" La T.E.C. sio Tamko la Bandari, ni waraka wa Bandari kwa Watanzania wote" au (barua ya kichungaji kwa watanzania.)

HANGAYA THE CHIEF

JF-Expert Member
Sep 10, 2021
329
947
Tusichanganye dini na siasa, au viongozi wa dini ingieni kwenye siasa, imekuwa silaha kubwa kwa wanasiasa wezi, mafisadi, majambazi, wabadhirifu wa mali za umma, kuwazuia viongozi wa dini kufanya kazi yao ya kufundisha kuonya, na kukemea maovu katika jamii. hata wakati mambo yanakwenda vibaya, viongozi wa dini wamekuwa na wakati mgumu sana waseme nini maana wanaogopa macho ya wanasiasa. Hivyo imekuwa ni kawaida kwa wanasiasa kutumia mwanya huo na kuwagawa wananchi wao kwa kufanya watakayo kwa sababu hakuna wa kuwakemea wala kuwaonya kwa sababu ukiinua sauti kama kiongozi wa dini utaambiwa mnatugawa kidini.

Kqwa wakristo wakatoliki, tamko la maaskofu ni fundisho na rejea, ( kwa sababu linatoka kwa mamlaka fundishi), hakuna mtu yeyeto aliye juu ya maskofu, katika kanisa katoliki, ( hata papa ni askofu wa roma), kwa hiyo hakuna padre, shemasi, sister, katekista, mwenyekiti wa parokia, au yeyote atakayepinga mamlaka hiyo. kwa hiyo linachukuliwa jinsi lilivyo na kufundishwa lieleweke.

makada wanahoji kwa nini wameonge? kuwa wanachanganya dini na siasa?, ni utaratibu wa kanisa tangu zamani kuwa kazi kubwa ya kanisa katika jamii ni kufundisha na kuonya maadili mema katika jamii, rejea katika biblia barua au nyaraka za namna hii ni za kawaida, kwa mfano nayraka au barua za mtakatifu Paulo (ndio askofu wa wakati huo), kwa Warumi, Wagalatia, Wakoritho, na kadhali hizi zilikuwa nyaraka au barua za kitume kufundisha au kuonya jambo fulani katika jamii.

palipo kuwa na shida katika jamii mitume (maaskofu wa wakati huo ) walikutana Yerusalem, na kutoa waraka au barua kuonya, kukemea na kuonya.

Kwa wakatoliki barua zitokazo kwa maaskofu zina mamlaka fundishi, zinaonya, na kutuelekeza, ukiona mkatoliki anasema mimi ni mkatoliki na anapinga hajui anachokisema.

kwa wakatoliki na watu wengine lililotolewa na maaskofu katoliki sio tamko, ni waraka au barua ya kichungaji kuhusu rasilimali bandari kwa watanzania wote, inatuonya na kutufundisha na kutuonya kuwa tuache ubinafsi kwenye rasilimali bandari.

waraka huo mara nyingi unaambatana na amri ya kimamlaka ya kiaskofu kuwa na ISOMWE.
 
Muda sio mrefu machawa ya viongozi yataanza kujitokeza kujidai kuonya eti viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa, muda huu yapo kimya yanapangwa yatoke vp!.
Yanatumika hovyo kama toilet pepa!.
 
Waambie warudishe kwanza fedha za escrow
 
Muda sio mrefu machawa ya viongozi yataanza kujitokeza kujidai kuonya eti viongozi wa dini wasichanganye dini na siasa, muda huu yapo kimya yanapangwa yatoke vp!.
Yanatumika hovyo kama toilet pepa!.
yanasoma upepo, lakini pale ndio mwisho wa reli
 
Back
Top Bottom