Abuse..( Dhuluma)

AD mpenzi nitakujibu kwa namna ninavyoelewa mimi kama mimi....Punishment ni ile reward ambayo mtu anapata kwa kile alichokifanya..........s/he deserves to be punished kwa alichokitenda............lakini hiyo punishment iwe imezingatia vigezo vingi including respect ya mtu, utu wa mtu na position au uhusiano kati ya muadhibiwa na mtoa adhabu.

Abuse inaweza isiwe punishment kwa maana ya kuwa si lazima anayekuwa abused awe amekosea au amefanya kitu cha kumfanya aabusiwe. Abuse inawezatokea palipo na uonevu, inakuwa disrespective na haiangalii utu wa anayeadhibiwa/abusiwa. Maneno ya kashfa, dharau, udhalilishaji, disrespect, ignoring n.k vinaangukia kwenye abuse na si adhabu......kupiga bila makosa, kubaka, kulawiti na hata kupata sexual pleassure without the consent of the giver are forms of abuse my darling.

MJ1 dear
asante sana
umeelezea vema na kuelimisha vizuri

Naomba kila mtu asome hapa ili tusichanganye
haya mawili jamani ni mambo mawili tofauti kabisa..

hapo kwenye red hivi kama watu wameoana na wanaishi
pamoja kwa muda lakini kila mara mmoja hajisikii kufanya sex
na mwingine akawa anamlazimishia na mara nyingine kumwingilia
kwa nguvu Je waweza sema hiyo ni abuse??

sante mpenzi kwa majibu yako ya kuaminika ...
 
AD, haya husababishwa na sababu nyingi kama
Matusi: Hili hutokana na makuzi, dharau, jeuri na (ujuaji kwa madereva wa dsm) au kujihami
Kimwili; ubabe, uonezi na jeuri ya pesa
Ngono; uonezi, jeuri ya pesa, ubabe, tamaa na ulevi
kutelekezwa: uoga wa maisha, uvivu wa kufikiri, tamaa, ukatiri na ubinafsi
hate: visasi binafsi na vya kurithishwa, wivu na historia mbaya
Katika yote hayo ni ulimbukeni tu unaosumbua

Ni mtizamo wangu tu

asante sana kwa mtazamo wako
ningependa kukuliza ni group gani la watu
mfano.. watoto , wanawake, waume , vijana
wanaokubwa na hizo type za abuse na kwa nini
hilo group is the main target???
ntakuongezea maswali baada ya hayo ..
mmmhh Pole ae usinichukie sababu nakubana sana
hahahhahaah lol unasaidia wengi dear ..
 
My dear
kwanza nashukuru sana
kwa wewe kuweka mawili matatu ya muhimu
naona kila mtu anachapa mwendo mmmhhhh

sehemu iliyonivuta zaidi ni hapo kwenye red..
Nadhani hilo ndilo tatizo kubwa tulilo nalo nafikiri
kwa vile ni baba yangu na mume wa mama yangu
kila afanyacho kinabaki ndani ya nyumba hatutaki kumvunjia kheshima
au kila mtu anaona familia yetu ni nzuri sana basi hatutasema lolote.
au ni watu tu wanaogopa?......

ukiweza kurudi naomba unijibie hili swali dear..
nini tofauti kati ya punishment ya kawaida na abuse ???
maana naona wengi wanachanganya sana haya..
haya ukiweza ntakuwa hapa nakusubiri asante tena..
Punishment ya kawaida ni kukemea,kukaripia,kofi moja wak sio mbaya ni adhabu ya kawaida,kumlaza mtoto njaa,kumfunga mikono ukamchoma moto eti kaiba sumni,kumtandika mtoto hadi vitako vikachanika,kumchezea mtoto viungo vyake .....etc hiyo ni abuse,na abuse ZOTE ni punishable by law,anayefanya abuse akidakwa ajue atakula mvua tu.
 
Haya nimerudi sasa ....
Well kuna sababu nyingi zinaweza kumfanya mtu awe mnyanyasaji.....internal na external factors hapa zote zinahusika!!

