Madereva wa mabasi ya abiria watakiwa kuacha matumizi ya vilevi kuepuka ajali

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,814
11,991
426d7512-1e42-4dd8-9cee-2af758cb38ed.jpeg
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani limefanya ukaguzi wa mabasi ya abiria katika Stendi Kuu ya Mabasi kabla ya kuanza safari na kuwataka madereva kuzingatia Sheria, Kanuni, Alama na Michoro ya Usalama Barabarani ili kuepuka ajali.

Akizungumza Disemba 23, 2023 mara baada ya kuendesha zoezi la ukaguzi wa mabasi ya abiria Stendi Kuu ya Mabasi Jijini Mbeya, Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mrakibu wa Polisi, Hussein Gawile amewataka madereva kujenga utamaduni wa kufanya ukaguzi wa vyombo vyao vya moto kabla ya kuanza safari.

Aidha, Mrakibu wa Polisi Gawile amesema kuwa, licha ya kufanya ukaguzi wa mabasi ya abiria pia wameendesha zoezi la kuwapima ulevi madereva wa mabasi ya abiria kwa kutumia kifaa maalum kabla ya kuanza safari zao ili kujiridhisha kama hawajatumia kilevi au la.

"Nipo na kikosi kazi cha wakaguzi wa magari wa Jeshi la Polisi pamoja na wataalam ambao watawapima madereva ulevi kabla ya kuanza safari ili kuangalia kama wapo vizuri kiafya ndipo waanze safari," alisema Mrakibu wa Polisi Hussein Gawile.
a8df60ee-de60-4f3c-b820-09a404f06926.jpeg

7537defd-5b20-4e94-ab21-d3834843cef8.jpeg
Naye, Afisa Habari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, Koplo Esther Kinyaga amesisitiza suala la kuwa na matumizi sahihi ya kifaa maalum cha kuzimia moto (Fire Extinguisher) kwa kuwataka madereva kuhakikisha wanakuwa navyo kwenye magari yao ili kuchukua tahadhari endapo utajitokeza moto.

Sambamba na hilo, abiria wanaofanya safari zao kwenda maeneo mbalimbali, wamehimizwa kupaza sauti kukemea vitendo vya ukiukwaji wa Sheria za Usalama Barabarani kupitia Kampeni ya "Abiria Paza Sauti" (APS) inayoendeshwa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Mabalozi wa Usalama barabarani (RSA).
4bcc27dc-9078-4af1-8af9-2afbdd59ba3c.jpeg
 
Madereva wengi wa mabasi ya Mikoani wana fujo sana wawapo barabarani. Sijui wana matatizo gani.
 
Back
Top Bottom