Ajali ya Dr. Mwakyembe na yatokanayo

KIKWETE HAKUJUI MBEYA WALA HAKUMHUSU,
HALI KADHALIKA WANANCHI WA MBEYA HAWAMJUI KIKWETE NA WALA HAWAHUSU.....
MAHUSIANO YA BWANA MKUBWA NA WATU WA KANDA HIYO YA CHINI MAGHARIBI NI MBAYA.....
HAMNA HAJA YA VISASI.
UJENZI WA BARABARA KUTOKA SUMBAWANGA HADI MBEYA, NA MAREKEBISHO MAKUBWA KWENYE BARABARA YA KUANZIA MBEYA HADI MIKUMI NI MUHIMU SANA KWA TAIFA LETU....
HAWA JAMAA TUNAO WAACHA NA BARABARA YAO MBOVU NDIO WANAOLISHA NCHI...
TUWAHESHIMU KWA KILE WANACHO TUSETIRI NACHO
 
1. Get well soon mzalendo!

2. Ule uwanja wa Songwe ukiwa tayari sioni haja ya kusafiri kwa gari ndogo toka Mbeya hadi Dar..ni mbali sana..na ni cheaper na salama zaidi kutumia ndege!
 
Pole Dr. Mwakyembe pia inatukumbusha Waziri Mkuu Sokoine wakati wa ajali yake pamoja na yule mbunge wa chadema, tuwe makini wa Tz kwani hizi sehemu tunazosema zinamatukio mengi ya ajali na jamii kuamini hivyo kuna uwezekanao zikatumika na wengine kwa kukamilisha matakwa yao kwa kutumia kigezo kama hicho kuwa hii sehemu inasifika kwa ajali .(don`let them full you all the time.)
 
1.

2. Ule uwanja wa Songwe ukiwa tayari sioni haja ya kusafiri kwa gari ndogo toka Mbeya hadi Dar..ni mbali sana..na ni cheaper na salama zaidi kutumia ndege!

Kama wewe ni mzalendo halisi usingezungumzia ndege. Labda unatania. Mzalendo halisi anasikia tu mlio wa ndege. Halafu unasema "cheaper", kweli? Mwanza ni mbali zaidi kuliko Mbeya kutokea Dar. Je, ni wangapi wanapanda ndege kwenda Mwanza. Je, unadhani hawapendi kuwahi kufika na kuwa salama? Linganisha na mabasi yanayoondoka kila siku kwenda Mwanza. Pole Mwakyembe.
 
Wakulu,

Kwanza naombautoa pole kwa wale wote waliopata Ajali bila kuangalia huyu ni nani,hapa wote tumekaa kuangalia Mwakyembe peke yake na hatuangalia Dereva ana khali gani.,Hii ni tabia ambayo tumerithishwa na CCM,ubinafsi na ndiyo inatufanya tuwe hapa kila siku

Tunathamini wale wenye majina tu,yaani ni bora mtu amsikini aliyeko sehemu flani afe ila mwingine apone na ndiyo maana ukeienda Hospital Bombo au sehemu za starehe na ukiwa umeongozana na Pedeshee au Mkuu yoyote wata ku-skip..

anyway Bongo yetu

Wenye Taarifa Derve anaendeleaje?Je kuna wengine wlaiokuwapo katika hiyo Gari?

Gembe hata wachungaji wanazikwa na maaskofu, hiyo haina maana kuwa muumini wa kawaida hana thamani mbele ya askofu, sipokuwa ni kawaida ya binadamu kuguswa na sahibu linalomkuta mtu aliye karibu naye kuliko... katika hili Dr. Mwakyembe yupo karibu na Watanzania wote bila kujali jinsia wala rangi, kwani amesimamia upande wao katika vita takatifu dhidi ya ufisadi, na hili ndilo linalofanya kila mtu kuguswa na hili tukio.
 
Uwanja wa ndege wa songwe...
Mbona kichekesho??/
nani kasema utaisha siku za jirani??
Mwaka kesho ujenzi utapamba moto ile mbaya,
mwezi wa kumi na mbili utasimama....
Mwaka 2015 january ujenzi utaanza tena....
Lazima tuutumie sana uwanja ule kwa ajili ya kupata kura za wanchi wabishi wa huo mji mkuu wa chini magharibi
 
Kama wewe ni mzalendo halisi usingezungumzia ndege. Labda unatania. Mzalendo halisi anasikia tu mlio wa ndege. Halafu unasema "cheaper", kweli? Mwanza ni mbali zaidi kuliko Mbeya kutokea Dar. Je, ni wangapi wanapanda ndege kwenda Mwanza. Je, unadhani hawapendi kuwahi kufika na kuwa salama? Linganisha na mabasi yanayoondoka kila siku kwenda Mwanza. Pole Mwakyembe.

