CHADEMA Katavi yasema inaunga mkono kauli ya Mbowe ya kuandamana Januari 24

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Katavi kimejipanga kutekeleza kufanya maandamano ya amani yanayotarajiwa kufanyika Januari 24, 2024.

Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Katavi, Roda Kunchela ameyasema hayo akiwa katika ofisi ya chama hicho mkoani humo ambapo amesema agiza la Mwenyekiti Taifa, Freeman Mbowe la kufanya maandamano ya amani nchi zima ni tamko la Kikatiba katika mstakabali wa kudai haki ya maoni ya Wananchi.

Roda amewaomba Wananchi wa Katavi kushiriki ipasavyo katika maandamano ya amani yatakayofanyika tarehe Januari 24, 2024.

Elizabeth Kasela ni Mwenyekiti wa Baraza la Vijana katika Chama hicho Mkoa wa Katavi amewaomba vijana kujitokeza katika kutekeleza maandamano ya amani huku Wanawake na wazee wakiombwa kujitokeza siku ya maandamano ya amani.
 
Mimi siungi mkono ila naomba nipewe kitengo cha usalama pale police kuna kitu nahitaji kukisimamia hiyo siku
 
JamiiForums753274111.jpeg
 
Back
Top Bottom