Kujiweka juu-mtu ambae yupo kwenye kundi hili ni yule anaemnyanyasa mwenzake ili yeye ajisikie kwamba ni zaidi yake.Anamchukulia
anaemnyanyasa kwamba ni DHAIFU na yeye ana nguvu.Mara nyingi watu kama hawa hua ni wadhaifu internaly kwahiyo
anatafuta wale walio wadhaifu zaidi yake ili aweze kujipa kile anachokosa ndani yake.

Lawama-Huyu ni yule ambae anatumia lawama kama kigezo cha kumnyanyasa mwingine...yani yeye haoni anakunyanyasa kwasababu
WEWE NDO UMESABABISHA.Hawa ni wale wa usiingefanya kitu flani haya yote yasiingetoea...

Visingizio-Huyu hata siku moja hawezi kusema samahani nilichofanya ni kosa ila atakwambia yote ilikua ni hasira tu....kazini wameniboa..
nilishindwa kujizuia....yani hawa wanatumia hisia zao zisizohusiana na mhusika kumnyanyasa mhusika!!

Kubadili maoni-Hawa ni wale ambae kitu kisipoenda vile alivyotarajia/taka yeye ataanza kumkashifu mwenzake kwa maneno ili ajisikie
vibaya.Mara nyingi ndo wale unaosikia wanarudishiwa kwamba wasemacho ni maneno ya mkosaji....yani kilichokua kizuri
kikiwa sio chake kinakua kibaya.Ndo unakuta watu wameachana alafu mmoja anaanza kumnyanyasa mwenzake kwa
maneno ''ahh mtu mwenyewe mbaya...sura kama mbuyu na kadha wa kadha.

Umiliki-Mnyanyasaji anasikia raha ya kummiliki mnyanyaswaji pale mnyanyaswaji anapokubali kunyanyaswa....

Hasira za haraka-Hawa ni wale ambao mikono yao na maneno yasiyo mazuri yanawatoka haraka sana.Yani hawezi kudhibiti hasira zake kiasi kwamba hafikirii anachokifanya mpaka baadae wakati ameshaharibu tayari.Hii unaweza kusema hua haitokea kwa kukusudia maana wengi wao hua wanajuta baadae.

Kisasi-Kuna watu ambao wamewahi kunyanyaswa kwahiyo ile hasira anayotembea nayo anamtolea yeyote ili kujipa yeye unafuu.Na hii inamfanya asijione mdhaifu....

Chuki-Hii wala haihitaji ufafanuzi.Mtu akikuchukia anaweza fanya chochote kukuumiza iwe kwa maneno au kwa matendo.

Kwa sababu hizo hapo juu unaweza kuona kabisa wengine wananyanyasa wenzao kwa makusudi na faida binafsi na wengine wanashindwa kujidhibiti kwasababu wana matatizo yaliyoko ndani zaidi kwahiyo sio wanyanyasaji wote ni wabaya kwa maana ya kwamba sio wote wanachagua kua walivyo.
Kuwasaidia ni ngumu sana especially wale wanaofanya kwa makusudi.Na ugumu upo kwenye kujua kama kweli mtu anpofanya vile anakua hajakusudia maana wengi hua wanaishia kulaumu kitu kingine au watu wengine zaidi ya wao binafsi. Kumsaidia inabidi ujue chanzo cha ile tabia na yeye mwenyewe atake kubadilika....siku zote huwezi kumbadili mtu kwa lazima kwahiyo inabidi mhusika mwenyewe aseme kweli sipendi kua hivi na nasikia uchungu kwa ninayo/niliyofanya.
Ikiwa anataka kubadilika kwanza inabidi ajitambue yeye kama mnyanyasaji ....ajichunguze ndani yake kujua sababu na awe anajutia matendo/maneno yake.Ikifuatiwa na kumfanya ajisikie vile anavyofanya wenzake wajisikie...hii itamfanya ahisi huruma....alafu kutokana na majuto yake ajue kwamba anapofanya vile haimsaidii hata yeye maana at the end of the day anaishiia kulilia msamaha.Baada ya hapo aface hicho kinachomfanya awe vile ili aweze kuondokana nacho.
 
.......................................................................................................................................................

