Andrew Chenge: Kwangu gamba limeishia kiunoni tu

Hivi kuwa fisadi tanzania ni kosa chini ya sheria ipi?, na kama ipo nani anatakiwa kuisimamia na kuwashtaki mafisadi? Hamuoni kuwa huyo ndio fisadi mkubwa? Mi nadhani kumwita mtu fisadi huku hashtakiwi na we mwenyewe ndio jukumu lako la kuchukua hatua ni kutomtendea haki! Kama hawana makosa muwaache na kama wana makosa chukueni hatua! CHENGE USIONDOKE CCM MPAKA WATHIBITISHE WEWE NI FISADI GAMBA!, TENA IKIBIDI WASHTAKI WAACHE KUKUDHARIRISHA!
 
kwakweli cjui Tanzania inaelekea wapi,ccm mwishiwe itajivua na ngozi kabisa! :A S 39:
 
Hajui kama yeye NI Gamba au hajui kama yeye NDIYE Gamba?!!!
Hata mi siamini kama Chenge (na wenzake wawili), NDIYE Gamba... Anaweza kuwa Gamba ndiyo (kwa maana ya fisadi), lakini siamini kama ndiye anayeidumaza CCM. Tusubiri akishajivua tuone kama CCM itasafishika machoni mwa Watanzania.
 
nnape AKIKULIMA BARUA UTAJUA TU

Hana jeuri hiyo.
Kama walitaka kuwashughulikia walipaswa wawambie pale pale kwenye kikao na wachukue hatua pale pale. Haya ya kuandikiana barua hayatawezekana. Ebu tafakari barua hiyo itasemaje (contents) - kwamba fulani wa fulani umefukuzwa kwenye nafasi zote za uongozi katika ccm kwa kuwa unatuhumiwa kwa ufisadi wa EPA?
Huyo mtu akifungua kesi ya kashfa si ccm yote itafilisika. Na katika kesi kama hiyo itabidi ccm ndiyo idhibitishe ufisadi naye huyu atatoa ushahidi kuwa fedha hizo zilitumiwa na ccm?
 
kawaida ya mwizi hata ukimkamata huwa hakubali kama ameiba atasita kukubali, kwahiyo namshaa huyo aliyepoteza muda wa kuhoji fisadi sijui alitegemea jibu lipi tofauti na gamba kukataa kama yeye siyo gamba
 
Nyoka anatakiwa kukatwa kichwa, ndipo usalama utakuwepo. Usimwamini aliyejivua gamba!

Nyoka akijivua gamba ndiyo sumu inaongezeka. Nadhani ccm ingewatendea haki wananchi kama kwa kauli moja ingeamua kukivunja hicho chama na kuunda chama kipya hapo ndiyo tutaelewa kuwa wamejivua gamba
 
Wednesday, 27 April 2011 21:59



Ramadhan Semtawa
MBUNGE wa Bariadi Magharibi, Andrew Chenge amesema anasubiri taratibu za Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuona kama atapewa barua ya kumtaka ajivue nafasi zake za uongozi kwani hadi hivi sasa hajui kitu hicho.Kauli hiyo ya kwanza ya Chenge inakuja kipindi ambacho Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amekuwa akitangaza kwa nguvu mpango mkakati wa chama hicho kujivua gamba. Makada wa chama hicho wanaotakiwa kupima nafasi zao na uzito wa tuhuma zinazowakabili ni wale wanaohusishwa na kashfa mbalimbali zikiwamo za Richmond, Kagoda na wizi wa EPA.

Source: Mwananchi.

Kaazi kweli kweli, kumbe hata mafisadi hawajijui kama ni mafisadi, kazi ipo Tanzani. Ninani atakaye simama na kusema jamani natubu na ufisadi na uhacha? Kila mtu anajihesabu ni masafi. Labda ndo maana hata mkulu nae kajisahau, anataka mafisadi watoke ktk chama na yeye sijui atakuwa nani tena. Ni utata kweli.

hahahahahahahaahhahhahaha. Chenge amesema ukweli maana ni wachache wanaojua weaknesses zao.
 
Hivi nyoka akivua gamba siyo kuwa ndio anakuwa hatari zaidi? au akivua gamba anabadilkika kuwa chura?

hahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahahah:smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big::smile-big:
 
Jakaya Mrisho Kikwete amerikoroga kama ambavyo niliwahi kusema hapo awali. Alianza kwa kutumia UVCCM kupanga mkakati wa kuwatosa hao Mapacha watatu na hawakuwa hao tuu, alikuwemo Sumaye na Malecela.

