangu,,, hapa nchini kwetu ukiwa mtu makini, mwenyekujitambua, mwenye uwezo wa kudhibiti mihemko, mwenye mawazo na akili iliyohuru bila kukontroliwa na mtu mungine ambae ataitumia akili yako kwa faida yake na familia yake huku akikuacha wewe ukidhalilika, ukiwa mwenye kutafakari kwa kina juu ya mstakabali wa nchi na future za wananchi, hakika utaweza kuona madudu mengi yaliojificha nyuma ya migongo ya viongozi wenye njaa. Kuona huko kunaweza kufanikiwa kupitia historia zao, maneno yao, na vitendo vyao.

Fikiria kiongozi mkubwa wa chama cha siasa anafika Kariakoo, badala ya kuwaeleza watu sera za chama chake, badala ya kuwaeleza watu namna watakavyofaidika, au taifa litakavyosonga mbele kimaendeleo na huduma bora kwa wananchi kutokana na sera hizo endapo chama chake au chao kitafanikiwa kushika dola.

Yeye anakuja na upepo wa bandari kwa kuwaeleza watu maneno mawili matatu ya kuuponda mkataba wa bandari bila kuonesha sehemu anayodai kuwa haifai, baada ya hapo anaanza kuomba michango na baadae akishachangiwa chake anatokomea anapokujua yeye kununua nyama, mchele, mafuta na mahitaji mengine ya lazima huku waliomchangia wengi wao wakienda kula dagaa na ugali usiku ule.

Sasa mtu mwenye akili unajiuliza kama mtu ana njaa hadi anaamua kuwakamua wale anaodai kwamba anawasaidia, je atashindwa kupokea hongo atakayohongwa na kundi lenye lengo la kumtumia kupush ajenda zao mbele.

Kama anachukua hadi elfu ya masikini muuza pilipili wa Kariakoo atawezaje kukataa milioni 1 au 2 ya wale wapitisha madawa ya kulevya bandarini, wezi wa vifaa vya magari na mizigo mbali mbali bandarini, wakwepa kodi na ushuru wa bandarini?

Jibu utapata kwamba jamaa amehongwa ili awapambanie waliomuhonga, na hizo za Kariakoo anazitumia kununua mahitaji yake ya siku. Ndio maana tunasema hawa viongozi wanapambana kwa sababu ya njaa zao na wakishapata chao wanatokomea kula na familia zao. Mnaosubiri kupata maendeleo kupitia viongozi hawa, hamna tofauti na mtu anaesubiri nazi ianguke kutoka juu ya mkungu.
Dudumizi wewe hauna nauli ya kukupeleka Kibaha huku unayemsema kila mwezi anapanda ndege kwenda majuu, sijui nako kutembeza bakuli? Bora ungekaa kimya tu.
 
Msipotoshe mambo hakuna mtu mwenye akili anaye tetea TICTS waendelee ; mkataba wao wa miaka 27 umekwisha wamefunga vilago!
Tatizo ni terms za contract ya kimangungo Samia aliyosaini hata kabla ya kupata idhini ya bunge kuwapa DpWorld bandari zetu!!! Nobody questions their capability, it is the terms under which they will operate basi!! Samia ndio anasema ameziba masikio liwalo na liwe lakini DpWORLD will operate under the signed terms na hayo ndiyo wananchi hawakubaliani nae!!
Mkuu naona na wewe hauna tofauti na wanaharakati njaa au wanasiasa uchwara ambao siku zote wapo tayari kupinga au kuongea uongo wowote ilimradi wawe na uhakika kuwa uongo huo utasaidia ku feed their big stomach.

Sijui wamewapeni nini mpaka mmekuwa wazito kujifunza kupitia uongo wao wa kila siku. Japo siamini uchawi, lkn kuna muda nahisi kuwa uchawi upo na huwa unatumiwa kuwapumbaza akili zenu kiasi cha kufikia hatua ya kuamini chochote mnachoambiwa na hao jamaa hata kama hakina ushahidi wowote mbele ya macho yenu.

Maana kwa mtu ambae hajarogwa hawezi kuwaamini watu waliodanganya umma wa watanzania kuwa Lowasa ni fisadi, afu baadae waje wadhihirishe na kukiri wenyewe kuwa sio fisadi. Swala la Lowasa halikuwa la bahati mbaya, bali lilikuwa limepengwa mahususi na Mungu ili kuwafungueni macho kuwa msiweke imani na uaminifu zaidi kwa binadam mwenzako, haijalishi ni rafiki yako, kiongozi wako au ndugu yako as longer as ni binadamu basi muda wowote anaweza kukudanganya kwa masilahi yake na familia yake.

Imagine watu wanasema mkataba ni wa kuuza bandari nk, lkn mpaka leo hakuna alieuweka huo mkataba wote hadharani ili kila mtu azione hizo kasoro. Wao ni kuhadaa kwa maneno matupu kama walivyofanya kwa Lowasa ili kuokota akili za wanaowaamini as longer as yeye atapata fursa fulan kupitia kupinga huko.
 
Wanaopinga ufisadi uliofanyika na DpWORLD ili kupewa Bandari wana ushahidi kuwa pesa imetembea tena pesa ndefu!!
Kwa Mfano mmoja tu ambao kama watu wazalendo wa TISS wamo humu wajalibu kufuatailia ili kuthibitisha pasipo shaka ; Kuna waziri mmoja mwanamama amenunua nyumba SYKES CLOSE mbezi beach ufukweni kwa bei ya $$$ 550,000 na amelipa cash!! Sasa ndugu zangu jiulizeni huyu mwanadada amezipataje hizo fecha za kununua nyumba na kulipa csh na sisi mishahara ya mawaziri wetu pamoja na marupu rupu yao hawawezi kuwa na ziada ya pesa hiyo!! Lazima kuna njia ya haramu imetumika kuzipata hizo pesa. Hivi sasa nae yuko mikoani akitetea DpWorld!
Kosa lile lile la kuamini tetesi za binadamu 🤣🤣🤣

Wanasiasa washagundua hitilafu katika akili za baadhi ya watanzania wenzetu. Sasa wanazitumia hizo hitilafu kwa masilahi yao ya kisiasa nk.

Bado kuna safari ndefu sana ya kuwafungua vijana macho na kuziweka akili zao huru kutoka katika makucha ya wanasiasa njaa.
 
Dudumizi wewe hauna nauli ya kukupeleka Kibaha huku unayemsema kila mwezi anapanda ndege kwenda majuu, sijui nako kutembeza bakuli? Bora ungekaa kimya tu.
Mkuu mimi ni masikini jeuri ninaekula kwa jasho langu, simpigi mtu mkuki wa hela ya kula wala nauli ya kwenda mjini.

Yeye unamuona ni tajiri sababu ya kula majasho ya watu, ukute hata nauli ya kuja Tz vijana wa ubelgiji walimchangia. Sasa huo ndio utajiri gani!!
 
😃😃
 
Back
Top Bottom