ASHA D UPO SAHIHI KABISA KABISA,
NA UMENIKUNA SANA HAPO KWENYE MFANO WAKO (RED),
MANAKE US NI MR NA MRS PERFECT HAWANA MAKOSA KABISA,ILA WAO SIKU ZOTE WANAONA MAKOSA YANAYOFANYWA NA WENZAO TU, PIA WANAJIONA KUWA NI WAO PEKE YAO NDIYO WENYE RUHUSA YA KUTOA ADHABU KWA WAKOSAJI. NA HAKUNA ADHABU NYINGINE ANAYOSTAHILI MKOSAJI ZAIDI YA KIFO......LAKINI NAAMINI KUTOKA NDANI YA MOYO WANGU KUWA IPO SIKU WATAONA MAKOSA YAO NA KUYAKUBALI KULIKO HIVI SASA AMBAPO JAPO WANAYAONA MAKOSA YAO LAKIN HAWAYAKUBALI...HAIJALISHI WATAKUWA WABABE KWA MIAKA MINGAPI LAKINI NAAMINI IPO SIKU ITAFIKA MWISHO WA UBABE WAO.

Maovu/matendo yote mabaya/huo ubabe/uonevu YOTE YANA CHANZO CHAKE,SABABU ZAKO,
VICHOCHEO vyake, ambavyo VIPO KATIKA JAMII zetu, na hata vinapoanza kujitokeza tunavidharau na kushindwa kuvikemea, tunapoanza kuchukua hatua tunakuwa tumechelewa au tunachukua hatua ya kutibu/kuzua maua badala ya kushughulikia mizizi yake.

eeee
kweli umeongea cha maana sana kuhusu US dahhh
mimi topic yangu ilikuwa ina target familia na jamii tuu
kumbe hata nchi na nchi zina dhulumiana dahhhh
asante kwa kunifungua macho dear ..

nway Je mafano baba ni mnywaji sana
baba anampiga mama kila jua likizama,
anatukana hajali nani ni nani anachukia
familia yake for no reason anatekeleza familia every now and then
Je kama kuna mtoto wa kiume aliye kulia kwenye familia ya namna
hiyo , unadhani atakuwa kama baba yake kwa kiasi fulani akikua??
au unadhani baba kuwa hivyo ita muaffect vipi(mtoto) katika maisha yake??
 
Da Asha asante sana mwaya
kwa kujibu maswali yangu ipasavyo

kitu kimoja tu ambacho nataka kugusia ni hapo kwenye harassment
mimi nilikuwa sana sana naelekea kwenye sexual abuse upande wa kifamilia
sio hiyo ya kujitakia ila ya mtu anakamatwa sema na mjomba wake au house
girl anakamatwa na baba mwenye nyumba lakini hasemi kitu ..

just roughly ukikutana au ukigundua mtu wa namna hii wewe kama wewe
utamsaidia vipi au utampeleka wapi apate msaada kama wewe huwezi
na utamfarijiri vipi...??

samahani kama nimekukaza sana ni kwa benefit ya wengi wakusomao..
asante

In red.. Asante kwa kunielewesha hilo...Hivyo Noted.

In nyeusi bolded... Bahati nzuri au mbaya huwa katika jamvi ni vigumu kumfahamu mtu vizuri because hua tunaanika yale ambayo tuko comfortable to admit... Nikisema hua sikubali kitu kama hicho (hasa mambo yamhusuyo mwanamama underpreviledged na children) kikifanyika na am aware nikae kimya - hope you believe...Nasema hivi sababu katika hili suala la sexual abuse na molestation ni suala ambalo liko saana katika jamii but kwa kujificha mno, maeneo ninayoishi yaweza changia nisishudie mara kwa mara but ukweli unabaki kua ni wengi.... Kitu kama hicho kimetokea na najua si rumors ni kweli kabisa hata kama hio family siwafahamu nitaingilia kati mana siwezi condone...Kuingilia kunategemea mambo mengi tokana na jamii yetu jinsi ilivyo, wahusika ni wanafamilia ama si wanafamilia, victim ana ndugu ama hana ndugu au mtu wa kum-support, victim anataka iwe reported ama lah! Umri wa huyo victim ni under 14, under 18 au over that age... Hivyo vitu ndio vita determine ni namna gani naweza msaidia - kwamba imekaa kifamilia au ki chombo husika....

