Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

thank god. Alikuwa amepata shock ya ajali na sasa amezinduka. Madaktari wametuondoa hofu kuwa hana majeraha makubwa. Wanasubiri vipimo kufanya uchunguzi zaidi kabla hawajamruhusu kutoka.

bwana amuwekeee mikono ya wakovu apone haraka. Bwan yu nae na sisi tuko nae
 
Wapinga ufisadi wote hawapaswi kupata ajali, kuugua, kuandikwa vibaya, kukosolewa,.... na ikitokea hayo mabalaa yakawakuta, mafisadi waandamwe, walaaniwe,...Hebu tukuekue kidogo WATANZANIA wenzangu.
Hivi na wewe ukifa leo kwa bahati/bahati mbaya nani atajua?
 
LATEST: Mpiganaji Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa Dar kwa charter plane mchana huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kidaktari. Kwa sasa anaendelea vizuri Wadi No 5 katika hospitali ya mkoa Iringa. Dereva wake ni mzima kabisa, na yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa sasa, hapo hapo hospitali. Anahojiwa kutokana na kudanganya hapo awali kuwa gari yake iligongwa kwa nyuma. Mtu aliyeenda eneo la ajali na baadaye hospitali anasema gari ya Dr Mwakyembe aina ya Landcruiser ilikuwa ina-overtake malori mawili na ghafla dereva alishtukia shimo kubwa mbele yake akapoteza control na gari ikapinduka ikiwa pia imegonga mti mkubwa na kuuong'oa.
 
Aisee tumwombee vilevile make ni mpginaji hasa na wanguvu sana, natumaini Mungu atamjalia apone haraka.Lakini wachunguze pia chanzo cha ajali, hawa madreva wetu sio wakuamini asilimia 100.
 
Duh pole nyingi sana kwa Dr na dereva wa gari lake.... Mola atawasaidia mtapata nafuu na kurudi katika majukumu. Wanafamilia wote muuguze salama!!
 
kutokana na jambo ili nimejifunza mambo mengi sana hapa.kumbe JF karibu member wote ni wacha Mungu kiasi hiki? mmh!
 
E Mungu tunaomba umponye ndg yetu Dr MWAKYEMBE,ambaye taifa letu bado linahitji mchango wake.
 
kutokana na jambo ili nimejifunza mambo mengi sana hapa.kumbe JF karibu member wote ni wacha Mungu kiasi hiki? mmh!

hujatembea humu ndani vizuri wewe. kuna madushu mpaka basi. Mungu ana muda wake humu
 
Jamani, taarifa zinazsma kuw Mwakyembe anahamishishwa kutoka iringa analetwa Dar leo hii
 
LATEST: Mpiganaji Dk Harrison Mwakyembe atapelekwa Dar kwa charter plane mchana huu kwa ajili ya uchunguzi zaidi wa kidaktari. Kwa sasa anaendelea vizuri Wadi No 5 katika hospitali ya mkoa Iringa. Dereva wake ni mzima kabisa, na yuko chini ya ulinzi wa polisi kwa sasa, hapo hapo hospitali. Anahojiwa kutokana na kudanganya hapo awali kuwa gari yake iligongwa kwa nyuma. Mtu aliyeenda eneo la ajali na baadaye hospitali anasema gari ya Dr Mwakyembe aina ya Landcruiser ilikuwa ina-overtake malori mawili na ghafla dereva alishtukia shimo kubwa mbele yake akapoteza control na gari ikapinduka ikiwa pia imegonga mti mkubwa na kuuong'oa.

I'm worried na hawa madereva wa mawaziri na wabunge ... look at Salome Mbatia's accident ... Chacha Wangwe's ... Zito kukoswakoswa ... and many others! can't these drivers be bribed ili wawapoteze wapiganaji???? aren't they intelligency affiliates?? who hires them??? some of these drivers waweza kuwa wanalipwa mshiko mkubwa ili kutekeleza mipango ya wakuu wa nchi ....
 
Mpiganaji MWAKEYEMBE? de man himself....

Kila mtu atembea na kifo, tusihofu wenzangu yatajiri ya mwenyezi Mungu..naamini hata sir God hawapendi mafisadi, so lets pray 4him to recover well.

Ajali ya gari?....tuelezwe ukweli tafadhali, maana ya Kapuya nayo kiini macho, ya Mudhihiri ndio changa la macho kabisaaa kwani yasadikika/yaaminika alikatwa mkono na mume wa mtu(ambaye alibaini uhusiano wa Mudhihir na wife wake) wakatudanganya alipata ajali iliyopelekea kukatwa mkono "ON THE SAME DAY"...madaktari mpo hapo?...tumuachie Ngoswe.

Mr Clean/Mwakyemebe ugua pole mkuu
 
Nakutakia upone haraka Mhe Mwakyembe pamoja na wengine waliohusika katika ajali hiyo. Kama kuna mkono wa ufisadi ushindwe kwa jina la Yesu.
 
yote yanamwisho, kama mwisho wa mwakyembe sio huo, na sio kwa ajali ya gari basi tutakuwa nae mpaka mwisho wa mapambano lakini kama ndio mwisho wake basi ni mapenzi ya mungu
 
HABARI ZA SASA.
Dr. atasafirishwa wakati wowote kwenda MOI DSM kwa ajili ya check up zaidi. Anendelea vizuri ingawa amepata maumivu ya shingo. Ofisi ya Bunge inatarajia kutuma ndege ndogo mchana huu kwa ajili ya kumfikisha MOI DSM.

Tunashukuru RAS wa Iringa, Ofisi yake na timu ya madaktari wa Hospitali ya Mkoa wa Iringa kwa kusimamia suala hili vizuri.

Tunamshukuru pia Chief Secretary Bw. Philemon Luhanjo kwa kufika haraka kumuona pale hospitali. Bw. Luhanjo alikuwa hapa kuhudhuria mazishi ya mtoto wa nduguye ambaye ni Daktari katika Hospitali ya Mkoa.

WITO wetu pamoja na kudhibiti ajali za barabarani ni vizuri Wizara ya Afya ikatoa haraka mwongozo wa namna ya kuimarisha hospitali za Mikoa ambazo wao sasa wanataka ziwe za rufaa. Wanapochelewa kutoa ikama za watumishi wa hospitali hizo wajue wanachelewesha kuongeza idadi ya Madaktari ambao wangeweza kukabiliana kwa haraka na matukio ya aina hii yanapotokea.

Nadhani sasa baada ya saa chache wenzetu wa DSM watatupatia maendeleo ya hali yake.
 
nyie set-up inatoka wapi? accidents are the most inefficient way of killing someone
kwanza thez no guarantee of them dying. Mmeskia ajali tuu ata masaa hayajapita mshaanza speculation.. watu wa AJAbu sana nyie!
 
Back
Top Bottom