Andrew Chenge: Kwangu gamba limeishia kiunoni tu

DEKA

Member
Apr 11, 2011
14
2
Wednesday, 27 April 2011 21:59



Ramadhan Semtawa
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.Kauli hiyo ya kwanza ya Chenge inakuja kipindi ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekuwa akitangaza kwa nguvu mpango mkakati wa chama hicho kujivua gamba. Makada wa chama hicho wanaotakiwa kupima nafasi zao na uzito wa tuhuma zinazowakabili ni wale wanaohusishwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za Richmond, Kagoda na wizi wa EPA.

Source: Mwananchi.

Kaazi kweli kweli, kumbe hata mafisadi hawajijui kama ni mafisadi, kazi ipo Tanzani. Ninani atakaye simama na kusema jamani natubu na ufisadi na uhacha? Kila mtu anajihesabu ni masafi. Labda ndo maana hata mkulu nae kajisahau, anataka mafisadi watoke ktk chama na yeye sijui atakuwa nani tena. Ni utata kweli.
 
Wednesday, 27 April 2011
Ramadhan Semtawa

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.

Kauli hiyo ya kwanza ya Chenge inakuja kipindi ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekuwa akitangaza kwa nguvu mpango mkakati wa chama hicho kujivua gamba.

Makada wa chama hicho wanaotakiwa kupima nafasi zao na uzito wa tuhuma zinazowakabili ni wale wanaohusishwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za Richmond, Kagoda na wizi wa EPA.

Hata hivyo, Chenge jana alipoulizwa na gazeti hili kuhusu kutajwa kwake kuwa mmoja wa wanachama wanaotakiwa kupima uzito wa tuhuma zinazowakabili na kujiondoa wenyewe ikiwa ni hatua ya chama hicho kujisafisha kwa kujivua gamba, alisema: "Sijui hicho kitu. Naheshimu vikao na taratibu za chama hilo ni jambo la chama si la vyombo vya habari."

Alisema chama kina taratibu zake za kiutendaji na kuongeza: "Siwezi kuanza kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu mambo ambayo yana taratibu zake ndani ya chama."


Alisema kamwe hatakiuka taratibu za chama na kwamba uamuzi wote utakaofanyika au kutolewa huwa unafuata vikao vya chama.

Alipoulizwa juu ya kusubiri kwake taratibu za chama wakati tayari jambo hilo linafahamika kwa umma alijibu: "Kwa ‘public' ipi wewe? Mimi sijui hilo jambo, nasubiri taratibu za chama na siwezi kuzungumza zaidi nje ya chama."


Akizungumzia utekelezaji wa maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama hicho (NEC-CCM), Nnauye alisema taratibu zimekuwa zikiendelea na kuwataka wananchi kuwa na subira.Juzi, Nnauye alikaririwa akisema kwamba taratibu hizo zingefanyika baada ya Sikukuu ya Pasaka na kusisitiza: "Ambacho nimekuwa nikikisema kiko palepale."


Mapema mwezi huu, NEC-CCM ilitoa muda wa siku 90 kwa watuhumiwa wote wa kashfa mbalimbali ndani ya chama hicho kujipima wenyewe na kujiondoa kwenye nafasi hizo vinginevyo, chama kingewang'oa kwa nguvu. Azimio hilo limekuwa likitangazwa kwa nguvu katika mikutano mbalimbali ya hadhara ikiwa ni mkakati wa chama hicho kurejesha imani chama kwa wananchi ambayo imeanza kupotea kutokana na tuhuma za ufisadi.


Juzi, Nnauye akizungumza na Shirika la Utangazaji la Taifa (TBC Taifa), alisema chama hicho hakitishiki na uwezekano wa makada hao kuhamia upinzani.


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, akihutubia sherehe za kuzaliwa chama hicho Februari 5, mwaka huu alitangaza mkakati huo wa chama kujivua gamba na kurejea katika misingi ya maadili ya uongozi iliyorithi kutoka Tanu na CCM ya nyuma.


Sekretarieti ya CCM kukutana kesho

Katika hatua nyingine Sekretarieti ya CCM inatarajiwa kukutana kesho kujadili pamoja na mambo mengine, utekelezaji wa maazimio ya NEC-CCM.

Kwa mujibu wa duru za kisiasa kutoka CCM, mkutano huo utajadili ajenda hiyo kwa kufanya tathmini ya azimio hilo na namna ya utekelezaji wake.

