Asante mh. Mbowe kwa kuliona hili,huu mkoa umefanywa shamba la bibi.

PISTO LERO

JF-Expert Member
Mar 8, 2011
2,819
1,454
Mbowe: Wananchi lazima wanufaike na Mlima K’njaro

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema Mlima Kilimanjaro hauna budi kuwaletea manufaa wananchi wa mkoa wa Kilimanajro ambao wanauzunguka mlima huo badala ya mapato yanayopatikana kuwanufaisha watu wengine.

Mbowe alisema Mlima Kilimanjaro umekuwa na mapato makubwa ambapo kwa mwaka 2010/11 zilipatikana sh bilioni 88, huku kukiwa hakuna kiasi chochote kile kilichorejeshwa kwa wananchi wa mkoa wa Kilimanajaro.

Mbowe alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa kampeni za mgombea udiwani wa kata ya Nanjara Rea, jimbo la Rombo, na kumnadi mgombe udiwani kupitia CHADEMA, Frank Salakana, ambapo maelfu ya wananchi walijitokeza.

Kampeni hizo zilihudhuriwa na wabunge mbalimbali akiwemo Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini, Suzan Lyimo, Lucy Owenya, Meya wa Manispaa ya Moshi Japhary Michael, madiwani na mkurugenzi wa masuala ya Bunge wa CHADEMA, John Mrema.

Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, alisema wananchi wanaozunguka mlima huo wana haki ya kufaidi matunda yanayotokana na mlima huo, kwani hata mlima huo ukiwaka moto wananchi hao wanakuwa wa kwanza kuzima.

“Serikali ya CCM haina huruma; mlima huo unazunguka maeneo kama Marangu, Mwika, Kilema, Rombo na Machame ambayo yako wilaya ya Hai na Siha. Ukiwauliza wananchi wa maeneo haya kama kuna fedha zozote zilikwishawahi kurudishwa kwa ajili ya kuwasaidia, watakuambia hakuna, zimeenda Dar es Salaam kuliwa na mafisadi,” alisema Mbowe.

Alisema chama hicho tayari kilikwishakutana wabunge wa mkoa wa Kilimanajaro kujadili jinsi ya kuwatetea wananchi wanaozunguka mlima huo huku akisema hata kama ikishindikana wananchi wakiipa nchi CHADEMA lazima wananchi wanaozunguka mlima huo wanufaike.

Katika hatua nyingine, Mbowe alisema chama hicho kimejipanga kuhakikisha kuwa kati ya kata 29 ambazo zina kinyang’anyiro cha udiwani lazima kata 20 ziende CHADEMA, Nanjararea ikiwa mojawapo.

Alisema safari ya kudai ukombozi wa nchi ina changamoto nyingi ambazo chama hicho kimekuwa kikikumbana nazo kwa kupambana na dola, polisi ambao wamekuwa wakiwapiga mabomu na risasi huku hata wengine wakipoteza maisha.

Hata hivyo Mbowe alikemea vikali kitendo kilichofanywa na Jeshi la Polisi kuwakamata vijana ambao walikuwa waje kwenye mkutano huo wa CHADEMA kwa kuwafungulia mashtaka ya kudai rushwa na kusema polisi wako kwa ajili ya kulinda usalama wa raia wasiruhusu kutumika na CCM.

Kwa upande wake, mgombea udiwani, Frank Salakana, aliwaomba wananchi wa kata hiyo kumchagua ili kuwawakilisha vema kwenye vikao mbalimbali vinavyohusu maendeleo ya wananchi pamoja na kushirikiana na mbunge wa jimbo hilo kuwaletea maendeleo.
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.
 
Ni wakati muafaka kumuuliza Mbowe ni Tanzania ipi anayoizungumzia kuipatia ukombozi? au M4C= MOVEMENT FOR CHAGA'S.Kuitenganisha CDM na udini.ukanda na uchaga ni sawa sawa na kutenganisha ulimi na kinywa.
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.

Hii ndiyo tunaikataa mkuu haiwezekani dhahabu itoke kahama na almas mwadui shinyanga inufaishe Lindi hilo hatutaki lindi watapata ziada kwanza wananchi wanaozunguka.Leo gesi lazima iannze na wana lindi si kuwafaidisha shinyanga ambao wana madini ya dhahabu na kilimanaro wenye mlima na utalii.Hii ndiyo tunataka katiba mpya iseme.sehemu zenye rasilimali nyingi baada ya kupata mgawo wa kutosha ziada ndiyo isaidie penye pengo kubwa hapo tutaona kasi ya maendeleo.
 
Kama wananchi wa eneo fulani hawafaidiki na rasilimali/uwekezaji kwenye eneo lao, hawawezi kutoa mchango wa kulinda, kuboresha rasilimali hizo. Mt Kilimanjaro kila mwaka unakumbwa na tatizo la moto. Watu hawaoni faida na sasa wanataka kuchukua kile wanachoweza (hata kwa gharama kubwa ya kuharibu mazingira).