Kuhusu kukwazika AD mtu ukija katika jamvi hili la GT ukifikiri unajua kila kitu na what you know ndo ukweli naamini kwa mtazamo wangu kua such a person has to be disqulified... Tunakutana na kupeana mawazo mbali mbali, tunaongeza maarifa, knowledge, tunagusia mambo ya jamii na most importantly kusikia maoni ya wengi ambao mtu lazima utatoka na moja kama si mawili.... Hivyo AD mimi napenda sana mtu kunirekebisha nilipokosea for that is how we become mo' knowledgeable and wise... Like i said before nimependa observation yako...
 
  • Verbal abuse (matusi),
  • Physical abuse (kimwili),
  • Sexual abuse(unyanyasaji wa ngono,)
  • (Neglect)kutelekezwa)
  • Hate (chuki)

Ni vitu ambavyo viko sana kwenye jamii yetu
ni vitu ambavyo vinatokea kila saa, tonaona jinsi watoto wetu
wanavyo danganywa na wazee wazima, tunaona jinsi mama zetu
wanavyopigwa na kutukanwa, tunaona jinsi watu wanavyotengwa na jamii
sababu ya vitu wanavyofanya au jinsi walivyo na ambayo ipo kila sekunde
ni sisi kwa sisi kuchukiana .

wandugu ningeomba sana leo tuongelee hizi Dhuluma..

Nini kinampeleka mtu kufanya haya mambo??
Je kila afanyaye haya mambo ni mtu mmbaya??
na ni vipi tunaweza kuwasaidia waliokuwa kwenye hizi
situation .... You are more than welcome to share anything....

(samahani wakuu ningeomba sana tutumie lugha ya kiswahili na English kidogo)

(ili kila mtu aelewe )
AD
AD yote tisa,mi ugomvi wangu ni hapo kwenye red,yaani kila kukicha dhulma zote ni sisi kina baba tunawatendea mama zenu,ya kweli hayo? Mangapi ya ajabu na kusikitisha kina mama wanawatenda waume zao wengine hadi kuwasababishia vifo tena wakati mwingine wakishirikiana na mabinti zao?
 
.......................................................................................................................................................

ASHA D UPO SAHIHI KABISA KABISA,
NA UMENIKUNA SANA HAPO KWENYE MFANO WAKO (RED),
MANAKE US NI MR NA MRS PERFECT HAWANA MAKOSA KABISA,ILA WAO SIKU ZOTE WANAONA MAKOSA YANAYOFANYWA NA WENZAO TU, PIA WANAJIONA KUWA NI WAO PEKE YAO NDIYO WENYE RUHUSA YA KUTOA ADHABU KWA WAKOSAJI. NA HAKUNA ADHABU NYINGINE ANAYOSTAHILI MKOSAJI ZAIDI YA KIFO......LAKINI NAAMINI KUTOKA NDANI YA MOYO WANGU KUWA IPO SIKU WATAONA MAKOSA YAO NA KUYAKUBALI KULIKO HIVI SASA AMBAPO JAPO WANAYAONA MAKOSA YAO LAKIN HAWAYAKUBALI...HAIJALISHI WATAKUWA WABABE KWA MIAKA MINGAPI LAKINI NAAMINI IPO SIKU ITAFIKA MWISHO WA UBABE WAO.

Maovu/matendo yote mabaya/huo ubabe/uonevu YOTE YANA CHANZO CHAKE,SABABU ZAKO,
VICHOCHEO vyake, ambavyo VIPO KATIKA JAMII zetu, na hata vinapoanza kujitokeza tunavidharau na kushindwa kuvikemea, tunapoanza kuchukua hatua tunakuwa tumechelewa au tunachukua hatua ya kutibu/kuzua maua badala ya kushughulikia mizizi yake.

nnunu... nini naweza ongea hapa....I AM ALWAYS IN AGREEMENT WITH YOU... Asante kwa ile fidbak.
 
hapo kwenye red hivi kama watu wameoana na wanaishi
pamoja kwa muda lakini kila mara mmoja hajisikii kufanya sex
na mwingine akawa anamlazimishia na mara nyingine kumwingilia
kwa nguvu Je waweza sema hiyo ni abuse??

sante mpenzi kwa majibu yako ya kuaminika ...

