Ajali Tanzania: Mawazo mbadala kuhusu udhibiti wa ajali Tanzania

kwa sisi abiria tusikubali madereva wanaoendesha kwa mwendo kasi pindi tuwapo kwenye mabasi yao. Tuungane kuzuia uendeshaji huo
 
Ndg wanabodi Heshima kwenu..

Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..

Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..

Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..

1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..

Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.

Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..

Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.

2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:

Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.

3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE

Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.

Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..

4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE

Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.

5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE

Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...

Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.

6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..

Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..

7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE

SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...

Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

Karibuni kwa Mawazo chanya pia.
 
Meremeta walisema haiwezi kuongelewa, Mwanakijiji akaja na kuweka riport nzima kwa bei nafuu kabisa. Sasa Madereva nao wamethibitisha kuwa ajali zinaweza zikapunguzwa kwa bei nafuu zaidi. Ningelitegemea Serikali au NGO iwasaidie hawa jamaa maana kuokoa maisha ni kazi kubwa saana.

Madereva wa mabasi waanzisha ukaguzi wao ili kupunguza ajali
Na Sharon Sauwa , 20th October 2009

Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Uchukuzi, (COTWU), Tawi la Ubungo Terminal Jijini Dar, limebuni mbinu mpya ya kupunguza ajali za barabarani kwenye mabasi ya abiria kwa kuweka wakaguzi wao maalum katika barabara zote zitokazo Dar kwenda mikoani.

Mwenyekiti wa tawi hilo, Chrisant Kibogoyo, amesema zoezi hilo lilifanyika kwa mwezi mzima wa Septemba mwaka huu na kwa bahati, hakuna ajali yoyote iliyotokea.
"Tulichokifanya ni kuweka wakaguzi katika kila barabara ya kwenda mikoani... wakaguzi hao walikuwa wakipanda mabasi ya mwanzo ambayo huondoka alfajiri kila siku ili kuhakikisha kuwa hakuna basi linalolipita jingine lililotangulia," akasema.
Aidha, akaongeza kuwa kwenye mabasi hayo, wakaguzi hao walihakikisha yanakwenda kwa mwendo uliopangwa wa Kilometa 80 kwa saa.
Akasema wakaguzi hao walikuwa wakiwasiliana na maofisa usalama barabarani katika kila mkoa ili kutoa taarifa zozote za uvunjaji wa sheria, ambapo waliobainika wote walikamatwa.
Mwenyekiti huyo akasema zoezi hilo lilifanyika kwa mwezi mmoja kwa majaribio na mkakati unafanywa ni kulifanya liwe endelevu. Akasema changamoto zinazokikabili chama hicho ni ukosefu wa fedha za kuwalipa wakaguzi hao. Akaomba wadau wote kusaidia mpango huo ili uwe endelevu na baadaye kumaliza tatizo la ajali za barabarani.
Akasema baada ya zoezi hilo, imebainika kwamba ajali nyingi zimekuwa zikisababishwa na mwendo kasi unaofanywa na baadhi ya madereva.
"Hali hiyo inatokana na madereva wengi kutokuwa na mikataba ya ajira na wenye mabasi," akasema.
Akaongeza kuwa madereva hao wamekuwa wakilipwa kila wanapofikisha salama basi.
Akasema asilimia 80 ya madereva wa mabasi hawana mikataba na wamiliki wa mabasi huku asilimia 80 ya madereva wakilipwa mishahara ya chini ya ile iliyopangwa na Serikali.
Akitoa mfano, Kibogoyo akasema madereva wanaotoka Dar es Salaam kwenda Arusha hulipwa kati ya Sh. 15,000 na Sh. 30,000 kila wanapofika mwisho wa safari.
Ajali za barabarani, hasa katika mabasi ya abiria, zimekuwa zikipoteza maisha ya wananchi wengi wasio na hatia, hali iliyomlazimu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete, kutoa agizo la kutaka kurekebishwa kwa sheria za sasa ili kupunguza tatizo hilo .