Ukienda Nyamongo, au Bulyanhulu na kwingineko, ni hivyo hivyo. Watu wanachungulia tu magari yakihamisha mchanga! Mwisho wa siku ndio tunaona migogoro, na sasa wakubwa wamewapachika jina la 'wavamizi!. Lakini ukweli unabakia, wananchi wanataka wafaidike na rasilimali zilizowazunguka.
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.

na ndio maana hatuendelei.kila watu katika mikoa yao wana rasilimali zao.kila mkoa uhakikishe unanufaika na utajiri unao patikana katika maeneo yao. in that way mikoa ya wavivu itabaki nyuma na lazima ibaki nyuma kwasababu asiye fanya kazi imeandikwa asilie.ALMASI ya shinyanga wafadike watu wa dAR Kwanini? mlima upo KILIMnjaro MAPATO YANAPELEKWA DAR,why? kifupi ni kwamba kama mimi nimejitahidi nikaweka duka,asiwepo mtu wa kutaka utajiri wangu tugawane eti faida ya wote!!! HONGERA MH MBOWE MAWAZO YANGU NA YAKO YAKO SAMBAMBA
 
Ni wakati muafaka kumuuliza Mbowe ni Tanzania ipi anayoizungumzia kuipatia ukombozi? au M4C= MOVEMENT FOR CHAGA'S.Kuitenganisha CDM na udini.ukanda na uchaga ni sawa sawa na kutenganisha ulimi na kinywa.
Una matatizo ya kudhani utatawala milele. hata mseme nini wananchi wanitaka CDM 2015 inatia timu ikulu.
 
Jambo analo lisema mh.Mbowe ni lazima lichukuliwe kwa tahadhari kubwa,la sivyo linaweza kusababisha tatizo la ukanda/ukabila katika nchi.
 
Una matatizo ya kudhani utatawala milele. hata mseme nini wananchi wanitaka CDM 2015 inatia timu ikulu.

Haiwezekani Almasi imechimbwa Mwadui toka mkoloni lakini wakazi wa utemini waliokutwa na Wiliamson wakicheza bao kwa kutumia almasi wanaishi kwenye nyumba za tembe. Inauma sana.
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.

Inawezekana huelewi kile unacho kisema au hukumwelewa Mbowe, mim sitokei huko na wala siko huko kaskazini but hivi kwanini maeneo yenye madini, wilaya husika huwa zinatakiwa kupewa USD 200,000/= Kwa mlima Kilimanjoro kinachosumbua hapo ni nini? To me Mbowe is right, sema tu issue imetolewa na mpinzani, mbaya zaidi ni mkazi wa huko, lakini hili angeweza kulisema mtu yeyote tu!
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.
Mbona gharama za kuunganisha umeme huko Mtwara na Lindi zimeshushwa kuliko maeneo mengine ya Tanzania?.
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.

hapo umenena vyema.
Hivi kila mtu akisema afaidike na kilichopo eneo lake tutafika kweli?

Hapo ndo alipoonyesha udhaifu wake.
Au anasema kwavile kilimanjaro ndo kwao?

Watu wa mwanza wangekataa maji za ziwa viktoria yasipelekwe shinyanga, singida na dodoma.
Tungefika kweli?
 
Ni wakati muafaka kumuuliza Mbowe ni Tanzania ipi anayoizungumzia kuipatia ukombozi? au M4C= MOVEMENT FOR CHAGA'S.Kuitenganisha CDM na udini.ukanda na uchaga ni sawa sawa na kutenganisha ulimi na kinywa.

Kuwafaidisha watu walio kwenye eneo husika halipingiki, sidhani kama mbowe anasema pesa yote ibakh hapo, lakini kwa kweli ni muhimu watu waone faida ya raslimali zilizo eneo lao ndipo zingine zigawiwe kwa wengine, yaani gesi itoke mtwara kuja dar af wao wakae gizani, this is absolute nonsence!
hatahivyo kwa heshima kabisa naomba unisaidie hivi udini wa chadema mnaupima kwa vigezo gani?
 
Mimi CDM lakini hapo Mbowe amechemka! rasilimali ziwanufaishe watanzania wote bila kujali ukanda au sehemu inayotoka rasilimali hizo.Next time asirudie ujinga huo.Slaa for presidency 2015.

kama kwenu hakuna rasilimali tulia. Unajua hali za watu wa pale zilivyo? na unajua maana ya mrabaha? Wa kilimanjaro wanahitaji mgao zaidi kutokana na mlima!
 
kama kwenu hakuna rasilimali tulia. Unajua hali za watu wa pale zilivyo? na unajua maana ya mrabaha? Wa kilimanjaro wanahitaji mgao zaidi kutokana na mlima!

Ndugu yangu acha kuwa na akili za mgando! kila mkoa ukisema ufaidike na rasilimali zake ndio mwanzo wa kujitenga na umoja wetu utakuwa shakani.Ukweli ni huo mbowe kachemka na hiyo loop hole itatumiwa na magamba.
 
Ili huu mlima wananchi waweze kuuenzi lazima wanufaike na sehemu ya pato lake, Sio lazima billion zote ziachwe hapo kwa wachagga.
 
Back
Top Bottom