kilimasera
JF-Expert Member
- Dec 2, 2009
- 3,068
- 268
KIKOSI cha polisi wa usalama barabarani kimeanzisha mpango kazi kwa kuwashirikisha askari wa vikosi vingine kama njia ya kupunguza ajali na malalamiko kwa askari wake.
Kauli hiyo imetolewa jana na Ofisa Mnadhimu wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Kamishna Msaidizi Mohammed Mpinga alipotoa taarifa ya kikosi chake nchini.
Alisema mpango huo utasaidia kudhibiti vitendo vya rushwa, ajali na kupunguza lawama kwa polisi wa usalama barabarani.
Akizungumzia utoaji wa leseni mpya, Kamanda Mpinga alisema mikoa tisa imetengwa na kujengewa uwezo wa kutengeneza mifumo ya kompyuta kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato (TRA).
Aliitaja mikoa itakayohusika kwa utoaji wa leseni awamu ya kwanza kuwa ni Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Ilala, Temeke, Kinondoni, Mbeya, Dodoma na Mwanza.
Kamanda huyo alisema utaratibu wa vikosi kazi utaenea kila mkoa na kusaidia katika kupambana na makosa ya usalama barabarani na ajali kwa ufanisi.