CHANZO: ALASIRI

Ajali.jpg

Ndg wanabodi Heshima kwenu..

Bila shaka vifo vingi vinavyotokea kwa kiasi kikubwa hivi sasa ni kutokana na ajali za magari barabarani hasa Mabasi..

Tunaipongeza serikali kwa hatua mbalimbali ambazo imekua ikichukua ili kukabiliana na Changamoto hii kubwa japo kwa kiasi kikubwa bado ajali ni janga kwa nchi yetu..

Kwa kua akili ni nywele na kila mtu anazake,nami pia naomba kuwashirikisha fikra nilizonazo kama ifuatavyo..

1)SERIKALI IANZISHE VYUO MAALUMU KWA AJILI YA MAFUNZO YA UDEREVA WA MAGARI YA ABIRIA PEKEE..

Serikali na sio vyuo binafsi vianzishe vyuo maalumu kwa ajili ya Madereva wa Abiria pekee...
Hii itasaidia kupunguza madereva wa Mtaani wanaopiga dayworker kisha baada ya Muda wanaendesha mabasi ya Abiria.

Nimesema vyuo maalumu na wala si VETA wala vyuo binafsi Kutokana na sababu kua sasa ,VETA na vyuo vingine binafsi vimekosa credibility yaani mtu yeyote anaweza pata leseni hata kwa magumashi ilimradi awe na pesa..

Lakini pia ili mtu A-qualify kusomea udereva wa magari ya abiria awe amesoma mpaka kidato cha nne na awe amefaulu ili kupata watu makini wanaojielewa na si kuokoteleza hadi STD VII kama ilivyo sasa.

2)KILA BASI LISAFIRI NA ASKARI WA BARABARANI ANGALAU MMOJA:

Sio lazima askari aanze mwanzo wa safari mpaka mwisho wa safari...kunaweza kua na utaratibu wa askari maalumu wa barabarani kupokezana kila wilaya ambako gari hiyo itapita..hii itasaidia kwa kiasi kikubwa kum-control driver hivyo kufata sheria zote za barabarani kama inavyopaswa.

3)MISHAHARA YA MADEREVA IBORESHWE

Hii itasaidia watu wengi kuwa motivated na kupenda kazi ya udereva ma mabasi hivyo kupata watu wengi wanaoqualify,hii inamana mtu aiendeshe gari kwa kua ameona ndo sehemu ya kutokea bali udereva uwe tamanio la mtu mwenyewe.

Wapewe pesa ya kutosha na posho juu ili kumfanya Dereva afurahie kazi yake na kupunguza msongo wa mawazo..

4)MISHAHARA YA ASKARI WA BARABARANI IBORESHWE

Hii itasaidia kwa kiasi kikubwa askari hawa kutoshawishika kuchukua pesa ndogondogo wanazopewa njiani hivyo kupelekea kufanya kazi zao kwa uaminifu na umakini wa hali ya Juu.

5)ASKARI WA BARABARANI WAPUNGUZWE

Wingi wa Askari wa barabarani waliopo hivi sasa haimanishi ni kuboresha utendaji na udhibiti wa ajali barabarani..unaweza kua na askari wachache na wakafanya kazi nzuri yenye zaidi,iwapo madereva hawataokotwa mitaani,wakalipwa pesa vizuri na askari nao wakalipwa pesa vizuri hakika makosa barabarani yatapungua kwa kiasi kikubwa..hii ina apply kwa madereva wa magari yote barabarani...

Iwapo adadi ya askari barabarani itakua ndogo itakua rahisi kuwa hudumia financially na kwa pesa nzuri zaidi.
Nashauri askari barabarani walipwe kuanzia milioni 1 kwa Mwezi.
Utitiri wa askari barabarani haimanishi ndio uimarikaji wa utendaji kazi.

6)UKAGUZI WA MABASI YA ABIRIA KABLA YA SAFARI UIMARISHWE..