Unajua AD maisha ya ndoa are very complicated si straight forward kama wengi wetu tunavyofikiria.............. kwa kuanzia tu ni vema kujua nini kinasababisha kwa mtendwa kutokuwa na hamu ya kusex na mume/mke wake kabla ya kumuhukumu mume/mke aliyeforce sex. Kuna mengi hapo huchangia and we have to be makini kutohukumu pasipo kuanalyse yalotokea au sababisha

Definetly it is not acceptable kuforce sex from your spouse ...not at all BUT...kama kweli unampenda and you deny him/her of sexual pleasure unategemea akapate wapi?.......to some extent.......kama hujui chanzo its better not to jump into conclusion......sometimes it is better to be bakwad (kistaarabu lakini) by your hubby/wifey than letting him go and quench his thirst somewhere else....kama huna sababu ya msingi ya kudeny him of his righ.(Mkinishambulia mnishambulie tu)
 
Punishment ya kawaida ni kukemea,kukaripia,kofi moja wak sio mbaya ni adhabu ya kawaida,kumlaza mtoto njaa,kumfunga mikono ukamchoma moto eti kaiba sumni,kumtandika mtoto hadi vitako vikachanika,kumchezea mtoto viungo vyake .....etc hiyo ni abuse,na abuse ZOTE ni punishable by law,anayefanya abuse akidakwa ajue atakula mvua tu.

my dear asante sana
simpe and well explained..

samahani kwa swali hili..
Je we unadhani kwa familia za hapa
kwetu Tanzania ni rahisi kwa mtu ku
report kitu kama hicho ???
 
hahahaha...nimependa topic yako sana. Lazima nikubali hapa kuwa mimi natumia verbal abuse sana, lakini sio kwa marafiki au ndugu bali kwa wafanyakazi wenzangu. Sijajua tatizo...nitachunguza zaidi kesho nikienda kazini...
 
daahhh
Hivi hii topic ni ngumu kiasi hicho???
naona kila mtu anakimbia mmmhh

Hii topic ina mambo mengi sana my dia
Yaani ni kama umekusanya mafaili ya ofisi tatu za Mamlaka za Kodi nchi za USA, China na Brazil halafu umeweka ktk kajidude kamoja kadogo (flash)

Kwanza naomba nikurekebishe kwamba Sexual Abuse tunatafsiri kwa kiswahili kama Unyanyasaji wa Kijinsia

hatari.jpg

Naomba sasa nielezee kisa kimoja cha Unyanyasaji wa Kijinsia.

Kuna mdada ana mtoto mmja ameolewa, ana miaka minne katika ndoa yake, alizaliwa miaka 24 iliyopita.
Yeye na mume wake walikua wana pendana sana na mpaka sasa mdada anasema bado anampenda tena sana mume wake.

Ananiambia, " Yaani CPU, siku hizi mume wangu kabadilika sana kiasi najuta hata kuolewa yaani kidogo kanitukana mara mshenzi mara mjinga mara ananitisha kunipiga kwa kusema mimi simjui vizuri ndio maana nashindwa kufanya atakavyo.

Ukweli ninachanganyikiwa mume wangu anakuwa kigeugeu anaweza akakwambia "mimi sipendi uvae nguo ndefu", ukivaa fupi kwa muda huo aliosema anafurahi sasa itokee siku nyingine akuambie tutoke ukivaa hiyo nguo fupi anaanza
" . . . . unaenda kumuonyesha nani? Unatakautongozwe kwani mimi sikutoshi? "
Ukivaa ndefu au suruali ananyamaza.

Juzi simu yangu ilijizima nikiwa salon iliyo nje ya uzio wa nyumba tunayo ishi. Akampigia rafiki yake akaja mpaka saloon nikaongea naye kupitia simu ya rafiki yake. Jamani hakutaka kukata simu mpaka muda wa kazi uishe, karudi home hakuna salam ananiambia "utanieleza uliko kuwa" huku anatafuta mkanda aanze shunghuli. Mimi nikamwambia mimi sijatoka hata gengeni sikwenda.

Siku hiyo ndipo alipo mwita mtoto wake mwenye miaka minne nilimkuta naye akamuuliza, ndipo mtoto akamwambia "mama leo hajaenda mahali zaidi ya saloon anako sema" mume wangu akaona aibu akaondoka.

CPU, hata sasa nikimuuliza kwa nini ananifanyia hivyo ananiambia nisimkumbushe anakasirika mpaka nashindwa hata kuendelea kumuuliza. Ni mengi lakini naomba unisaidie "
 
Tabia ni kama ngozi ya mwili na mtoto wa nyoka ni nyoka;
Hivi vitu vilikuweko toka enzi za babu yetu DAUDI kwani alimdhulumu askari wake mke tena akampeleka vitani ili auawe ndo aweze kumla mjane kwa raha zake.

Haya mambo ni takribani 95% ya mambo yatendekayo duniani, halafu 5% ni usamaria wema ambao usipokaa vizuri unapigwa changa la macho pia.
 
my dear asante sana
simpe and well explained..

samahani kwa swali hili..
Je we unadhani kwa familia za hapa
kwetu Tanzania ni rahisi kwa mtu ku
report kitu kama hicho ???
Oh dear siku hizi mbona watu wengi wamefungwa sana tu.Zamani jinai hizi zilikuwa haziadhibiwi kwa sababu ya ukimya wa jamii,siku hizi watu wameamka,wakiona mathalan mtoto kafanyiwa mbaya wanachofanya ni kumtonya mwandishi wa habari(wamejaa tele mitaani tunakoishi),akishaaandika tu kwenye gazeti/TV/radio -hasa kipindi cha clouds 'Leo tena' saa 3 asubuhi,Kova akisikia tu wangu wangu anatuma vijana wa kazi maana anajua kesho yake media itamdai mrejesho.
 
Haya nimerudi sasa ....
Well kuna sababu nyingi zinaweza kumfanya mtu awe mnyanyasaji.....internal na external factors hapa zote zinahusika!!

Kujiweka juu-mtu ambae yupo kwenye kundi hili ni yule anaemnyanyasa mwenzake ili yeye ajisikie kwamba ni zaidi yake.Anamchukulia
anaemnyanyasa kwamba ni DHAIFU na yeye ana nguvu.Mara nyingi watu kama hawa hua ni wadhaifu internaly kwahiyo
anatafuta wale walio wadhaifu zaidi yake ili aweze kujipa kile anachokosa ndani yake.

Lawama-Huyu ni yule ambae anatumia lawama kama kigezo cha kumnyanyasa mwingine...yani yeye haoni anakunyanyasa kwasababu
WEWE NDO UMESABABISHA.Hawa ni wale wa usiingefanya kitu flani haya yote yasiingetoea...

Visingizio-Huyu hata siku moja hawezi kusema samahani nilichofanya ni kosa ila atakwambia yote ilikua ni hasira tu....kazini wameniboa..
nilishindwa kujizuia....yani hawa wanatumia hisia zao zisizohusiana na mhusika kumnyanyasa mhusika!!

Kubadili maoni-Hawa ni wale ambae kitu kisipoenda vile alivyotarajia/taka yeye ataanza kumkashifu mwenzake kwa maneno ili ajisikie
vibaya.Mara nyingi ndo wale unaosikia wanarudishiwa kwamba wasemacho ni maneno ya mkosaji....yani kilichokua kizuri
kikiwa sio chake kinakua kibaya.Ndo unakuta watu wameachana alafu mmoja anaanza kumnyanyasa mwenzake kwa
maneno ''ahh mtu mwenyewe mbaya...sura kama mbuyu na kadha wa kadha.

Umiliki-Mnyanyasaji anasikia raha ya kummiliki mnyanyaswaji pale mnyanyaswaji anapokubali kunyanyaswa....

Hasira za haraka-Hawa ni wale ambao mikono yao na maneno yasiyo mazuri yanawatoka haraka sana.Yani hawezi kudhibiti hasira zake kiasi kwamba hafikirii anachokifanya mpaka baadae wakati ameshaharibu tayari.Hii unaweza kusema hua haitokea kwa kukusudia maana wengi wao hua wanajuta baadae.

Kisasi-Kuna watu ambao wamewahi kunyanyaswa kwahiyo ile hasira anayotembea nayo anamtolea yeyote ili kujipa yeye unafuu.Na hii inamfanya asijione mdhaifu....

Chuki-Hii wala haihitaji ufafanuzi.Mtu akikuchukia anaweza fanya chochote kukuumiza iwe kwa maneno au kwa matendo.

Kwa sababu hizo hapo juu unaweza kuona kabisa wengine wananyanyasa wenzao kwa makusudi na faida binafsi na wengine wanashindwa kujidhibiti kwasababu wana matatizo yaliyoko ndani zaidi kwahiyo sio wanyanyasaji wote ni wabaya kwa maana ya kwamba sio wote wanachagua kua walivyo.
Kuwasaidia ni ngumu sana especially wale wanaofanya kwa makusudi.Na ugumu upo kwenye kujua kama kweli mtu anpofanya vile anakua hajakusudia maana wengi hua wanaishia kulaumu kitu kingine au watu wengine zaidi ya wao binafsi. Kumsaidia inabidi ujue chanzo cha ile tabia na yeye mwenyewe atake kubadilika....siku zote huwezi kumbadili mtu kwa lazima kwahiyo inabidi mhusika mwenyewe aseme kweli sipendi kua hivi na nasikia uchungu kwa ninayo/niliyofanya.
Ikiwa anataka kubadilika kwanza inabidi ajitambue yeye kama mnyanyasaji ....ajichunguze ndani yake kujua sababu na awe anajutia matendo/maneno yake.Ikifuatiwa na kumfanya ajisikie vile anavyofanya wenzake wajisikie...hii itamfanya ahisi huruma....alafu kutokana na majuto yake ajue kwamba anapofanya vile haimsaidii hata yeye maana at the end of the day anaishiia kulilia msamaha.Baada ya hapo aface hicho kinachomfanya awe vile ili aweze kuondokana nacho.

dahhh
asante sana kweli
umeelezea kwa kina na kirefu sana asante
nilichogundua hapa unasema kwamba hao watu wanao abuse wengine
wanafanya hivyo ili kujitosheleza walichokosa au kufurahisha nafsi zao..

Je unadhani mtu wa namna hiyo
ataweza kuacha hayo mambo peke yake
au anahitaji some series Help??
 
  • Verbal abuse (matusi),
  • Physical abuse (kimwili),
  • Sexual abuse(unyanyasaji wa ngono,)
  • (Neglect)kutelekezwa)
  • Hate (chuki)

Ni vitu ambavyo viko sana kwenye jamii yetu
ni vitu ambavyo vinatokea kila saa, tonaona jinsi watoto wetu
wanavyo danganywa na wazee wazima, tunaona jinsi mama zetu
wanavyopigwa na kutukanwa, tunaona jinsi watu wanavyotengwa na jamii
sababu ya vitu wanavyofanya au jinsi walivyo na ambayo ipo kila sekunde
ni sisi kwa sisi kuchukiana .

wandugu ningeomba sana leo tuongelee hizi Dhuluma..

Nini kinampeleka mtu kufanya haya mambo??
Je kila afanyaye haya mambo ni mtu mmbaya??
na ni vipi tunaweza kuwasaidia waliokuwa kwenye hizi
situation .... You are more than welcome to share anything....

(samahani wakuu ningeomba sana tutumie lugha ya kiswahili na English kidogo)

(ili kila mtu aelewe )
AD

Pole kwa kutendwa
 
In red.. Asante kwa kunielewesha hilo...Hivyo Noted.