Alipoulizwa jana, Nnauye alithibitisha kufanyika kwa mkutano huo lakini alisema ni kikao cha utendaji cha kawaida.Kwa mujibu wa Nnauye, kikao kama hicho kiliwahi kufanyika Mjini Dodoma baada ya kuundwa kwa sekretarieti hiyo na pia tayari ilikwishakutana Dar es Salaam.


Alisema kikao hicho si maalumu wala cha dharura na kwamba hufanyika mara moja kwa wiki.


"Siyo kikao cha dharura wala kikao maalumu, ni sehemu tu ya utendaji wa sekretarieti. Tunafanya vikao kama hivi mara moja kwa wiki, kwa hiyo hakuna kikao maalumu," alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Hivi nyoka akivua gamba siyo kuwa ndio anakuwa hatari zaidi? au akivua gamba anabadilkika kuwa chura?
 
Nnape analoloma tu lakini anajua kuwa kuwang'oa hao mapacha watatu
siyo zoezi rahisi. Yetu macho!
 
ni jana tu tulipata breaking news toka CC headquaters kwamba barua za hawa mabwana haziandikiki, na cheki majibu yake jamaa, anajiamini kupita maelezo. Lets wait n c, hapo bado EL.
 
hakunalka maana litafanyika hapa ...labda awe mtu mwingine sio JK
 
Chenge kaanza anasikilizia upepo Lowassa akija yaan CCM watajutia kutaka kuwatosa wakati wote ni magamba

Chenge usikubali kudhalilika afta all years ya kuwa kibaraka wa CCM
 
NAPE anacheza ngoma asiyeijuwa vema ...kwa watu wanaojua vema kupanga strategies watakuwa wanamshangaa...vita hii ilitakiwa kupiganwa kimya kimya.....kwani kwa kuongea sana ,tayri anawajengea mapacha watatu GAMBA LA KOBE amabalo kulivua hadi kobe afe.....

Wewe fikiria kelele za NAPE tayari zimesababisha wananchi wa ARUSHA ,mONDOLI ,MTO WA MBU..Na sehemu nyingine na maeneo ya wamasai ...watake kuandamana wiki iliyopita kwenda CCM arusha ..na wengine kutaka kutuma ujumbe kwenda kwa rais IKULU .....Kumtetea Lowassa..yote hii inatokana na makelele ya NAPE..kama angekuwa kimiya kama wenzake isingeamsha hisia za wananchi wanaowapenda hao wanaowaita magamba....hii vita wameshashindwa na wakilazimisha kuipigana basi wajiandae na madhara makubwa zaidi ya ilivyotarajiwa .....yote hii ni kwa ajili ya PAPARA!!

...Rais anaaibika kwa mara nyingine tena!
 
Chenge yuko sahihi sana. Kama yeye ni gamba, kati ya viongozi wa CCM nani asiye GAMBA? Nadhani anatumia ule msemo usemao kabla ya kutoa KIBANZI ndani ya jicho la mwenzio, utoe kwanza BORITI ndani ya jicho lako. Kwa nafasi alizokuwa nazo ndani ya chama na serikali zake, sijui nani atakayesimama!
 
Nchi hii imejaa usanii kweli kweli, ebu jamani someni hii:

MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.

Hivi huyu Bw hakuwepo kwenye hicho kikao?

Hivi hiki chama kinafikiri Watz wote hamnazo, kwa nini mwenyeketi hakutangaza mara moja kuvuliwa nafasi za haya magamba mpaka magamba yasubiri barua kutoka ndani ya chama na yeye ameshiriki maamuzi ya hicho kikao.

Kumbe haya Magamba yanajua mwenyekiti na sekretariati yake hawana uwezo wa kuandika hiyo barua ndo maana gamba moja limeamua kuongea kwa kejeli -soma hiyo bold hapo juu.
 
Ni kawaida yake kujitoa akili huyo hata mwanzo alipoulizwa fedha zetu zilizopo New Jersey alisema hajui kama ana mahela huko na alipobanwa sana akaseama kumbe watu wanazungumzia vijisenti vyake

RA alipoulizwaga kuhusu DOWANS aliikana sana na kusema ingekuwa fahari kubwa kwake kuwekeza katika nishati ya umeme kulikomboa taifa lake baada e kumbe bdiye mmiliki kwa hiyo ni kawaida yao hao kujitoa fahamu nakutufanya sisi wajinga muda wote
 
Back
Top Bottom