Ukaguzi wa maramojamoja unaofanywa na askari wa barabarani kwa sasa unamapungufu makubwa..
Pawe na kikosi kazi maalumu ambacho kazi yake ni kukagua mabasi yote ya abiria siku moja kabla ya safari na gari hiyo iwe na alama kua imekidhi vigezo vya kusafirisha abiria kesho yake..Hii itasaidia hasa kupunguza ajali zitokazazo na uchovu wa magari yenyewe hasa yale yanayounga safari bila kupumzishwa..
ikiwa na pamoja na kumpima dereva kabla ya kuanza safari kama hatumii madawa ya kulevya wala kilevi chochote..

7)SUMATRA WASIFANYE KAZI KWA MATUKIO PEKEE

SUMTRA Wasisubiri kupaza sauti katika kuwaambia umma kua nauli zitapanda kutokana na bei za mafuta kuongezeka,na wasisubiri mpaka matatizo yatokee ndo wajitokeze kwa waandishi wa habari kama wanavyofanya hivi sasa.SUMATRA Ifanye kazi yake ipasanyo na isifanye kazi kisiasa...

Nimesema ni mawazo tu sio msaafu wala Biblia unaweza kosoa au kuboresha kwa Mtazamo chanya ili kutoa mawazo sahihi kisha yafanyiwe kazi na mamlaka husika.

Karibuni kwa Mawazo chanya pia.

Kwanza kabisa nikupongeze kwa kuguswa na hili na kutuletea mada yanye tija kwa kila mmoja wetu,nategemea kuwaona watu mkiweka maoni yenu hapa kuliko kushabikia siasa zinazojadili watu badala ya mijadala yenye tija kama hii.

Naungana na yote uliyoyasema isipokuwa hilo la mabasi kusafiri na Askari.

Mawazo yangu ili kudhibiti ajali ni lazima kwanza kutambua vyanzo vya ajali,

pamoja na vyanzo kuwa vingi lkn mwendo kasi na uzembe wa madereva ndio chanzo kikuu cha ajali za barabarani.

Suluhisho ni kuwapangia muda madereva kufika kwenye vituo.

Mfano mabasi yaondoke Dar saa 12.00 alfajiri na yafike morogoro saa 4:00 yafike Dodoma saa 8:00,yafike manyoni saa 9:30,Singida Saa 11:00,Misigiri saa 12.30, Igunga saa 1:50,Nzega Saa 2:30 na hatimae kahama saa 4:00.

Masaa hayo yapangwe kitaalamu na watu wa sumatra baada ya kujiridhisha umbali toka eneo moja kwenda eneo jingine,

Kila kituo kiwe na askari ambao wapo serious na kuwepo na utaratibu kama ule wa treni wa kupewa line clear,hivyo mtu atachukua kibali maalum mahala anapoanzia safari kinachoonyesha muda na atapaswa kukabidhi kibali hicho kwenye kituo cha mbele na kupewa kingine kinachomruhusu kuendelea na safari,afanye hivyo mpaka mwisho wa safari yake,.

ili kuepusha usumbufu maeneo vinapotolewa vibali pawepo na vyoo pamoja na hotel za kula chakula,lengo ni kutumia mudaa wa kuonyesha kibali huku abiria wakiruhusiwa kuchimba dawa na kupata chakula,hivyo hakutakuwa na malalamiko,

Kama hilo halitoshi tunaweza kuyatumia maeneo mizani kama check point ya muda wa kuwasili eneo husika.

tukifanya hivi italeta self control ya madereva ,adhabu yake iwe kuahirishwa safari na abiria kuwekwa katika mabasi mengine kwa kibali maalum na dereva kuwekwa ndani mwezi mmoja na gari kufungiwa kusafirisha abiria kwa muda wa mwezi mmoja.

kama tutafanya hayo hakika hakuna dereva wala mmiliki wa gari atakaefika eneo husika kabla ya wakati.

