Mingoi
JF-Expert Member
- Jul 21, 2012
- 11,715
- 6,119
Huyu jamaa hakuandaliwa kuja kuwa kiongozi na wala hana sifa za uongozi.Ninahisi hata ukarani BoT alipewa na baba mkwe ex-Governor.Ukiachilia mbali kuitumikia nchi katika maeneo tofauti na kuifahamu nchi sidhani hata kama JKT kwa mujibu wa sheria alipitia.Ukizungumzia watu wanaozunguka mlima kunufaika je wanajeshi wetu wanaolinda mipaka ya nchi usiku na mchana watalipwa nini? leo kama hakuna ulinzi wa mipaka ya nchi ambao askari wake ni wa makabila yote kutoka mikoa yote ya Tanzania kuna Mlima Kilimanjaro? Ni aibu maneno kama haya kutamkwa na mtu anaetajwa kama kiongozi na ni fedheha kwa wafuasi na wanachama wake.