Andrew Chenge: Kwangu gamba limeishia kiunoni tu

Je gamba lipi ambalo linaanzia kichwani mpaka kiunoni ambalo vijisenti kalivua na hilo la kiunono mpaka mkiani ni lipi na kwanini hataki kulivua mpaka litumike shoka tujadili hapa.
 
WanaJF,moja kati ya mambo yanayoitesa CCM leo ni dhana ya kujivua gamba.Nimeshawishika kuwasilisha topic hii baada ya kufikiri sana na nikaona mambo makubwa matatu.
MOJA-Ni namna falsafa ya kujivua gamba ilivyopokelewa ndani na nje ya CCM.Inawezekana mwenyekiti alikuwa na nia njema sana lakini mtu ni yeye na dhamira yake
MBILI-Katibu wa Itikadi na uenezi alipata hisia kwamba walengwa wa falsafa hiyo ni E.Lowasa,A.Chenge na R.Aziz ndio maana alianza kusemasema huku na kule,Hatimae Rostam kuamua kuachia ngazi.Lakini Chenge akasema hajijui kama yeye ni gamba ndani CCM.Huku Lowasa akiitisha mkutano na waandishi akasema HATOVUMILIA KUCHAFULIWA KWENYE VYOMBO VYA HABARI.
TATU-CCM imekuwa rahisi kumvua gamba Rostam kwa kuwa hakuwa kwenye system ya serikali,yeye ni mfanyabiashara wa kimataifa.Lowasa-waziri mkuu mstaafu.Hivi kweli CCM wanaweza leo kumng'oa eti ni gamba? Chenge-mwanasheria mkuu wa serikali mstaafu,kweli leo ni Gamba?Sina hakika kama watawatosa,kazi kwenu tafakarini.
 
Mwizi hawezi kujitangaza kwamba yeye ni mwizi, unless amekata shauri la kuokoka!
 
Alikuwa na wadhifa gani serikalini?
kinachojaalisha ni influency yako kwa chama na serikali sio madaraka yako . Lowasa na Chenge hana madaraka serikalini kwa sasa lakini kutokana na pesa zao na uwezo wao wa kuwahonga wajumbe wa vikao mbalimbali na vya chama hata Kikwete anawaogopa! Same applie to RA, MO dewji,
Karamagi . Isitoshe wana ubia kwenye Uraisi wa Kikwete maana mtandao wao ndo umemuweka pale
 
Tumetoka mbali

Mkuu,unaujua huwa hatumuelewi chenge.huwa akiongea tuna Cheka na kumkebehi! Ila kama tukijadili kauli zake in deep, utaona Kuna Kitu kikubwa amemaanisha! Alisema yeye Ana vijisenti,tukaona anatukebehi wa Tz, la hasha hakutukebehi! jamaa inawezekana Kuna wenzake Wameshakula Mara hamsini ya alizonazo Change! Sasa ni kina Nani Hao!? kazi inaanzia hapo.Hapa amesema gamba lake lipo nusu mlingoti! labda anamaanisha Kuna magamba yapo chini ya kapeti, ambayo yapo mwili mzima na hayagusiki,inawezekana kuwa Change huwa anakuwa mtu wa kati,kazi yake yeye ni kucheza na sheria anakula chake, ILA WENYE DILI WAPO!
 
'Hekima hukaa ktk moyo wa mtu mwenye ufahamu' Chenge hana hekima kwani hana ufahamu wakiwepo viongozi wengi wa CCM.
 
Chenge ukipona tena safari hii basi uache wizi kabisaa na mrudie mungu wanko uchawi ww, wizi wewe sio maisha hayo mzee, keko wanakusunilia kwa hamu sn
 
Back
Top Bottom