We Congo acha ubishi hivi unajua ku-drive land cruiser toka mwanza hadi Dar ni shilingi ngapi (mafuta)? hapo bado hujamlipa posho dereva. Ukifanya hesabu zako vizuri utatambua kuwa ndege ni cheap zaidi. au ulipigia hesabu ya basi? lol

Halafu aliyekuambia mzalendo lazima awe masikini ni nani? yaani tajiri hawezi kuwa mzalendo! nimechoka kabisa.
 
Ndo maana sipendi kuwa mwanasiasa kwani nitawaachia majonzi familia yangu kabla ya wakati...

Mungu ampe afya na apone mapema

Msanii, familia hiyo hiyo itaanza kujiuliza, hivi baba yetu ameishi miaka 75 au 90 kuna lolote la maana alilifanya kwa famili au taifa letu kwa ujumla? bila shaka watahitimisha kuwa bora tu asingezaliwa au kuishi miaka yote hiyo na kutuletea dhiki hii kuu.
 

Wewe uliyedokeza kwamba ni Rostam anahusika, ulidhani mazuri hayo kuyasema?

Na wengine waanze ku speculate kwamba alikuwa anakimbiza gari maporini huko, sawa? Au tuanze ku speculate kwamba kalewa huku anaendesha?

Ajali wapate kunguru, akipata njiwa njama!

Kwa hiyo wewe ndio advocate wa RA?
 
teh teh teh..olalalalala..umeangukia pua.
hii ni ajali na aliyepata ajali ni MTANZANIA MWENZETU, BINADAMU MWENZETU lakini pia ni KIONGOZI katika nji hii, tumuombee apone na kumtakia afya njema...harakati zake katika kupigania usawa na kuupinga ufisadi nchini wengi tunaziunga mkono ndio maana wengine wamesema we need him now than ever...inabidi asaidiwe maana hawezi kufanya kazi peke yake..hata wazo la kuangalia usalama wake hapo alipo ni la muhimu....
 
Wapinga ufisadi wote hawapaswi kupata ajali, kuugua, kuandikwa vibaya, kukosolewa,.... na ikitokea hayo mabalaa yakawakuta, mafisadi waandamwe, walaaniwe,...Hebu tukuekue kidogo WATANZANIA wenzangu.

Waislamu na wakristu wanaamini kuwa mabaya yote yanatoka kwa shetani. Na binafsi naamini kuwa mafisadi ni maadvocate wa shetani wakati wapinga ufisadi wanasimamia kweli ambayo ni mapenzi ya Mungu; hivyo inaniwia vigumu kuwatenganisha mafisadi na chochote kibaya kinachowatokea wapenzi wa Mungu ambao wanaisimamia ile kweli.
 
Pole Mwakyembe Mungu akujaalie afya njema baba. Sijui kina JK watasema tena anajitafutia umaarufu!!
 
Haiwezi kuwa imetoka moyoni, huo ni unafiki tu wa RA kama kweli ametuma hizo salam za pole.
Halafu hawa TBC wanavibweka. Kwanini wamtafute RA ili atume salam?mbona wasimtafute Selelii au Anna Malecela? Mi nadhani ile nguvu aliyoitumia kupata kipindi maalum kumjibu mzee Mengi bado imewalevya tbc ya Dunstan Tido Mhando.

watu wengine humu ndani na nyie mtapata ajali, kwani hamjui kwamba RA ndiye Mwenye Nchi?
 
Mungu wa mbinguni awape uzima wote waliohusika na hii ajali. Wapone haraka ili isije leta fadhaa kwa Wa-TZ.
 
Inasemekana Dr. Mwakyembe ameumia kidevu ila ana nafuu, gari lake limeharibika vibaya. Je walikuwa wangapi kwenye gari? Mungu amsaidie na dereva wake ambaye pia nasikia kaumia.

Mambo mengine yanasikitisha sana!

Ajali imetokea maeneo ya Ifunda ambayo ni mji kabla ya kufika njia panda ya kwenda Iringa mjini.

Mtanzania hapo si karibu na jia panda ya mjini kwa kuna kilomita karibu 40 au zaidi mpaka kufika njia panda ya town
 
watu wengine humu ndani na nyie mtapata ajali, kwani hamjui kwamba RA ndiye Mwenye Nchi?

Ni kweli kabisa mkuu, najua mwenye nchi hawezi kupata ajali kama sisi lakini hatutachoka kusema madhambi yake. Akitaka tusiseme asiishie kutusababishia ajali tu bali ahakikishe kuwa tunakufa woote tunaopinga ufisadi, abakie na ma-advocate wake tu ili wafurahie maisha.
 
Back
Top Bottom