Kufanya hivyo kutawafanya madereva kutembea mwendo wa kawaida na hivyi kupunguza ajali kwa kiwango kikubwa.

Pendekezo hili ni baada ya safari yangu toka Dodoma,gari ya kwanza kufika Dodoma ilikuwa campuni ya KISBO ikiduatiwa na Leina na CITY BOY.

Hizi ni basi zilizojizolea umaarufu kwa kukimbia kupita kiasi kiasi cha kufika kahama saa 12:30 badala ya saa tatu usiku.

Tulipofika manyoni walisimama petrol station na kutueleza abiria kuwa tunasubiri muda wa kufika Singida.

ilikuwa saa 7:20 za mchana na singida tulipaswa kuingia kuanzia saa 10.30 au zaidi ya hapo.

Hivyo tulilazimika kukaa muda wa saa moja na nusu ndipo tukaendelea na safari,

Gari zoote zilizotoka Dar zilikuwa kama msafara na hakuna aliethubutu kukimbia,waliogopa faini kubwa ambayo hutozwa singida endapo Gari itafika kabla ya muda uliopangwa.

Mwisho ni kwetu wapiga kura ambao ndio wahanga wa ajali hizi,tusiwachague tena wafanyabishara kuwa wabunge wetu,maana wengi wao hutumia fursa ya vyeo vyao kuwafanya hata askari Polisii wayaogope magari yao.
 
Hapo umenena ila hapo kwa traffic ni ngumu sana kudhibiti kwani hata wakilipwa milioni mbili ni yaleyale kwani rushwa itabaki kuwa posho mbadala wacha mshahara
 
Hapo umenena ila hapo kwa traffic ni ngumu sana kudhibiti kwani hata wakilipwa milioni mbili ni yaleyale kwani rushwa itabaki kuwa posho mbadala wacha mshahara

Ila angalau itapunguza mkuu, kuliko ilivyo sasa.
 
hayo mabus wamiliki wake ndio wafadhili wa ccm utaanzia wapi kuwadhibiti?
CC:zakaria wa mwanza_sirari
 
Mkuu safi sana,

Kwa ufupi mawazao yako ni mazuri, isipokuwa swala la Askari kuwemo kwenye basi, hii ni ngumu kwa sababu ya wingi wa mabasi. Badala yake ni bora kujenga mfumo imara wenye kujali uwajibikaji hasa self discipline ya madereva ambapo inatakiwa watii utaratibu wa matumizi ya barabara bila shuruti.

Hili ni moja ya eneo ambalo KATIBA bora inaweza toa mwelekeo chanya na kuleta mabadiliko makubwa, ni bahati mbaya sana tunapoongelea katiba watu wengi wanawaza siasa tu.

M.
 
hizi ni zama za digitali,kwann magari yote ya abiria ya masafa marefu yasiwe na "car tracking system" kufuatilia mwenendo wa magari!
 
Kuna mengi nyuma ya ajali, niliwahi kusikia kampuni moja inayoelekea kufilisika ila ilivuma sana ilikuwa na tabia anampa dereva wa basi pinzani kiasi fulani cha pesa ili alisababishie ajali basi ili kupunguza ushindani!! Hapo vipi??

Lakini pia wamiliki wana nafasi kubwa sana kupunguza ajali kwa kuwa wajali kwa madereva wao!! Dawa ni moja, kampuni imeleta ajali na ikaonekana ya kizembe ifungiwe kabisaa!! Ili wamiliki nao washiriki katika hili, maana wamekaa kimya kama nao hawahusiki vile!!
 