Baada ya kupima upepo wakaona walikuwa hawapati support kutoka kwa wananchi na baadhi ya wanachama kutoswa kwa Sumaye na Malecela, kwa hiyo akapanga na sekretariati ambayo wote ni maswahiba wake wa karibu.

Mkuchika walikuwa wote chuo kikuu na baadaye jeshini
Chiligati walikuwa wote chuo kikuu na baadaye jeshini
Makamba walikuwa wote Singida, Kikwete alivyoanza kazi Tanu. Alitaka kumtosa Makamba papo akashindwa baada ya Makamba kumuendea ofisini kwake kulia na kugaragara miguuni kwake mpaka JK, akashindwa kuamua akisema hajawahi kuliliwa na mtu
mzima kama Makamba

Msekwa ni mentor wa Jakaya katika safari yake ya kisiasa
Meghji walikuwa wote chuo kikuu lakini urafiki umekuwa kama ndugu wa damu.

Hawa wote Jakaya angeweza kuwaeleza kinachomtatiza na pia kuwaomba wamsaidie akoe chama kwa wao kusacrifice nafasi zao na wao kwa uaminifu wao kwake wakakubali kucheza naye mchezo wa kiduku kudanganya wananchi kumbuka.

Makamba mara nyingi akiongea na vyombo vya habari alishatubatiza wananchi kwamba ni wasaharifu na tusiofuatilia mambo kwa hiyo walikuwa na uhakika kwamba hatutajua kwamba huo ni mchoro ulioshorwa kutughiribu.

Kwa Mahesabu mafupi ya CCM na UWT waliamua kuwatosa Mapacha watatu lakini sasa wakiangalia response ya wanachama wao na wananchi nyingine kwa kutaka Gamba lianze kuvuliwa na Mwenyekiti wa CCM-Jakaya KIkwete hapo ndio equation isipofanya kazi.

Na wameshakamatika na ukweli kifo chao ndio hiki,manake baada ya siku 90 kuisha bila Mafisadi wote kujivua magamba akiwemo mwenyekiti wa CCM wananchi tutawalazimisha wayavue kwa njia yeyote.
 
Mmoja wa wanaotakiwa na CCM kujivua gamba (kuondoka ndani ya chama) kwa madai ya ufisadi amelieleza mwanahalisi kuwa "kwangu gamba limeishia kiunoni,kuliondoa hapa lilipo sharti uje na shoka"Chenge alikuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti la mwanahalisi lililotaka kufahamu ni lini ataondoka katika uongozi wa chama chake kutokana na kutuhumiwa na ufisadi.

Nape Upo hapo?
 
Mmoja wa wanaotakiwa na CCM kujivua gamba (kuondoka ndani ya chama) kwa madai ya ufisadi amelieleza mwanahalisi kuwa "kwangu gamba limeishia kiunoni,kuliondoa hapa lilipo sharti uje na shoka"Chenge alikuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti la mwanahalisi lililotaka kufahamu ni lini ataondoka katika uongozi wa chama chake kutokana na kutuhumiwa na ufisadi.

Nape Upo hapo?


Amekata mzizi wa fitina hapo. Hilo jibu ni zito mno
 
Mmoja wa wanaotakiwa na CCM kujivua gamba (kuondoka ndani ya chama) kwa madai ya ufisadi amelieleza mwanahalisi kuwa "kwangu gamba limeishia kiunoni,kuliondoa hapa lilipo sharti uje na shoka"Chenge alikuwa akijibu swali la mwandishi wa gazeti la mwanahalisi lililotaka kufahamu ni lini ataondoka katika uongozi wa chama chake kutokana na kutuhumiwa na ufisadi.

Tatizo ni kuwa shoka linaweza likatoa kiwiliwili chote na gamba likafia hapo bila kutoka. Pia anaweza akakosekana mwenye guts la kunyanyua shoka kutoa hilo gamba!!!
 
Jeuri na kiburi cha chenge,.............nani alaumiwe?
 
".........kwangu Gamba limeishia kiunoni kuliondoa hapa lilipo inabidi uje na Shoka"-Source Mwanahalisi la Leo kwenye Story ya JK KIGEUGEU
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom