CCM wakimpitisha Chenge kuwania Uspika, nitaamini kuwa Watanzania hatuko serious

The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
15,397
12,981
Kuna minong'ono kwenye jukwaa letu kuwa jina Mtemi Chenge ndilo liko likely kupendekezwa na chama. Kama hii itatokea kwa kweli nitaamini kuwa kama Taifa hatuko serious. Change ana tuhuma kadhaa huko nyuma za ubadhirifu na ufisadi. Ilifikia mpaka kwa kiburi najeuri kudai wazi wazi kuwa zile pesa zinazosemekana kuwa kwenye account yake huko visiwa vya Jersey kuwa ni visenti tu.

Ingawa hajawahi kuchunguzwa au kuwa convicted kwa tuhuma lakini kitendo cha yeye kusema hivyo ni dhahiri kuwa alikubaliana kuwa ana pesa huko nje lakini hakuja wazi clean kuwa alizipataje. Hakuwahi kutuonyesha kama Taifa yeye kama mtumishi wa serikali tena wakati ule wa mishahara njiwa, yeye alizipataje pesa zote hizo mpaka za kufungua account kwenye bank za Matajiri nje ya nchi!?

Kana kwmba haitoshi, huyu Mtemi Chenge alikuwa involvolved kwenye kesi ya Capable homicide ambapo alipata ajali usiku wa manane akitoka ulevini na mtu akafa. Ingawa alishinda kesi, bado wenye akili zetu hii kesi ilituachia maswali mengi. Ukichukulia kwamba huko nyuma yeye alishawahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa miaka 10. Hivyo kuna possibility kubwa kuwa inawezekana alitumia connections zake kujisafisha.

Binafsi simchukii Chenge kama watu wanavyoweza kutafsiri na inawezekana pia Chenge anatafuta nafasi ya kujisafisha lakini kama Taifa ni wakati wa kutumia akili mpya na kuachana na hawa walioshindwa kutufanyia lolote kama taifa walipopata nafasi na badala yake wamekuwa ni mifano mibaya kwa kizazi chetu. Kama Rais kawaondoa akina Kabudi na Lukuvi kwa kudai ni Wazee, why bring Chenge back wakati yeye ni mzee zaidi ya hao aliowaondoa kwenye Uwaziri.

Wanasilisha
 
Kuna minong'ono kwenye jukwaa letu kuwa jina Mtemi Chenge ndilo liko likely kupendekezwa na chama. Kama hii itatokea kwa kweli nitaamini kuwa kama Taifa hatuko serious. Change ana tuhuma kadhaa huko nyuma za ubadhirifu na ufisadi...
Sasa kwenye yale matakataka yaliyochukua fomu wakimwacha Mtemi Chenge watampa nani? Tulia au Msama?
 
Kama Chadema walimpitisha Lowassa kumpa nafasi ya kugombea urais na watanzania hao hao wakampigia kura ndio uje kuwashangaa watanzania endapo ccm watampitisha Chenge? Hilo mbona dogo tu kwa watanzania.
Kwa maana hiyo unataka kutuambia kuwa Chadema ndiyo yard stick ya siasa za Tanzania au unamaanisha nini ...!!?
 
Kwa maana hiyo unataka kutuambia kuwa Chadema ndiyo yard stick ya siasa za Tanzania au unamaanisha nini ...!!?
Point yangu ni kwamba watanzania hawanaga userious,hilo la chadema na Lowasa ni mfano tu kuonesha watanzania ni watu wa aina gani.
 
Lini watanzania tulishawahi kujitambua,maana tuliaminishwa kwamba Tanzania ndiyo CCM.
 
Hata mimi nashangaa, mtu ana matuhuma lukuki za ufisadi lakini bado watu wanampendekeza. Tz is going down b'coz of ccm
 
Lini watanzania tulishawahi kujitambua,maana tuliaminishwa kwamba CCM ndiyo Tanzania ,uzuri kwa Sasa Hakuna kisingizia Chadema kuwa ndiyo wanaleya mfumuko wa bei wa kutuchelewesha kupata maendeleo.
 
Back
Top Bottom