Khaa!!™® Nadhani jambo la maana ni kupunguza msongamano kwa mabasi ya abiria. Njia mbadala kama treni za kasi, ndege na meli xa kasi ziimarishwe na kufanywa rahisi ili kila. Mmoja azitumie. Barabara tuache kwa mabasi machache na magari binafsi. Kiasi kikubwa cha abiria na mizigo isitumie barabara
 
Hiyo ni long term plan Mkuu, wanasiasa kwenye ilani za vyama vyao watakua nazo hizo..ila sasa itachukua 25 years ku implement hilo kwa viongozi wetu.Ngoja tujadili kinachowezekana sasa maana Vifo kila kukicha vinatokea wala havisubiri hizo barabara pana,treni za kisasa,ndege na Meli.
 
Kwanza kama Mwananchi na mdau wa usafiri ninaumizwa sana na hizi ajali ambazo zinaendelea kuchukua uhai wa ndugu, jamaa na marafiki huku zikiacha wengi wakiwa na ulemavu.

Mkuu wa kitengo cha Usalama barabarani jana ametoa kauli ya kutoa matumaini sana kwa watanzania.

Kwa uzoefu uliopo ajali nyingi zinatokana na madereva wasio na elimu na kazi waifanyayo na kukosekana mikataba ya kazi na si mwendo kasi kama tunavyoamini sasa.
Mpinga ametangaza kuanzia jumatatu kila dereva atembee na cheti chake kilichomwezesha kupata leseni ya udereva kwa ajili ya ukaguzi.

Tuwe wakweli na wawazi madereva wengi wa haya magari ya abiria hawana sifa ya kuendesha hayo magari ila wanalindwa na askari wa Usalama barabarani hatimae kusababisha ajali na vifo.

Magari yanayokimbia sana yanajulikana, lakini ni nadra sana kusikia hizo bus kupata ajali Sababu madereva wanaelewa jukumu lao wakiwa barabarani.

Mwisho niombe tu wote kwa pamoja tushirikiane kuwafichua madereva wanaotumia vilevi njiani.
 
Ni jambo jema.lakini lazima tukiri kuwa vyeti pekee haviwezi ondoa ajali barabarani. Hili jambo linatakiwa mchanganyiko wa hatua zikiwemo za sheria kwa watakao sababisha ajali za kizembe, ukaguzi wa magari hasa juu ya ubora wa tairi na vinginevyo, n.k
 
Kwakweli nidhamu ndio jambo la msingi sana,unaweza kuwa na dereva analipwa hata 2mil,na ni degree holder lakn kama akiwa barabarani hana nidhamu itakuwa hakuna jipya
 
Askari wanahucka sana,wao hata km dereva hajaqualify lakn wakipew cent ndogo tu bac dereva anaachiwa,dereva akikosea akitoa cent anaachiwa,wangekuwa wanapiga fain,serikal ingepata fedha na madereva wasingerudia kufanya uzembe wao,coz kutoa hela kirajic inauma kidogo
 
Vyeti tena? kibongobongo tu. Kwa nini wamiliki nao wasiguswe na adhabu hasa kwenye ajali hizi za kizembe kabisa?!
 
Wasiishie hapo waende wawashughulikie na hao waliowapa hizo leseni bila kukagua vyeti, maana hao ndiyo wenye sumu kali kuliko madereva wanao nunua hizo leseni
 
Mawazo ya mleta uzi ni mazuri na applicable Kwa muda huu. Tatizo hawa viongozi wanaguswa hadi wafe ndugu zao tu ila tukifa sisi hawajali si malikitu kwao.

Akina zitto walishikia bango kifo cha Betty last week eti cyber bulling na wakati waTz kibao hawana access na hiyo mitandao tu, wanasahau ajali zinazoua ndugu zetu kila siku
 
Wasiishie hapo waende wawashughulikie na hao waliowapa hizo leseni bila kukagua vyeti, maana hao ndiyo wenye sumu kali kuliko madereva wanao nunua hizo leseni

Hapo umesema kweli, lakini tujiulize nani wa kumshughulikia mwenzie, Labda kiundwe chombo kingine cha kuwachukulia hatua hawa askari.
 
Back
Top Bottom