Indume Yene
Platinum Member
- Mar 17, 2008
- 2,950
- 711
Ndg wanabodi Heshima kwenu..
Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..
Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..
Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..
1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..
Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.
Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..
Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.
2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:
Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.
3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE
Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.
Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..
4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE
Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.
5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE
Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...
Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.
6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..
Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..
7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE
SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...
Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.
Karibuni kwa Mawazo chanya pia.
Mawazo yako mbadala nayaunga mkono, kitu kingine ambacho ningependa kuongeza ni kubadili sheria ya barabara. Naamini ukitenganisha lanes zinazokwenda muelekeo mmoja na upande mwingine, ajali za uso kwa uso ambazo Tanzania zimekuwa nyingi zitapungua. Ukiwa na lanes kama hizi hapa chini, ajali za ana kwa ana zitapatikanaje? Hata kama mtu ana-over pass gari nyingine, anafanya hivyo akiamini kabisa hakuna gari atakayokutana nayo ikiwa inakuja kuelekea direction nyingine. Tumeona ziara nyingi za JK kufungua barabara mpya but sidhani kama suala la ajali mara nyingi huwa linaangaliwa. Kinachoangaliwa ni kura na kula tu. Ni wakati sasa sheria ya barabara ibadilishwe ili ziweze kupanuliwa na kutengwa by traffic directions kama kwenye hii picha chini.