Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 21,512
- 37,829
Ukitaka vichekesho bila gharama soma Taarifa za Polisi. Katika tukio la hivi karibuni la kupote na Kuuawa kijana Robert Mushi na kishà maiti yake kukutwa Mortuary ya hospitali ya rufaa ya Polisi Kilwa road, Jeshi la Polisi limetoa Taarifa ya kuumizwa na maneno wanayoyaita ya uzushi wa taharuki toka Kwa wanaharakati G.J Malisa na Boniface Jacob na kamwe hutaona mahali walipoumizwa na kifo cha Robert Mushi.
Mbali ya Taarifa yao kutoa hitimisho la chanzo cha kifo kuwa ajali ya kugongwa na gari lililokimbia (Hit & Run), hakuna sentensi hata moja inayoonyesha gari Hilo linatafutwa au limeshakamatwa.
Hiki ni kichekesho kinachohuzunisha. Watu wakiwatuhimu Polisi kuhusika ni vigumu kukwepa. Haiwezekani Polisi ishughulike na kesi ya kukashifiwa wao binafsi kuliko kuwasaka waliomuua Mushi iwe ni Kwa ajali au ajali ya kutengeneza.
Leo utawaambia nini watu huusiki wakati lugha ya matusi/kashifa ni kosa kubwa kwako kuliko kifo cha Mtanzania masikini?
Kwanini Polisi haitumii nguvu hiyo hiyo kuwasaka wauaji wa Robert kama inavyotumia nguvu na gharama kubwa kuwasaka WAZUA TAHARUKI. Kipi kina thamani Kati ya UHAI wa Robert na HESHIMA ya Polisi?
Polisi mnashindwa kujeshimika sababu ya maamuzi ya ovyo kama haya. Yaani heshima yenu ni muhimu kuliko uhai wa mtu?
Pia soma:
- Kamanda Muliro: Malisa GJ, Boniface Jacob wakamatwe kwa tuhuma za kupotosha taarifa za kifo cha Robart Mushi
- Utata sakata la ndugu wa Boniface Jacob: Kupotea mpaka kukutwa mochwari ya polisi, Amana wapigilia msumari!
- Boniface Jackob afika kituo cha Polisi cha Oysterbay ili akamatwe kama alivyoagiza RPC
- Jeshi la Polisi lapekua nyumba ya Boniface Jacob, laenda na GJ Malisa Moshi kupekua nyumba yake