Acha propaganda zako, mtu kuandika hapa JF atamkwamisha vipi mbunge ku deliver? kwahiyo JK akishindwa ahadi zake ni kwasababu anaandamwa JF? Kuandamwa ndiko kunaweza kuwa chachu ya kukufanya uongeze juhudi na sio vinginevyo.hatuwezi wote kuwa polotician ila ni wajibu wetu wote kuleta maendeleo. Siku moja niliwaza kwanini James Carville au Paul Begala Wasigombee urais wenyewe badala yake wanampa akili zao zote president Clinton au Karl Christian Rove asingekuwa yeye president badala ya Bush kwa mtizamo wangu huyu jamaa ni ten time clever than bush pia David Axelrod badala ya obama mzee wa teleprompter guess who is writing.
Jibu nililolipata ni kwamba si lazima wote tungombee uraisi au ubunge bali nijukumu letu wote kuhakikisha kile tunachoamini kinafanikiwa (kwa watu wa kyela ni shule, maji afya na watu kuacha uvivu).
Badala ya kumchukia mbunge wako na kutaka ukagombee wewe (ni haki yako) akikisha amepewa muda wa kutosha kutekeleza majukumu, Ili miaka mitano( bila kumchomolea tairi za gari hakuna uchaguzi mwingine) ingalau kitu kifanyike ukimkwamisha kabisa kwanza miaka mitano inakwenda bure na pili huna uhakika wa kufanikiwa na tatu unkuwa umetesa maelfu kwa ubisfsi wako.
Mbunge wetu angefanya mambo mengi na makubwa sana kama watu wangetofautisha muda wa kampeni na muda wa kufanya kazi. sasa hata asipo deliver ana sababu kubwa ya kutuambia. Na uchaguzi wa kyela hautakuwa wa issues hata siku moja bali utakuwa wa events tu. Tutasikia hata siku moja kura zikiombwa kwa "nimeleta maji kwa vijiji 4 kata ya saba nipeni muda nimalizie vilivyobaki " bali itakuwa "mimi ninaungwa mkono na raisi"
Mbona Dr. Slaa kazungukwa na CCM kila upande na anachapa kazi?
Acha kutafuta scapegoats wa kila failure, haikusaidi wewe wala haimsaidii huyo mbunge wako. Kama watu wamechomoa tyre ya gari lake toa ushahidi, vinginevyo unakuwa kama Yahaya Hussein.
Hakuna aliyemkwamisha mbunge kufanya kazi zake Kyela; kama unaamini hilo basi akina Zitto wasingefanya kazi yoyote kule kwenye majimbo yao.
Mkuu usipotoshe watu; tuna mifano mingi tu ya kuonyesha kwamba anayekwamisha maendeleo ni yeye mwenyewe kwa hofu ya kwamba kila anayefanya jambo la maana Kyela anataka kumwondoa kwenye ubunge. Tulimwunganisha hata na watu wa kusaidia baadhi ya mambo Kyela lakini hata siku ya appointment hatokei; watu tukapata aibu kweli kweli; mtu kama huyo utamsaidia vipi?
Kweli sio kila mtu anaweza kuwa mwanasiasa na sio kila mwanasiasa anaweza ku deliver na ndio maana kuna uchaguzi kila baada ya miaka mitano ili wale walioshindwa kazi kuwe na njia ya kuwaondoa. Hata ningetaka kugombea ubunge ni haki ya raia yeyote wala haiwezi kumfanya mbunge aliyepo ashindwe kufanya kazi.
Kama mtu anashindwa ku deliver ni kwasababu hana uwezo; mengine yote ni visingizio tu.