In nyeusi bolded... Bahati nzuri au mbaya huwa katika jamvi ni vigumu kumfahamu mtu vizuri because hua tunaanika yale ambayo tuko comfortable to admit... Nikisema hua sikubali kitu kama hicho (hasa mambo yamhusuyo mwanamama underpreviledged na children) kikifanyika na am aware nikae kimya - hope you believe...Nasema hivi sababu katika hili suala la sexual abuse na molestation ni suala ambalo liko saana katika jamii but kwa kujificha mno, maeneo ninayoishi yaweza changia nisishudie mara kwa mara but ukweli unabaki kua ni wengi.... Kitu kama hicho kimetokea na najua si rumors ni kweli kabisa hata kama hio family siwafahamu nitaingilia kati mana siwezi condone...Kuingilia kunategemea mambo mengi tokana na jamii yetu jinsi ilivyo, wahusika ni wanafamilia ama si wanafamilia, victim ana ndugu ama hana ndugu au mtu wa kum-support, victim anataka iwe reported ama lah! Umri wa huyo victim ni under 14, under 18 au over that age... Hivyo vitu ndio vita determine ni namna gani naweza msaidia - kwamba imekaa kifamilia au ki chombo husika....

Kuhusu kukwazika AD mtu ukija katika jamvi hili la GT ukifikiri unajua kila kitu na what you know ndo ukweli naamini kwa mtazamo wangu kua such a person has to be disqulified... Tunakutana na kupeana mawazo mbali mbali, tunaongeza maarifa, knowledge, tunagusia mambo ya jamii na most importantly kusikia maoni ya wengi ambao mtu lazima utatoka na moja kama si mawili.... Hivyo AD mimi napenda sana mtu kunirekebisha nilipokosea for that is how we become mo' knowledgeable and wise... Like i said before nimependa observation yako...

I am super impressed with your answer
very smart thank you so much..
one more thing hapo kwenye red
Hivi kweli inajalisha kama anataka au la??
kama mtu yuko kwenye abuse relation na
anampenda sana mumewe na akisema
hataki u report na we unajua sana hali si nzuri
hivi kweli itajalisha hapo??
 
AD yote tisa,mi ugomvi wangu ni hapo kwenye red,yaani kila kukicha dhulma zote ni sisi kina baba tunawatendea mama zenu,ya kweli hayo? Mangapi ya ajabu na kusikitisha kina mama wanawatenda waume zao wengine hadi kuwasababishia vifo tena wakati mwingine wakishirikiana na mabinti zao?

my dear samhani sana
ila huo ni mfano tu ..
na nimeweka hivyo maana
ni majority (wanawake na watoto)
mara nyingi lakini kweli kuna
wanawake wengine ni sumu pia..
samahani kama nimekukwaza
 
Unajua AD maisha ya ndoa are very complicated si straight forward kama wengi wetu tunavyofikiria.............. kwa kuanzia tu ni vema kujua nini kinasababisha kwa mtendwa kutokuwa na hamu ya kusex na mume/mke wake kabla ya kumuhukumu mume/mke aliyeforce sex. Kuna mengi hapo huchangia and we have to be makini kutohukumu pasipo kuanalyse yalotokea au sababisha

Definetly it is not acceptable kuforce sex from your spouse ...not at all BUT...kama kweli unampenda and you deny him/her of sexual pleasure unategemea akapate wapi?.......to some extent.......kama hujui chanzo its better not to jump into conclusion......sometimes it is better to be bakwad (kistaarabu lakini) by your hubby/wifey than letting him go and quench his thirst somewhere else....kama huna sababu ya msingi ya kudeny him of his righ.(Mkinishambulia mnishambulie tu)

hahahahaahahaha lol
MJ1 bwana hapo kwenye red
umenichekesha kwa kweli lahhh

Nway leo tunaongela kuhusu hizo dhuluma tu..
mambo ya ndoa sintoingilia sana leo..ila nashukuru sana
na asante sana kwa majibu yako ya kistaarabu na ya kueleweka..

naacha kukuchimba maswali sasa hahahahhaah lol
lakini ukipata cha kuongezea au kusema
your more than welcome...
sante sana dada mzuri
God bless
 
hahahaha...nimependa topic yako sana. Lazima nikubali hapa kuwa mimi natumia verbal abuse sana, lakini sio kwa marafiki au ndugu bali kwa wafanyakazi wenzangu. Sijajua tatizo...nitachunguza zaidi kesho nikienda kazini...

mmmmhhhhhh
we ni fujo nyingi tu
mi si nakujua wewe
hahahaaahh lol

Hivi wana respond vipi kwako
pale unaporopoka kama uji wa ugali
hahahahha lol
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom