Dr Alfonsi
Member
- Jun 16, 2023
- 34
- 70
Mheshimiwa Rais wa JMT,
Pamoja kuwa upo busy na majukumu yako lakini ikikupendeza basi naomba usome huu ujumbe wangu pasipo kuchoka, na kama kuna wasaidizi wako basi itakuwa ni vema endapo watakufikishia ujumbe huu.
Taifa lolote lile duniani ili lifanikiwe linahitaji kuwa na watu ambao ni committed na wenye nia na ari ya kutaka kuitumikia au kuijenga nchi yao, huku wakitanguliza uzalendo kwa nchi yao na serikali yao.
Mwezi January, 2022 walijitokeza watanzania wasio pungua 70 kuomba ridhaa ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ili waweze kupitishwa na chama hicho kugombea nafasi ya SPIKA wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Watu hao pamoja na kuwa na UJASIRI wa kutaka kuongoza mhimili wa dola (Bunge la nchi hii), naamini wazi kabisa wana uwezo wa kulitumia taifa letu kwa weledi na kuwaletea manufaa watanzania wenzao na kulinda maslahi mapana ya nchi hii.
Mh. Rais, kama hukupata fursa ya kuona majina basi nitakuwekea hapo chini. Lakini ninachopenda kukumbusha ni kwamba hawa ni wana CCM kindakindaki na wanapenda kuitumikia nchi yao kwa maslahi mapana ya taifa letu.
Walio wengi kati yao (90%) ni waajiriwa katika serikali yako na pia ni wasomi wenye taaluma mbalimbali. Mh. Rais, nikukumbushe kuwa hawa wana CCM walikuwa radhi kujitoa kwa vipato vyao vidogo (Milioni moja) ili kupata fomu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ili wapate ridhaa ya kuisimamia serikali katika mhimili wa Bunge, lakini vikao vya maamuzi ya juu ya Chama waliridhia kwa kauli moja kuwa Dr. Tulia Ackson atosha kukiwakilisha chama. Baada ya zoezi hilo kwisha, je Mh. Rais (M/KITI wa CCM):
Mh. Rais, hapa chini nakuwekea orodha ya majina ya hao wana CCM kindakindaki waliojitokeza kukipigania chama hadi kufikia hatua ya kuomba ridhaa ya kutaka kuongoza Bunge la Tanzania.
Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu January 2022 ni hawa wafuatao :
Cc.
Pia Soma:
- Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika

- Umepata nafasi ya kuona CV za hao wagombea wengine?
- Umewahi kuwaza kuhusu potentiality ya hawa wagombea wengine kuwa wanaweza kukusaidia katika kutekeleza majukumu ya serikali yako?
- Umewahi kufikiri au kuwaza kuwa asilimia 90 ya hao wana CCM ni wasomi na ni hazina ya Chama na hivyo kuweza kuwatumia katika nafasi nyinginezo nyeti na muhimu ili kuliletea tija taifa letu?
Mh. Rais, hapa chini nakuwekea orodha ya majina ya hao wana CCM kindakindaki waliojitokeza kukipigania chama hadi kufikia hatua ya kuomba ridhaa ya kutaka kuongoza Bunge la Tanzania.
Wanachama wa CCM wanaotia nia kugombea nafasi ya uspika baada ya Spika Job Y Ndugai kujiuzulu January 2022 ni hawa wafuatao :
- Andrew Chenge : mwanasheria mkuu wa serikali wa zamani
- Sophia Mathayo Simba : Waziri wa zamani wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Utawala Bora), ni Mwenyekiti wa zamani Umoja wa Wanawake Tanzania UWT
- Dr. Mussa Shafii Ngonyani
- Wakili Faraji Rushagama
- Rahmaddin Rashid Ismaili - mwanafunzi UDSM
- Hamisi Rajabu
- Festo John Kipate
- George Francis Nangale : Mbunge wa zamani Bunge la EALA
- Barua Abdi Mwakilanga : mwanadiplomasia toka Buguruni DSM.
- Zahoro Rashid Hanuna : Afisa Biashara Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
- Thomas David Kirimbunyo
- Angelina Bello John
- Eng. Abdulaziz Jahad Hussein
- Dr. Tulia Ackson : Naibu spika chini ya Job Ndugai
- Dr. Thomas Kashililah : katibu wa bunge wa zamani
- Stephen Masele : naibu spika wa zamani Bunge la Afrika
- Mussa Azzan Zungu : meya wa zamani wa Ilala Dsm.
- Joseph Musukuma :
- Ezekiel Maige : waziri wa zamani
- Asia Juma Abdallah : mkuu wa wilaya wa zamani
- Dr. Titus M. Kamani : waziri wa zamani
- Tumsifu Mwasamale : Afisa Maendeleo ya vijana mkoa wa Dodoma
- Prof. Handley Mpoki Mafwenga : mtumishi wa serikali / umma
- Goodluck Mlinga : mbunge wa zamani wa CCM
- Prof. Norman Adamson Sigala : mwanasiasa toka jimbo la Makete, msomi mhadhiri
- Hatibu Madata Mjega :
- Dr. Linda Salekwa Ole Saitabau : mhadhiri chuo Kikuu cha Teknolojia Mbeya na mtafiti wa magonjwa yanayoambukiza na chanjo
- Emmanuel Simon Sindama
- Bi. Uwesu Msumi
- Hilal H. Seif
- Wakili Emmanuel Paul Mngare
- Athumani Mfutakamba
- Wakili Nduruma Majembe
- Mwemba Burton Mwemba : marketing expert and media presenter / msanii Mwijaku
- Henry Erasto Kessy
- Josephat Malima
- Adam Nyanyavanu
- Eng. Stella Manyanya: mkuu wa mkoa wa zamani
- Andrew Kevella
- Luhanga Mpina
- Hussein Migoda Mattaka
- Dr. Godwin Maimu : expert in CAPACITY BUILDING AND MICROFINANCE SERVICES
- Mohammed Ali Mmanga : mgombea ubunge wa zamani
- Esther Stefano Makazi : Kada wa CCM
- Comrade Amos Sollo : Mwanafunzi Chuo Cha Elimu ya Juu
- Godwin Kunambi - mkurugenzi wa zamani wa jiji la Dodoma
- Goodluck ole Medeye
- Juma Hamza Chumu
- Baraka Omary Byabato
- Hamidu Chamani : kada wa chama, Mtaalam mbobezi wa masuala ya kodi
- Fikiri Saidi : mkuu wa wilaya wa zamani
- Bi. Dotto Balele Mgasa
- Wakili Onyango Otieno
- Eng. Samuel Hayuma
- Merkion Ndofi
- Abwene Majula
- Patrick Nkandi
- Dr. Edison Wazoel Lubua : Doctor of Philosophy (PhD)Information Systems & Technology
- Alex Msama
- Samwel Magero : mjumbe wa Kamati kuu Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA),
- Peter Mjemu : mgombea nafasi ya Ubunge Jimbo la Chato mwaka 2020
- ....
Cc.
- Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Aione kwenye jalada).
- Katibu Mkuu Kiongozi (Aione kwenye jalada kwa utekelezaji)
- Katibu Mkuu wa CCM (Aione kwenye jalada kwa utekelezaji)
- Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa (TISS) - Aione kwenye jalada kwa utekelezaji - VETTING).
- Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais (kumfikishia hard copy - Mh. Rais ujumbe huu ili ausome).
Pia Soma:
- Majina ya wanaCCM waliochukua fomu za Uspika